.

.

.

.

Saturday, March 31, 2012

DIAMOND AKATAA KUTUNZWA NA WEMA NA KUMFANYA MREMBO HUYO KUTOKWA NA MACHOZI


Wema Sepetu akiwa na tabasamu akijaribu kumtunza wa KUMOYO wake wa zamani bila mafanikio katika shoo ya Nasseb Diamond iliofanyika jana usiku Mlimani City
Jamaa bado kala Kobisi
Basi isiwe tabu ...... wema akiondoka macho chini baada ya sakata hilo
Wema akilia huku Mashosti zake wakijaribu kumtuliza

Friday, March 30, 2012

BREAKING NEWS : FABRICE MUAMBA TODAY


It's the picture the world has been waiting to see.
Fabrice Muamba sits up in his hospital bed wearing a wide smile almost two weeks after collapsing mid-way through a match.
The footballer's fiance Shauna Magunda posted the heart-warming image earlier today to say thank you to the millions of fans who have supported her partner after he suffered a near fatal heart attack.
It shows the Bolton FC star wearing a blue hooded sports top and lying back in his hospital bed. His smile shows the miraculous recovery he has made since the game on March 17.

JOAKINA DE-MELLO APEWA TUZO YA MWANAMKE JASIRI TANZANIA

Mwanamke Jasiri Tanzania 2012, Bi. Joaquine De-Mello akitoa neno la shukrani baada ya kupokea tuzo.
Kaimu Balozi wa Marekani hapa nchini, Robert Scott akikabidhi Tuzo ya Mwanamke Jasiri Tanzania 2012, Bi. Joaquine De-Mello.
De-Mello akiwa katika mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) ambaye ni mmoja kati ya waliowahikupata tuzo kama hiyo Mwaka 2010, Bi. Ananilea Nkya (kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Under The Same Sun (UTSS) Tawi la Tanzania, Bi. Vicky Ntetema (kulia).

Wednesday, March 28, 2012

HILI NDILO TATIZO LA TANESCO

SHIRIKA la Umeme Tanzania (TANESCO), linadaiwa sh. bilioni 269 na Kampuni ya Kufua Umeme ya Aggreko ikiwa ndio sababu ya shirika hilo, kushindwa kutoa huduma ya umeme kwa ufanisi. Kutokana na deni hilo, Kampuni ya Aggreko imelazimika kuzima mitambo yake baada ya kukosa fedha za kununulia mafuta yanayotumika kuendeshea mitambo. Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini, Bw. January Makamba, aliyasema hayo Dar es Salaam jana wakati akizungumza na waandishi wa habari. Bw. Makamba alisema, Serikali iliombwa kuikopesha TANESCO sh. bilioni 408, lakini fedha hizo hadi sasa hazijatolewa ili kusaidia kulipa deni hilo. “Hata kama TANESCO watapewa hizi fedha, kwanza tunapaswa kulipa deni la sh. bilioni 269 na kiasi ambacho kitabaki hakitoshelezi kununua mafuta ya kuendeshea mitambo hii,” alisema. Alisema Kampuni ya Aggreko ilizima mitambo yake tangu Desemba 2011 kwa sababu ya kukosa fedha za kununulia mafuta ya kuendeshea mitambo. “Kimsingi tatizo la mgawo wa umeme litarrudi kama zamani kutokana na vyanzo vya maji ambavyo vinatumika kuzalisha umeme kupungua, kwa sasa umeme tunaopata unatokana na vyanzo hivi. “Maji yaliyopo kwenye mabwawa ni kidogo, ikifika Agosti mwaka huu itakuwa kipindi cha kiangazi sasa hali itakuwa mbaya zaidi, njia pekee ya kuondokana na tatizo hili ni kuharakisha ujenzi wa bomba la gesi ambalo Rais Jakaya Kikwete alitoa tamko lijengwe kwa miezi 18 tangu 2011,” alisema Bw. Makamba. Alisema kukamilika kwa bomba hilo, kutaondoa mgawo kwani umeme wa uhakika utakuwa ukipatikana muda wote. “Kama tutaendelea kuzalisha umeme kwa kutegemea mafuta, nchi yetu itaelekea kubaya kwani gharama za mafuta zinaongezeka siku hadi siku,” alisema. Kuhusu utaratibu mpya wa kuagiza mafuta kwa pamoja ambao umeanzishwa hivi karibuni kwa Sheria ya Bunge, Bw. Makamba alisema haujasaidia kupunguza bei ya nishati kama ilivyotarajiwa. Akizungumza na wadau wa mafuta, Bw. Makamba alisema hivi sasa kamati yake itakaa na kupitia upya kanuni na sheria ili kuangalia njia mbadala za kupunguza bei ya nishati hiyo kama ilivyokusudiwa. Alisema kati ya kampuni zilizokubaliwa kununua mafuta kwa pamoja, hadi sasa zabuni mbili zimeagizwa na mara ya kwanza ilikuwa Januari na Februari. Aliongeza kuwa, kipindi hicho ziliingia meli 16 zenye shehena ya mafuta ambapo awamu ya pili ilikuwa iwe Machi na Aprili mwaka huu kwa kuingia meli 17 lakini hadi sasa zimeingia meli mbili tu. Bw. Makamba alisema meli zimekuwa zikichelewa tofauti na walivyokubaliana kuwa zitaingia zote ambapo changamoto iliyopo ni bei ambayo haijashuka. Kwa upande wake, Ofisa Mwandamizi wa Masoko kutoka Shirika la Maedeleo ya Petroli nchini (TPDC), Bw. Leo Lyayuke, alisema hivi sasa wanakabiliwa na changamoto nne. Changamoto hizo ni kampuni za kuagiza mafuta, upatikanaji wa zabuni, ongezeko la bei na uchelewaji wa meli. Wakati huo huo, Kaimu Mkurugenzi Idara ya Petroli wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Bw. Godwin Samuel, alisema imebainika baadhi ya mafuta yanayoingizwa nchini hasa petroli hayana ubora wa kutosha. Alisema kutokana na hali hiyo, hivi sasa wanachukua sampuli ya mafuta yanayobaki bandarini na kuyapeleka kwa Mkemia Mkuu wa Serikali ili kubaini yana matatizo gani

Monday, March 26, 2012

ZAWADI YA PASAKA TOKA KWA REBECCA MALOPE

MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca Malope, ameahidi kuwaletea Watanzania zawadi ya Pasaka atakapotumbuiza katika tamasha la nyimbo za Injili la Pasaka litakalofanyika Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Akizungumza jana kwa njia ya simu kutoka Afrika Kusini, Rebecca alisema amewaandalia zawadi nzuri mashabiki wa muziki wa Injili wa Tanzania, na akatoa mwito wajitokeze kwa wingi siku ya tukio ili kumshuhudia. "Naahidi kuwaletea Watanzania zawadi ya Pasaka... nimewaandalia vitu vipya ambavyo naamini watavifurahia," alisema Malope. Malope aliyezaliwa katika shamba la tumbaku Afrika Kusini, alisema katika tamasha hilo la Pasaka mwaka huu ataimba nyimbo mbalimbali zilizomo kwenye albamu zake. Rebecca amewahi kutamba na albamu za Saturday Nite (aliyoitoa Januari 1, 2009), Hlala Nami (Novemba 11, 2003), Siyabonga (Desemba 21, 2000), Free at Last (Novemba 18, 1997), African Classics (Mei 5, 2009) na Greatest Hits (Januari 10, 2006). Malope atakuwa mmoja kati waimbaji siku hiyo wakiwemo Rose Muhando, Solomon Mukubwa, Anastazia Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Atosha Kissava, Mwinjilisti Faraja Ntaboba, Ephraim Sekeleti, Maryanne Tutuma, kundi la Glorious Celebration na kwaya ya Kinondoni Revival. Mwenyekiti wa Kamati inayoratibu tamasha hilo chini ya Kampuni ya Msama Promotions ya Dar es Salaam, Alex Msama, alisema Rebecca ataungana na waimbaji wa muziki wa Injili kutoka nchi jirani za Zambia, Kenya na Jamhuri ya Kidemokrasia na Congo (DRC). Mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe. Baada ya kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu ambako mgeni rasmi atakuwa Naibu Spika, Job Ndugai. Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane. Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000.

GAZETI LA IJUMAA WIKIENDA LEO


Saturday, March 24, 2012

AONYA WANAOKUZA MAKALIO ( WOWOWO)

WANAWAKE wanaotumia dawa au kuchoma sindano kuongeza makalio na viungo vingine vya mwili wametahadharishwa kuwa wanaweza kupata ugonjwa wa saratani. Aidha, wanawake wanaotumia mashine kutaka kusimamisha matiti wametahadharishwa huenda wakashindwa kunyonyesha watoto baadaye wakati wanaotumia vifaa maalumu kuridhisha hamu zao za kimapenzi wameelezwa kuwa wataathirika kisaikolojia. Daktari Ali Mzige akizungumza na HabariLeo Jumapili katika mahojiano maalumu yaliyozaa habari hii, alisema anashangazwa na wanawake na mabinti wa Kitanzania wanaohangaika kunywa dawa na kuchoma sindano kwa lengo la kuongeza makalio au sehemu zingine za viungo vya miili yao huku wakihatarisha afya zao, ikiwa ni pamoja na kupata saratani bila kujua. Mzige alisema wako wanawake wengine wanatumia vifaa maalumu ili kujiridhisha kimapenzi na kwamba wanaotumia vifaa hivyo huathirika kisaikolojia bila kufahamu na ndio hao baadaye wanakataa hata kuolewa kwa sababu tayari wameathirika. “Wanawake hawafahamu wanaiga tu, huko Ulaya wanaofanya mambo haya ya ajabu ni waathirika wa dawa za kulevya au tayari unakuta wameathirika kisaikolojia, lakini sisi tunataka kuiga tu k la kitu badala ya kutumia vitu vya asili,” alisema. Dk. Mzige ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya IMTU, alisema haoni makalio makubwa yanawapa faida gani wanawake na kwamba uvutaji wa matiti una husisha uvutaji wa misuli inayoshikilia nyama za matiti na matokeo yake baadaye mhusika anakuja kushindwa kunyonyesha mtoto. “Wanawake msidanganyike na vidonge, sindano mnaweza kupata saratani. Hivi ukirefusha matiti, maziwa yatoka wapi ukitaka kunyonyesha, acheni kuharibu afya zenu bila sababu,” alisema. Aliwataka wanawake kuacha kufanya mambo hayo kwa ajili ya kuridhisha watu wengine na kuharibu asili ya mwanamke wa Kitanzania na kuongeza kuwa kama wanawake wanataka kulinda uhalisia wao waache kutumia vitu vikali kama pombe, sigara na badala yake wale vyakula vyenye kujenga mwili. “Kama hutaki kuzeeka haraka acha kunywa pombe, kuvuta sigara, fanya mazoezi na kula vizuri. Ikumbukwe pombe na sigara hupunguza CD4… sijui kama watu wanafahamu kuna baadhi ya vitu ndani ya pombe au sigara mwisho hutumika kutengenezea dawa ya kuhifadhia maiti. “Haya mambo ya kutaka urembo kupita kiasi ndio yalisababisha mke wa Rais wa zamani wa Nigeria, Olesegun Obasanjo,Stella kufa hivi hivi akitafuta urembo wa bandia…unajiuliza mama kama huyu alikuwa na kila kitu amekwenda kufanya nini, ndio hayo ninayoeleza anakuwa tayari ameathirika kisaikolojia,” alisema. Mke wa Obasanjo alikufa wakati akifanyiwa operesheni nchini Hispania akipunguza unene. Alisema siku hizi wanawake wengi wanapopata ajali za magari unakuta ni kwa sababu ya ulevi na wengine ndani ya magari unakuta chupa za pombe kwa maana kwamba wanawake wanakunywa sana vilevi ambavyo baadaye vinaharibu afya zao na wanajiona kama hawapendezi tena na matokeo yake wanakwenda kujitengeneza kwa vitu bandia. Dk. Mzige alisema pia tatizo la umasikini limechangie wanawake kujiingiza katika mambo yasiyofaa, ikiwa ni pamoja kuingiliwa kinyume cha maumbile, jambo alilolielezea kuwa ni baya na linaathiri kwa kiasi kikubwa mfumo wa uzazi wa mwanamke. Alioonya mabinti kuacha kuendekeza umasikini na kujiingiza katika vitendo hivyo visivyofaa kwani madhara yake kiafya ni makubwa na sio utamaduni wa wanawake wa Kitanzania. Hivi karibuni gazeti moja liliripoti kuwepo kwa huduma ya kusimamisha matiti inayofanyika katika Saluni mmoja iliyopo Sinza, jijini Dar es Salaam na mteja hulipia kuanzia Sh 150,000. Habari hiyo ilitaja amshine hiyo kuwa inatiwa ‘Beauty Machine’ na kwamba ina uwezo wa kusimamisha matiti ya kila saizi na kwamba kazi kubwa ya mashine hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti.

Friday, March 23, 2012

MH.SEIF SHARIF HAMAD ATEMBELEA MASJID ASWABIRINA

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad akiongozana na viongozi mbali mbali wa dini ya Kiislam alipotembelea ujenzi wa Masjid Aswabirina katika mtaa wa Kitunda Mzinga Dar es Salaam. Kushotoni kwake ni Amiri Mkuu wa taasisi za kiislamu nchini Sheikh Mussa Kundecha na kuliani ni Kadhi wa Kariakoo Sheikh Ally Basaleh.Picha na Salmin Said-Ofisi Ya Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar --- Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema jamii inahitaji vijana waliojengeka kifikra na maadili mema, hivyo kuna haja kwa vijana kuweka mkazo katika kutafuta elimu yenye manufaa kwao na jamii kwa jumla. Maalim Seif ametoa kauli hiyo katika mtaa wa Kitunda Mzinga Dar es Salaam, alipokuwa akizindua harambee ya kuchangia ujenzi wa Masjid Aswabirina katika mtaa huo. Amesema msikiti ni kituo muhimu cha kutoa elimu kwa jamii na kuijenga kimaadili, hivyo ametoa wito kwa waislamu kuchangia ujenzi huo ili uweze kukamilika kwa wakati. Amewashukuru wakaazi wa eneo hilo kwa kuanzisha ujenzi huo ambao utasaidia maendeleo ya dini ya kiislamu. Kabla ya uzinduzi huo, Makamu wa Kwanza wa Rais alitembelea skuli ya sekondari ya LILASIA katika mtaa huo ambako alielezwa maendeleo na changamoto zinazoikabili skuli hiyo iliyoanzishwa miaka michache iliyopita. Maalim Seif ameahidi kuchangia shilingi milioni mbili (mil. 2) kwa ajili ya ujenzi wa msikiti huo, na shilingi milioni moja (mil.1) kwa ajili ya skuli hiyo, sambamba na kukubali kuwa mshauri na mlezi wa msikiti huo. Mapema akizungumza katika hafla hiyo, Kadhi wa Kariakoo jijini Dar es Salaam Sheikh Ally Basaleh, amewataka waislamu kuacha tabia ya kuiga na kufanya ibada kwa kufuata mkumbo, na badala yake watafute elimu ili kutekeleza ibada zao kwa uhakika. Amiri Mkuu wa kijiji hicho cha Kitunda Mzinga sheikh Khatib Yunus amesema wanakusudia kuufanya msikiti huo kuwa kituo cha taaluma na misaada kwa jamii, ambapo wanakusudia kuwasaidia mayatima 41, wajane 9 na wazee wasiojiweza katika kijiji hicho, sambamba na kuanzisha madrasa kwa ajili ya akinamama. Kiasi cha shilingi milioni mia mbili zinahitajika kwa ajili ya kukamilisha ujenzi huo ambapo hadi sasa zaidi ya shilingi milioni nne na nusu zimeshatumika. Hafla hiyo ilihudhuriwa na viongozi mbali mbali wa dini ya kiislam akiwemo Amiri Mkuu wa taasisi za kiislamu nchini Sheikh Mussa Kundecha. Na Hasssan Hamad Ofisi Ya Makamu Wa Kwanza Wa Rais Zanzibar

MSOSI .............

Raha ya wali kuwepo na ndizi mbivu pembeni
Hapo huniondoi

MNAKARIBISHWA


MILLEN MAGESE ZOEZI LA KUTAFUTA WANAMITINDO WAWILI

Mwanamitindo wa kimataifa wa Tanzania, Millen Happiness Magese ataendesha zoezi la kutafuta wanamitindo wawili (kwa vijana wa kike na kiume) watakoshiriki kwa mara ya kwanza katika maonyesho ya wiki ya Mavazi ya Afrika Kusini (South Africa Fashion Week) tarehe 1 April mwaka huu. Millen atafanya zoezi hilo kupitia kampuni yake ijulikanayo kwa jina la Millen Magese Group Company Limited chini ya mpango wake wa kuitangaza Tanzania kupitia fani ya mitindo (Tanzania International Fashion Exposé (TIFEX). Alisema kuwa wanamitindo wanaotaka kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika SAFW kufika siku ya Jumapili tarehe 25 mwezi huu kwa ajili ya mchujo huo kuanzia saa 8.00 mchana kwenye hotel ya Serena. Alifafanua kuwa anaamini kuwa wanamitindo wa Tanzania watakaopatikana katika zoezi hilo wataiwakilisha Tanzania vyema katika wiki ya maonyesho ya mavazi ya Afrika Kusini na kuitangaza Tanzania kimataifa kama anavyofanya yeye kwa hivi sasa. Alisema kuwa hiyo ni fursa pekee kwa wanamitindo kuweza kujitangaza wenyewe kimataifa na kufuata nyayo zake. Alifafanua kuwa wanamitindo wanaotakiwa kufika katika zoezi lazima wawe na vigezo vifuatavyo:- Umri miaka 18 mpaka 24, urefu 1. 75m, hips 37cm (ukiwa na nywele zako za asili) na kwa wanaume urefu ni 1.82m. “Naamini kuwa zoezi hili litawanufaisha wana mitindo wa kike na wa kiume wa Tanzania na vile vile ushiriki wao katika SAFW na katika maonyesho mengine ya mavazi nje ya Afrika na kusaidia kuitangaza nchi kimataifa,” alisema Millen. Alisema kuwa lengo kubwa la kampuni yake ni kuendeleza fani ya uanamitindo na vile vile kuitangaza Tanzania nje ya mipaka yake kwa kupitia fani ya mitindo na hata kwa njia ya utalii. Aliongeza kuwa japo Tanzania ina wanamitindo wengi na wabunifu, bado kuna pengo kubwa ukilinganisha na maendeleo ya fani hiyo katika nchi ya Afrika Kusini na Nigeria. Alisema kuwa nchi hizo zimepiga hatua kubwa sana na yeye kuhamasika kuanzisha kampuni yake iliyozinduliwa mwezi Machi mwaka jana kwa lengo la kuziba pengo hilo na kuleta maendeleo ili wahusika wafaidike na matunda ya fani yao. Majaji wa zoezi hilo ni Ritha Poulsen, Mustapha Hassanali na Khadija Mwanamboka na katika kuwekea umuhimu zaidi mchakato huo, MMG imemkaribisha mwanamitindo maarufu, Aminat Ayinde kutoka America Next top model cycle 12 kushuhudia zoezi hilo lililodhaminiwa na Clouds FM na Benchmark production.

KOTA ZA GEREZANI KUVUNJWA !!!

NYUMBA 106 zilizopo katika eneo la Gerezani Kota- Kariakoo jijini Dar es Salaam zitaanza kubomolewa leo alfajiri baada ya Mahakama Kuu Kitengo cha Ardhi kutupilia mbali pingamizi la madai yaliyokuwa yamewasilishwa na wakazi wa eneo hilo tangu 2008. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadik aliwataka wananchi wa maeneo hayo kuondoka mapema na kuokoa mali zao kabla ya kubomolewa nyumba zao ili kupisha ujenzi wa kituo cha Mradi wa Mabasi ya Kasi (DART). Alisema kuwa awali Halmashauri ya Manispaa ya Ilala ilitayarisha mpango wa uendelezaji upya wa eneo hilo lililokuwa likimilikiwa na Shirika la Reli na Mamlaka ya Bandari na baada ya mpango huo kukamilika, ulitangazwa kwenye Gazeti la Serikali la Januari 25, 2002. “Katika juhudi za Serikali kufanikisha ujenzi wa kituo kwenye eneo hilo Aprili 8, 2008 ilitangaza kutwaliwa rasmi kwa eneo hilo kwa manufaa ya umma na kupangwa kujengwa kituo cha mabasi ya Dart, ilitangaza mwenye malalamiko, pingamizi au madai ajitokeze lakini hapakuwa na aliyejitokeza,” alisema. Alisema kutokana na hilo ilifanyika tahmini ya eneo hilo na zikatolewa Sh bilioni 2.7 kwenda Wakala wa Majengo (TBA) na familia 34 kati ya hizo 106 ndiyo zilizojitokeza kuchukua fidia zao lakini nyingine 72 ziligoma na kuungana kufungua kesi hiyo mahakamani. Alisema tangu kipindi hicho kesi hiyo imekuwa ikisikilizwa kwa kusuasua na wiki iliyopita Mahakama ilitupilia mbali shauri hilo lakini wakati Serikali ikijiandaa kuanza kutekeleza amri ya Mahakama ya kuwahamisha watu hao, wananchi hao walipeleka pingamizi lingine mahakamani Jumatatu wiki hii. “Pingamizi hili lilitupiliwa mbali juzi lakini baadaye wakapeleka tena na jana limetupiliwa mbali hivyo tunawataka wahame na ubomoaji utaanza alfajiri na utafanywa na Kampuni ya udalali ya Yono Auction Mart,” alisema.

Thursday, March 22, 2012

MESSI AWEKA REKODI MPYA

BARCELONA, Hispania

  Juzi LIONEL Messi alifunga mara tatu na kufikisha mabao 234 tangu ajiunge Barcelona na kuvunja rekodi ya mabao iliyowekwa miaka 60 iliyopita na mshambuliaji wa zamani wa timu hiyo Cesar Rodriguez (57).Messi (24) alipachika mabao hayo katika mechi ya Ligi Kuu Hispania dhidi ya Granada, ambapo Barcelona ilishinda 5-3 na hivyo kuipiku rekodi ya muda mrefu ya mabao 232 iliyowekwa na Rodriguez. Nyota huyo wa Argentina aliyecheza Barcelona kwa mara ya kwanza mwaka 2004, aliifikia rekodi ya Cesar kwa kufunga bao la kwanza kwa guu lake la kushoto katika dakika ya 17, kisha akafunga lingine dakika ya 67 na kuifanya Barca kuwa mbele kwa mabao 3-2. Aliongeza bao lake la tatu kwenye mchezo huo lililokamalisha kuvunja rekodi hiyo katika dakika ya 86 na hivyo kufikisha mabao 54 kwa msimu huu. "Kipa wa Barcelona, Victor Valdez alisema,"amethibitisha kwamba hizi ni zama zake." Kwa jumla, Messi ameshapachika kwenye kamba mabao 234 katika mechi 314 alizocheza Barcelona. Messi, mchezaji bora mara tatu wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) , amefunga mara 17 katika mechi saba zilizopita na anaongoza orodha ya wafungaji bora Hispania kwa kufikisha mabao 34, mawili mbele ya mshambuliaji wa Real Madrid, Cristiano Ronaldo. Katika mechi 45 alizocheza msimu huu, amefunga mabao 54.'Hat trick' ya Messi usiku wa kuamkia juzi, ilikuwa ya 18 tangu alipojiunga Barcelona na kufikisha mabao 154 katika mechi 153 zilizopita. Kana kwamba hiyo haitoshi, mabao matatu aliyofunga juzi ilikuwa ni mara yake ya sita kwa Barcelona msimu huu pekee na hivyo kufikia rekodi kama hiyo iliyowekwa na Ronaldo msimu uliopita. Kwa kiwango kikubwa anachoendelea kukionyesha msimu huu kinaweza kumfikisha hata rekodi ya kufunga mabao 70.Baada ya mechi ya juzi usiku, wachezaji wenzake Messi walimpongeza na kuongea mengi, akiwemo Pique. "Ni changamoto kubwa kuwa katika kizazi kama chake," alisema Pique na maelezo yake kuwekwa kwenye tovuti ya mawasiliano ya Barcelona. "Naamini yeye (Messi) ndiye mchezaji bora zaidi katika historia. "Haijalishi anacheza wapi, kwenye joto, baridi siku zote huonyesha ni kwa kiasi gani yeye bi bora." Andres Iniesta alisema,"ushindi mkubwa, hata kimchezo tunazidi kuongeza pointi. Hongera sana Leo, mfungaji mahiri wa Barca." Kocha wa Barca, Pep Guardiola aliwapongeza wachezaji wake katika mkutano wa baada ya mchezo. "Kuna wachezaji wachache wanaweza kutawala, lakini yeye anatawala. Unaweza kumlinganisha vizuri na Jordan," alisema Guardiola. "Tunaendelea kushuhudia mazuri kila wakati kutoka kwake. "Anafanya yote, na anafanya kila baada ya siku tatu."


 REKODI YA MABAO:
 •2007-08: 16 Magoli 
 •2008-09: 38 
 •2009-10: 47 
 •2010-11: 53 
 •2011-12: 54 mpaka sasa.

VIWANJANI WIKI HII

DIAMOND ASEMA KWA SASA YUKO SINGO

MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Naseeb Abdul ‘Diamond’ amesema kwa sasa yupo singo na kwamba hana papara ya kutafuta demu mwingine. Diamond amesema ameamua kutulia kwa muda kwa sababu mapenzi hayapangwi, bali hutokea kimiujiza kama ilivyo kwa ajali ya aina yoyote. Msanii huyo mwenye mvuto alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita kupitia kipindi cha Friday Night Live kilichorushwa hewani kupitia kituo cha televisheni cha Channel Five. Diamond alisema kwa kipindi kirefu sasa, amekuwa akikumbana na mikasa mingi inayohusu mapenzi, hivyo ameamua kutulia na kumuomba Mungu ampatie mpenzi mwema. Msanii huyo alielezea msimamo wake huo, kufuatia hivi karibuni kutengana na mpenzi wake wa siku nyingi, Wema Sepetu. Mbali na Wema, Diamond pia amekuwa akidaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wasanii wengi nyota wakiwemo Jokate Mwegelo na Irene Uwoya. “Kusema ule ukweli, kwa sasa sina mtu, nipo singo. Na siwezi kusema nitapata mpenzi mwingine hivi karibuni kwa sababu siku zote mapenzi huwa yanapangwa, hayaji kama ajali,”alisema msanii huyo, ambaye kwa sasa anatamba na kibao chake cha Mawazo. Alipoulizwa kuhusu kitu gani asichokipenda katika maisha yake ya usanii, Diamond alisema hapendi kuwaudhi mashabiki wake kwa vile wao ndio wanaomwezesha kuwa kwenye chati ya juu kimuziki. Alisema siku zote amekuwa akijitahidi kubuni vitu vipya kwa ajili ya kuwaburudisha mashabiki wake na kusisitiza kuwa, msanii asipokuwa mbunifu, ni rahisi mashabiki kumchoka. Diamond amemmwagia sifa kedekede prodyuza mahiri wa video za muziki nchini, Adam Juma kwamba ndiye aliyewainua wasanii wengi wa muziki wa kizazi kipya. “Siku moja nilikaa mahali na Adam Juma nikamwambia, ‘bradha ikitokea siku ukasema unaacha kazi hii ama ikatokea Mungu amekuchukua mapema, wasanii tutapata tabu sana,’” alisema Diamond. “Unaweza kutengeneza nyimbo ya kawaida, lakini ikabebwa na video. Adam ni mkali mno katika kutengeneza video za muziki wa kizazi kipya. Na video ndizo zinazoufanya muziki uonekane kuwa bora,”aliongeza. Ili kwenda na wakati, Diamond alisema kwa sasa, ameamua kuwa na mbunifu wake wa mavazi, ambaye amekuwa akimtengenezea mavazi ya aina tofauti. Alisema wasanii wanapaswa kuwa na mwonekano maalumu badala ya kuvaa mavazi yanayoweza kuwafanya waonekane wasela ama wahuni. “Msanii hapaswi kuvaa nguo za makabitini. Wapo wasanii wengine wenye pesa na uwezo mkubwa, lakini hawapendi kuvaa, lakini ukishakuwa mtu maarufu katika jamii, unapaswa kubadilika,”alisema.

Wednesday, March 21, 2012

ENZI HIZO POSTA ZETU TANZANIA


PERFECT LEGS ......................


She's proud of her body after losing a staggering five stone, and Jennifer Nicole Lee seems as keen as possible to show off the fruits of her labour. The personal trainer put her body fully on display over the weekend as she stepped out in a tiny green dress that left little to the imagination. The 36-year-old celebrated the St. Patrick's Day holiday on Saturday by wearing green in its honour.

Tuesday, March 20, 2012

MH.MWAKYEMBE AANZA KAZI OFISINI

NAIBU Waziri wa Ujenzi, Dk. Harisson Mwakyembe, amerejea rasmi ofisini na kuanza kazi huku akivitaka vyombo vya habari nchini kuachana na suala la ugonjwa wake, akisema sasa imetosha. Waziri huyo alikaa nje ya ofisi kwa takribani miezi mitano baada ya kuugua ugonjwa wa ngozi unaodaiwa kupukutisha ngozi yake na kukimbizwa India kwa matibabu. Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuingia ofisini kwake, Dar es Salaam jana, Dk. Mwakyembe alisema hali yake sasa inaendelea vizuri na ndiyo maana amerejea kazini. “Naomba nitumie fursa hii kuwaeleza wananchi kuwa nilikuwa naumwa kwa muda mrefu ugonjwa uliojulikana kitaalamu baada ya vipimo kama Populia Thrulema yaani matatizo ya ngozi, lakini sasa naendelea vizuri,” alisema Dk. Mwakyembe ambaye alionekana mchangamfu huku akiwa bila glovu mikononi kama ilivyozoeleka tangu aanze kuugua. Awali akiwasili eneo la ofisi za Wizara ya Ujenzi, alikutana na kundi la waandishi wa habari hali iliyomfanya ashuke haraka kwenye gari na kuingia ndani kwa mwendo wa kasi sana, huku akiishia kuwasalimia waandishi hao na kupanda ngazi akikimbia. Alirejea nchini Jumamosi kutoka India. Hata hivyo, baadaye alipozungumza na waandishi hao, aliviomba vyombo vya habari vipumzike kuandika na kuchokonoa kuhusu ugonjwa wake na badala yake waiachie Serikali ambayo imeunda tume kuchunguza chanzo cha ugonjwa huo, ikamilishe uchunguzi wake. “Naomba jamani sasa ugonjwa wa Mwakyembe ufike mwisho kuandikwa. Watu walitarajia na kusubiri mengine, lakini nawaambia mliotaka kuandika vichwa vya habari vya kifo changu mjue tafadhali niko hapa sijafa, naomba yaishe sasa,” alisema Dk. Mwakyembe. Alisema alipokuwa India kwa mara ya pili kuendelea na matibabu, alitaarifiwa kuwa suala la utata wa ugonjwa wake kuwa ama amelishwa sumu au la, limeundiwa timu na Serikali ambayo Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai (DCI), Robert Manumba na polisi wamo ndani yake. Alisema sasa suala hilo anamwachia Mungu na Serikali inayolichunguza, ambapo alikataa kuzungumzia zaidi kwa nini anahisi alilishwa sumu. “Hili mnalolihoji nitalizungumza kwenye timu hiyo itakayokuja kunihoji, nawashauri muwe na subira ikikamilisha uchunguzi wake, itasema na hata mimi nitasema.”

KATUNI YA LEO


HARUSI YA KIMILA YA JACKLINE MAFURU

JACKLINEY
KWA SHIDA NA RAHA
JACKLINEY NA MASHOSTI WAKE

kwa picha zaidi BOFYA http://www.tmark-turn.blogspot.co.uk/

Monday, March 19, 2012

RAIS JK AMWAPISHA MKUU MPYA WA JKT

Mkuu Mpya wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Samwel Ndomba akila kiapo mbele ya Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete ikulu jijini Dar es Salaam leo asubuhi.Meja Jenerali Ndomba anachukua nafasi ya Meja Jenerali Samwel Kitundu aliyestaafu hivi karibuni kwa mujibu wa sheria.

Sunday, March 18, 2012

MSANII LINAH KATIKA POZI NCHINI MAREKANIMSANII wa muziki wa kizazi bongo Linah, ambaye yuko Nchini Marekani kwa ajili ya matamasha yaliyo na lengo la kuutangaza muziki wa bongo fleva pamoja na tamaduni za watu wa Afrika akiwa katika Kodak za Nguvu hivi karibuni. Wadau kaeni mkao wa kula kwa show zake Nchini Marekani kwa kufuatilia blogu ya Vijimambo.


http://lukemusicfactory.blogspot.co.uk/ 

BIASHARA YA MITALIMBO BANDIA YA KIUME YASHAMILI BONGO

Florence Majani -Mwananchi. 
KATIKA kile kinachoonekana kuwa baadhi ya wanawake wamedhamiria kumaliza hisia zao za kimapenzi wao kwa wao, biashara ya uuzwaji viungo bandia vya siri vya kiume, imeshamiri jijini Dar es Salaam. Mwananchi Jumapili lilifika hadi katika duka maarufu la vipodozi wilayani Kinondoni na kubahatika kuzungumza na muuzaji aliyejitambulisha kwa jina moja la Kelvin ambaye alisema, viungo hivyo bandia vimekuwa vikigombewa kwa kasi pindi vinafikishwa dukani hapo. Kelvin alisema, inamuwia vigumu mmiliki wa duka hilo kuwatosheleza wateja wake wengi, wanaoweka oda ya bidhaa hiyo, kutokana na idadi yao kuongezeka. “Akileta viungo 50, havikai kwa zaidi ya siku tatu, akileta 70 au 90, havimalizi wiki,” alisema Kelvin. Hata hivyo, muuzaji huyo alidai kuwa, kwa sasa hakuna viungo hivyo kwa sababu mzigo bado haujaingia jambo ambalo limesababisha wateja wengi kuulizia kila siku. “Kama jana amekuja msanii maarufu wa kike wa nyimbo za taaribu, alikuwa anahitaji viungo, na mbunge mmoja wa kike naye aliviulizia majuzi, lakini ndo hivyo mzigo bado haujaingia,” alisema Kelvin. Bei ya viungo hivyo Akizungumzia gharama za viungo hivyo, muuzaji huyo alisema, bei inategemea umbile akimaanisha, urefu au upana wa kiungo chenyewe. “Kuna uume wenye inchi sita, nane hadi 12, pamoja na ukubwa wa kiuno cha mvaaji, kila moja kina bei yake, lakini kiwango cha kawaida ni kuanzia Sh45, 000 hadi Sh 80, 000,” alisema muuzaji huyo. Kelvin aliwataja wateja wakubwa kuwa ni wanawake maarufu, raia wa kigeni na wanawake waliozoea maisha ya starehe. Alisema: “Wanaokuja kununua hapa ni wale watu wa ‘viwanja,’ wengine wale walioshindikana kabisa tunawajua wanavuta bangi na unga, lakini pia wanawake wa kizungu nao huviulizia.” Aidha alisema, duka hilo haliuzi viungo vinavyotumia umeme,(vibrator) kwa sababu vinasemekana kuwa na madhara. Mwananchi Jumapili lilipotaka kujua ni mahali gani pengine viungo hivyo vitapatikana,jijini Dar es Salaam, kijana huyo alisema, anaweza kwenda kuvipata kwa mama mmoja mkazi wa Msasani ingawa bei itaongezeka. Kelvin aliyataja maeneo mengine ambapo viungo hivyo vinaweza kupatikana kuwa ni katika maduka makubwa ya vipodozi ya Kariakoo na Sinza. Ili kupata uhakika wa ni lini viungo hivyo vitawasili, muuzaji huyo alitoa namba ya mmiliki wa duka hilo ambaye baada ya kupigiwa , alidai yeye huwa hauzi, lakini humtafutia wateja mwanamke mmoja mwenye asili ya kiarabu, mkazi wa Upanga ambaye ndiye muuzaji mkongwe. “Havijawasili hapa nchini siku nyingi, lakini mimi huwa siuzi, namtafutia wateja mama mmoja hivi mwarabu wa Upanga, hata hivyo bado nina bidhaa nyingine kama unahitahi dawa za kuongeza matiti, kuwa mweupe,” alisema mmiliki wa duka hilo. Wanawake wanasemaje? Baadhi ya wanawake waliohojiwa kuhusu kuongezeka kwa manunuzi ya viungo hivyo, walidai kuwa, hali hiyo inasababishwa na kukata tamaa katika mahusiano. Pendo Mallya mkazi wa Tabata jijini, Dar es Salaam, alitaja usaliti wa kimapenzi kuwa ndiyo chachu ya wanawake kuchukua uamuzi wa kununua viungo bandia. “Tumechoka kutendwa (heartbroken) , wanaume hawaaminiki, kwa hiyo ili kuepusha kubadili wanaume kila siku, ni bora ujitimizie haja zako mwenyewe,” alisema Pendo. Aliongeza kuwa licha ya kuepuka kutendwa na wanaume, lakini matumizi ya viungo hivyo yanakutoa katika hatari ya maambukizi ya magonjwa ya zinaa ukiwemo Ukimwi. “Kitu kingine, ni kuwa unakitumia kila unapokuwa na haja, tofauti na mwanaume atakuambia sipo, nimesafiri leo nimechoka na sababu nyingi,” alisema. Lakini Edwin Mnzeru alikuwa tofauti na Pendo ambapo yeye aliona wanawake wanaotumia viungo hivyo, wanashabikia ujinga. “Hizi ni athari za utandawazi, tujaribu kuiga mazuri, tuyaache mabaya, siyo kila kitu lazima tufanye,” alisema Aliongeza kuwa, serikali inatakiwa idhibiti uingizwaji wa bidhaa zote zinazoonekana kuvunja maadili. Mtaalam wa Saikolojia Mtaalamu wa masuala ya Saikolojia kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Richard Msambaiga, aliitaja sababu kuu inayowasababisha wanawake kununua viungo hivyo kuwa ni usaliti katika mapenzi. “Mwanamke anapoona anasalitiwa kimapenzi, anaona njia bora ni kujimalizia haja zake mwenyewe, kisaikolojia, anahisi ametibu majeraha kwa kujimiliki,” alisema. Aliongeza kuwa, wapo wenye hisia kuwa, kufanya mapenzi mwanamke na mwanaume, ni mfumo dume, hivyo anapopata nyenzo kama hizo, hudhani kuwa ametatua matatizo ya mfumo dume. Alizungumzia suala la utandawazi na kusema, umeruhusu kila taka kuingia, hivyo watu wamepata uhuru wa kujichagulia kile wakitakacho kiwe kibaya au kizuri. Alisema, wanawake kutumia viungo bandia vya kiume kufanya tendo la ndoa, ni suala la kina lenye sababu chekwa za kisaikolojia, kikubwa kikiwa ni wanawake kukata tamaa katika mahusiano na utandawazi. Nchi za Magharibi Katika nchi za magharibi, uuzwaji wa viungo bandia, umekuwa jambo la kawaida ambapo yapo maduka na kampuni mahususi kwa ajili ya bidhaa hizo tu. Hivi karibuni, kampuni za Magharibi ziliibuka na kuanza kuajiri watu watakaoweza kujaribu nyeti hizo bandia kabla ya kuziuza. Mmoja wa watu walioajiriwa ni Nat Garvey ambaye hulipwa kiasi cha Sh milioni 50 kwa mwezi kwa ajili ya kujaribu uwezo na ubora wa nyeti hizo bandia za kiume. Anachokifanya ni kujaribu, kisha kuitaarifu kampuni husika kasoro au ubora uliopo katika bidhaa hiyo. Takwimu zinaonyesha kuwa, kiasi cha viungo bandia vya siri milioni nne huuzwa barani Ulaya kila mwaka na huenda idadi hiyo ikaongezeka hadi kufikia milioni 400 katika siku za usoni. Hivi karibuni kumekuwapo taarifa za ongezeko la wanawake nchini, kufanya mapenzi wenyewe kwa wenyewe wakidaiwa kutumia nyeti badi za kiume.

AUNT EZEKIEL AANGUKA NA KUZIMIA !!!


NYOTA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ (pichani) amepatwa na maswahibu makubwa baada ya kukumbwa na ugonjwa wa ajabu uliomfanya kuanguka na kupoteza fahamu huku akitokwa na mapovu mdomoni. Tukio hilo limetokea usiku wa Jumatano mjini Morogoro ambako Aunt na mastaa wengine walikuwa wakirekodi filamu. Mmoja wa watu waliokuwepo katika tukio hilo, aliyejitambulisha kwa jina moja la Vivian ameliambia amesema kwamba, walipokuwa katika harakati za kurekodi, walimsikia Aunt akitoa sauti kubwa kisha akaanguka, mapovu yakamtoka mdomoni na baadaye akapoteza fahamu. Vivian aliendelea kusema kuwa, baada ya kutokea kwa hali hiyo, wasanii wote walipigwa na bumbuwazi, wakasimamisha shughuli zilizokuwa zikiendelea na kumsaidia mwenzao kumpeleka hospitali ya Mkoa wa Morogoro. “ Tulichanganyikiwa, hakuna mtu ambaye anaweza kukuambia kitu kilichotokea kwa ufasaha na hatujui Aunt amekumbwa na nini, ilikuwa ni kitendo cha ghafla sana,” alisema Vivian kwa majonzi. Kwa mujibu shuhuda huyo, Aunt alipata matibabu katika hospitali hiyo ya mkoa kwa kuchomwa sindano mbili na kutundikiwa dripu tatu ambazo zilimfanya aweze kuzinduka na kuongea. “Kwa kweli tulichanganyikiwa maana alikuwa hafumbui macho, anaongea kwa tabu, alikuwa akiuma meno huku povu likimtoka mdomoni lakini baada ya kupata huduma hiyo alitulia na akafumbua macho,” alisema. Usiku wa siku hiyo, Aunt alitolewa hospitali na utaratibu wa kumrudisha Dar ulikuwa ukiandaliwa. Auntalipigiwa simu na Risasi lakini ilipokelewa na Vivian ambaye alimpatia msanii huyo aliyekuwa akiongea kwa tabu. “Ni kweli naumwa, ila ningeomba nipumzike nitaongea muda mwingine,” alisema Aunt


 CHANZO: RISASI

Thursday, March 15, 2012

NICKY MINAJ ............

............. flaunted her ASSets in Hawaii yesterday as she filmed her new "Starships" video.

Wednesday, March 14, 2012

MAMBO YA MDUARA NDANI YA DAR LIVE

Mzee wa Vifuu Tundu "AT" akiwajibika na mwanadada SHILOLE
HAPO CHACHA!!!
OFFSIDE TRICK na Nyama ya Bata

SOLOMON MKUBWA KUTUMBUIZA TAMASHA LA PASAKA

Na Mwandishi Wetu

MWIMBAJI nguli kutoka Kenya, Solomon Mukubwa, anatarajia kutumbuiza katika tamasha la muziki wa Injili la Pasaka litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka Aprili 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha hilo, Alex Msama ambaye ni Mkurugenzi wa Msama Promotions, alisema Dar es Salaam jana kuwa Mukubwa ameahidi kufanya mambo makubwa. Msama alisema mwimbaji huyo wa nyimbo za kumsifu Mungu mwenye ulemavu wa mkono mmoja, hivi sasa anatamba na albamu yake mpya ya Usikate Tamaa, ambayo anaamini itamng'arisha katika tamasha hilo. Msama alizitaja nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ya Usikate Tamaa kuwa ni Usikate Tamaa, Mungu Wangu Nitetee, Niko na Yesu, Mke Si Nguo, Moyo Tukuza Bwana, Chunga Ahadi Yako na Yesu Jina Zuri. Mukubwa kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), anayeishi Kenya, amewahi kutoa albamu mbili ambazo ni Sijaona Rafiki na Mungu Mwenye Nguvu. Sijaona Rafiki Kama Yesu ambayo ni albamu yake ya kwanza ina nyimbo za Uwe Nami Bwana, Sijaona Rafiki Kama Yesu, Nitayainua Macho, Matendo ya Mungu, Bwana Wastahili na Yesu Kimbilio. Albamu yake ya pili ya Mungu Mwenye Nguvu ina nyimbo za Mungu Mwenye Nguvu, Mkono wa Bwana, Mfalme wa Amani, Siku Moja, Tabia Ina Dawa na Roho Yangu Ikuimbie. Mbali na Mukubwa, wengine waliothibitisha kushiriki tamasha hilo litakalofanyika Sikukuu ya Pasaka ni Rose Muhando, Anastazia Mukabwa, Upendo Nkone, Upendo Kilahiro, Christina Shusho, Atosha Kissava, Mwinjilisti Faraja Ntaboba kutoka DRC na kundi la Glorious Celebration. Pia kwaya mahiri ya Kinondoni Revival inayotamba na albamu yao mpya ya Mtu wa Nne, inatarajia kutumbuiza katika tamasha la Pasaka. Nyimbo zilizomo kwenye albamu hiyo ni Mtu wa Nne, Imekwisha, Chukua Hatua, Mtafuteni Bwana, New Season, Hakikisha, Ninakushukuru na Dini Iliyo Safi. Pia kwaya hiyo ya Kinondoni Revival imewahi kutamba na albamu yao ya Kilio cha Mcha Mungu yenye nyimbo nane za Kilio cha Mcha Mungu, Kwanini Unataka Kujiua, Ayubu II, Vumilia Kidogo, Nafsi Yangu, Natamani Kwenda Mbinguni, Ndugu Yetu Twakutafuta na Twalilia Tanzania ambazo pia wameahidi wataziimba. Msama alisema baada ya waimbaji hao kutikisa Uwanja wa Taifa, mashambulizi mengine yatahamia kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Aprili 9 mwaka huu. Tamasha la mwaka huu malengo yake makubwa ni kuchangisha fedha kwa ajili ya kuwasomesha watoto yatima na kuwasaidia mitaji wanawake wajane. Kiingilio katika tamasha hilo kimetengwa katika kategoria tatu na kitakuwa sh. 2,000 kwa watoto, sh. 5,000 kwa viti vya kawaida na viti maalumu sh. 10,000. Tamasha la Pasaka la mwaka huu pia litashirikisha waimbaji wa nyimbo za Injili kutoka nchi za Uganda, Rwanda, Afrika Kusini na Zambia. Pia kutakuwa na kwaya na vikundi vya burudani.

Tuesday, March 13, 2012

QATAR AIR KUANZA KUTUA KIA

NDEGE za Shirika la Qatar zinatarajiwa kuanza safari kati ya Doha na Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) kuanzia Julai mwaka huu. Mkurugenzi Mtendaji wa shirika hilo, Akbar Al Baker alitoa taarifa hiyo wakati wa maonesho makubwa ya wakala wa usafirishaji wa anga na utalii maarufu kama ITB Berlin, yaliofanyika mwishoni wa wiki iliyopita Jijini Berlin, Ujerumani. Alisema, shirika hilo itatoa huduma za anga uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro ikitumia ndege aina ya Airbus A320 kupitia jiji la Nairobi. Mkurugenzi Mtendaji wa KIA, Marco van de Kreeke alisema kuanzisha kwa safari hiyo kutafungua milango kwa wawekezaji kutoka Mashariki ya Kati, India, China na nchi nyinginezo za Asia. Alisema, wanatarajia huduma mpya za kila siku kupitia Doha zitasaidia kukua na kurahisisha uwanja wa ndege wa Kilimanjaro kuchangia uchumi wa taifa na kutangaza vivutio vilivyopo Kaskazini. Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania, Dk Aloyce Nzuki akitoa maelezo juu ya umuhimu wa safari hiyo katika maendeleo ya sekta ya utalii nchini, alisema mkoa wa Kilimanjaro na mikoa ya jirani ikiwemo Tanga, Arusha na Manyara itafaidika kupitia vivutio vya kitalii na baadaye kuchangia kukuza sekta ya utalii nchini. Taarifa ya ujio wa ndege za shirika la Qatar imekuja baada kutangazwa kwa ukarabati wa uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro utakaogharimu dola za kimarekani milioni 35 . Mradi huo ulioanza tangu Januari mwaka jana utajumuisha marekebisho ya njia za ndege mpya ili kuuongezea uwezo uwanja na upanuzi wa majengo yanaozunguka uwanja . Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mpaka sasa unatoa huduma kwa abiria 650,000 kwa mwaka. Idadi ya wasafiri kutoka nje imekuwa ikiongezeka kwa asilimia 15 kila mwaka kutoka 2003. Shirika la Ndege la Qatar linafanya safari mbalimbali duniani kutumia ndege za kisasa 105 na kuunganisha vituo 112 vya kibiashara na mapunziko barani Ulaya, Mashariki ya Kati, Afrika, Asia, Pasifiki, Amerika ya Kaskazini na ya Kusini.