.

.

.

.

Thursday, February 28, 2013

NEW HOUSE FOR SALE IN TABATA



Beautiful newly built house for sale in Tabata, Dar es Salaam.
Master bedroom/bathroom, 3 other bedrooms, kitchen, dining, living,
separate shower/toilet, water well and more
.



Bathrooms :     2
Bedrooms :     4
Location:     Tabata, Dar es Salaam   
Asking Price:     USD 300,000
Or for rent:       USD 1,000


contact:
+255717415868

RAIS KAGAME ATEUA MTANZANIA KUWA WAZIRI



 Rais wa Rwanda Paul Kagame
Waziri wa Miundombinu Rwanda Profesa Silas Rwakabamba
--
RAIS Paul Kagame wa Rwanda amemteua Mtanzania, Profesa Silas Rwakabamba kuwa Waziri wa Miundombinu wa nchi hiyo katika mabadiliko ya Baraza la Mawaziri yaliyofanyika Jumatatu iliyopita.

Kabla ya uteuzi huo, Profesa Rwakabamba alikuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Rwanda. Ni mmoja wa mawaziri wanaoingiza sura mpya katika Baraza la Rais Kagame ambalo amelifanyia mabadiliko kwa kuunda wizara nyingine mpya.

Sura nyingine mpya katika Baraza hilo ambalo liliapishwa juzi Ikulu ya Rwanda ni pamoja na Seraphine Mukantabana (Wakimbizi na Menejimenti ya Maafa) na Oda Gasinzigwa (Ofisi ya Waziri Mkuu- Familia na Jinsia).

Akizungumza kwa simu na mwandishi wetu jana, mdogo wa Profesa Rwakabamba, Timothy Rwamushaija anayeishi Dar es Salaam, alisema ndugu yake alizaliwa katika Kijiji cha Bushagara, Wilaya ya Muleba mkoani Kagera.

Alisema Profesa Rwakabamba alikuwa Mtanzania aliyeamua kuchukua uraia wa Rwanda na wote baba yao ni Mzee Titus Rwamushaija... “Huyu ni kaka yangu wa tumbo moja na kwa kweli tumefurahi sana kwa mafanikio yake sisi kama wanafamilia.

JENGO LA ATC KUPIGWA MNADA ???


MWANASHERIA Mkuu wa Serikali (AG), amelazimika kuingilia  kati sakata la jengo la Makao Makuu ya Shirika  la Ndege Tanzania (ATCL), kutaka kupigwa mnada kwa amri ya mahakama kutokana na maombi yaliyowasilishwa mahakamani na Kampuni ya Leisure Tours and Holdays Limited.
Kampuni hiyo imeomba mahakama hiyo iamuru jengo hilo liliko Mtaa wa Ohio, Dar es Salam lipigwe mnada ili kufidia deni lake inalodai ATCL, dola 716,259.25 za Marekani (zaidi ya Sh1 bilioni), kwa kulikodishia magari mwaka 2008.
Kutokana na ATCL kushindwa kulipa deni hilo kama walivyokubaliana nje ya mahakama, kampuni hiyo iliwasilisha maombi  Mahakama Kuu Kitengo cha Biashara na  mahakama iliamuru kampuni hiyo ifanye uthamini wa jengo hilo na kuwasilisha taarifa hiyo.
Mahakama hiyo ilitarajiwa kutoa amri ya kama jengo hilo lipigwe mnada jana, lakini AG aliwasilisha maombi akitaka naye ajumuishwe kwenye kesi hiyo.
Kwa mujibu wa maombi hayo,  AG anadai kuwa ameamua kuingilia kati sakata hilo ili kulinda maslahi ya Serikali, kwa kuwa jengo hilo ni mali yake.
Kutokana na maombi hayo ya AG, mahakama hiyo ililazimika kuahirisha kutoa amri yake,  badala yake ilipanga kusikiliza maombi ya AG Machi Mosi.

Wednesday, February 20, 2013

ALI KIBA NA OMMY DIMPOZ KUKAMUA LONDON JUMAMOSI HII


JUSTUS ESIRI DIES


Nollywood movie industry has been hit with another sudden death and it's veteran actor Justus Esiri. He passed way on Monday night after a short-time battle with an undisclosed ailment in his hometown. Few months ago, Nigerian singer and Mavin record member, Dr Sid introduced Justus Esiri as his father. Dr Sid real name is Onoriode Esiri, he is the youngest child of the deceased. As at the time of this report, no detail has been released regarding Justus Esiri's death but it is a shock to everybody as the family only released this few hours ago. A source said the now late Justus Esiri has been secretly battling an age related illness for a while but his family chose to make it a secret until his sudden demise Monday night at the age of 71. Last year over four top Nollywood stars including Pete Eneh and Enebeli Elebuwa died. Pete Eneh died of untreated leg infection on November 15, 2012 at a private hospital in Enugu while Enebeli Elebuwa died of stroke on the 4th of December 2012 at a private hospital in New Delhi, India. Just this last week two Nollywood actors died tragically. A source who claimed the angel of death has visited Nollywood might be proven true with the sudden demise of top Nigerian movie stars one after the other within the past 12 months. Before his death, Justus Esiri was a member of the Order of Niger (MON). He came into limelight in the early 80's through the popular Village Headmaster TV series. He has also featured in many interesting Nollywood movies. The late Justus Esiri was born in November 1942 in Oria, Abraka, Delta State. His studied at Catholic Secondary school in Warri in year 1948 before proceeding to Maximillan University in Munich, German in 1964. He also attended Prof. Weners Institute of Engineering, West Berlin, 1967 and the Ahrens School of Performing Arts in 1968. Justus Esiri, detoured into motion picture production in 1968 as a staff of the Schiller Theater, Berlin, Germany, where he stayed till 1976. During the 1977 FESTAC held in Lagos, he choreographed the Modern Dress exhibition. He was Production Manager for Dinner With The Devil. He worked as News translator and Newscaster with the Voice of Nigeria (German Service).

ASKOFU SHAO ALIA NA SELIKALI


ASKOFU wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Zanzibar, Augustino Shao na ndugu wa marehemu wa Padri Evarist Mushi wameitupia lawama Serikali kwa kuzembea kuwalinda viongozi wa dini hiyo waishio Zanzibar licha ya kupewa taarifa za viashiria vya hatari mara kwa mara.
Askofu Shao alisema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar na ndugu wawili wa Padri Mushi walieleza hayo huko Moshi.

Hata hivyo, Mkurugenzi wa Mawasiliano Ikulu, Salva Rweyemamu alisema jana kwamba hawajapata malamamiko yaliyoelezwa na Askofu Shayo na kwamba kama Rais Jakaya Kikwete angeyapata asingeacha kuyashughulikia.

Kamishna wa Polisi Zanzibar, Mussa Ali Mussa naye alikanusha madai hayo akisema:
“... Hapa tulipo tuna kesi nyingi na kuna watu wanahojiwa. Sisi hatufanyi kazi kwa shinikizo la mtu, kama ni hivyo vipeperushi hata sisi tunavipata siyo wao tu. Sasa tutawakamataje wakati watu wenyewe hatuwajui?”

Hata hivyo, Askofu Shao alisema hawaridhishwi na utendaji kazi wa Polisi na kudai kwamba Wakristo wa madhehebu yote wanalengwa na mashambulio yanayofanywa na watu aliosema kuwa wanapata msaada kutoka nje.

“Niseme wazi tu, haturidhishwi na utendaji wa Serikali katika kutulinda. Tumemwandikia barua Rais wa Zanzibar Dk Ali Mohamed Shein na Rais Jakaya Kikwete tukiwaeleza vitisho tunavyopewa, lakini hatuoni hatua zikichukuliwa,” alisema Askofu Shao na kuongeza:

“Walipomshambulia Padri Ambrose Mkenda watu hao walileta ujumbe kwamba, tumeshawaweza Padri Ambrose na Sheikh Fadhil Soraga na bado tutaendelea. Vijana wetu wa kazi wameshamaliza mafunzo Somalia,” alinukuu moja ya kipeperushi huku akisema kuwa tatizo la Serikali ni kutokuwajibika.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Mohamed Aboud Mohamed alikiri kupokea taarifa hizo za vitisho na kusema Serikali ina vyombo na taratibu zake katika kufanya kazi... “Sasa unataka Rais akamate wahalifu? Nadhani mtu sahihi wa kuzungumzia mambo haya atakuwa Kamishna wa Polisi. Ni kweli taarifa zimeletwa lakini nasi tulizipeleka kwenye vyombo vinavyohusika navyo ni Polisi.”

Askofu Shayo aliisifu Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akisema imejizatiti... “Bara wana nguvu, mtu akifanya kosa leo anakamatwa, lakini Zanzibar wanafanya kazi kwa kujuana.”

Askofu huyo alipinga kauli ya Serikali kuwa itahusisha taasisi za kimataifa kuwasaka wahusika wa mauaji akisema Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) likishirikiana na wananchi wanaweza kupata suluhu.

“Jeshi halijashindwa kumaliza uhalifu huu. Ukileta askari wa Shirika la Upelelezi la Marekani (FBI) watashindwa tu kwani hata Kiingereza hakitaeleweka. Bado watahitaji kupata msaada wa wananchi. Serikali inawajua wanaohusika, wanajua wanakokaa, tatizo ni uwajibikaji,” alisema Askofu Shao.

Hata hivyo, alisema kuwa hana ugomvi na Waislamu, bali anatofautiana na watu wote, wakiwamo Wakristo wanaotumia mgongo wa dini kufanya vurugu za kidini.
Askofu wa Mkuu wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycap Kadinali Pengo alisema kuwa mauaji ya Padri Mushi yangeweza kuzuiliwa kama viongozi wa nchi wangesoma alama za nyakati.

Akizungumza na Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) jana Kadinali Pengo alisema ni muhimu viongozi wa nchi kuchukua hatua na kuzuia yanayotokea na kuhusisha dini fulani.

Akimzungumzia marehemu Padri Mushi, Askofu Shao alisema: “Alikuja hapa Zanzibar tangu alipokuwa na miaka 18 akiwa anasoma elimu ya sekondari.

Mazishi yake

Askofu Shao alisema kuwa Ibada ya Mazishi ya Padri Mushi itafanyika Jumatano katika Parokia ya St. Joseph, Minara Miwili, Zanzibar na mwili wake utazikwa eneo la Kitope wanakozikwa viongozi wa kanisa.

Monday, February 18, 2013

MAONYESHO YA MAVAZI LONDON


Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe akiwa na mwanamuziki Freddy Macha aliyetumbuiza shughuli hii na gitaa lake.
- -
 Maonyesho maarufu ya mavazi  –London Fashion Week-  yaliyoanza rasmi Ijumaa iliyopita mjini London yameiweka ramani ya  Tanzania duniani. 
Shughuli hii muhimu kiuchumi na kisanaa inayoendelea  juma zima  na kuhusisha vituo vya kitamaduni na balozi 27  ina lengo la kutangaza vipaji vya wabunifu mavazi toka  nchi zisizojulikana  uwanja huu mahiri wa kimataifa unaosifika takriban miaka 30 sasa.
 “London Fashion Week”  ni moja ya maonyesho manne ulimwenguni yaliyoasisiwa rasmi kutukuza  ubunifu, ufundi na biashara  mwaka 1984.  Huendeshwa sambamba miji  ya New York, Milan na Paris kila mwezi Februari na Septemba.
Watanzania tulioingia  kwa dhamira ya “Swahili Flavour” (Ladha ya Kiswahili) tumefadhiliwa na  Ubalozi wa Tanzania London ukishirikiana na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Watayarishaji wa shughuli hii ni shirika la kitamaduni na elimu Uingereza- British Council lenye mahusiano ya kirafiki na nchi 100 duniani. “Maonyesho ya mavazi London ni fani ya hali ya juu na kibiashara ambapo waume kwa wanawake huwa pamoja wakibadilishana mapambo na visaidizi vyake,” anasema Julian Roberts, mbunifu mavazi wa British Council. 
Akiongea rasmi kwenye ufunguzi wa Ijumaa uliokuwa na vinywaji baridi na muziki wa Kiswahili, mke wa Balozi  Uingereza, Mama Joyce Kallaghe aliwasifu wabunifu mavazi wetu na kuwakabirisha wageni mbalimbali  waliohudhuria “kuzitembelea mbuga nzuri za Kitanzania kama watafurahishwa na mavazi na ladha yetu ya Kiswahili.”
 Wabunifu na washoni hao watatu ni Christine Mhando (  “Chichia London”),  Anna Lukindo ( “Anna Luks”) na Jacquleine Kibacha (“Heart 365”). Kibacha ambaye pia ni mtunzi wa mashairi huchanganya desturi za kijadi na kisasa kwa shanga shanga, manyoya ya ndege na mapambo yaliyotokana na sanaa za Wamasai. Miezi mitatu iliyopita kazi zake Kibacha zilipata tuzo maarufu la “Fashions Finest 2012.”
Akifafanua fani yake, Christine “Chichia” Mhando aliyehitimu chuo cha Usanii cha Kent mwaka 2002 alisema yeye huhamasisha vazi la Kanga, misemo na maneno ya Kiswahili mathalan “Tongoza”, “Ala Kumbe!” na “Zungumza” kama wajihi wa kazi hiyo.  Anna Luks aliyefuzu shahada ya mwanzo (BA) chuo cha Middlesex, alieleza azma  yake ni kumwonyesha mwanamke wa Kitanzania alivyo kupitia  mitindo kama “dunia pana” , “kaba roho” na “baibui.” Anna Luks huchanganya ushonaji wa mikono, kamba kamba na mavazi ya kisasa.  
 Naibu Balozi, Mheshimiwa Chabaka Kilumanga alisema maonyesho haya ya kimataifa yatakua nafasi kubwa kwa Tanzania kujitangaza kibiashara na ni sehemu mahsusi ya fahari ya utamaduni wetu. 
Wahusika wengine waliochangia  mafanikio ya shughuli  ni Mratibu Ubalozini, Bi Rose Kiondo; Afisa mwangalizi wa onyesho hilo, Samson Soboye na  Meneja  wa dhana  ya Swahili Flavour,  Mike Puplampu.
Habari zilizopatikana jana zilisema kwamba wabunifu mavazi wa Kitanzania wametajwa ndani ya kundi la washindi kumi bora. Ushindi huo unathibitisha dhahiri uwezo wa sanaa na ubunifu wetu ndani ya hulka ya mavazi ya kimataifa.
 Toka kulia, Mama Balozi- Joyce Kallaghe,  Anna Lukindo,  Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe,  Christine Mhando,  Naibu Balozi Chabaka Kilumanga na mkewe Irene. Picha na Urban Pulse


 Anna Luks, Mama Mhando na Chichia
 Mshoni Christine Mhando (Chichia London) akiongea na baadhi ya wageni
Moja ya vazi la kanga lililobuniwa na Chichia. Picha ya Urban Pulse
 Jacquiline Kibacha anayetumia jina la Heart 365. Picha na F. Macha
 Jacquiline Kibacha akipokea tuzo ya mapambo iitwayo “Fashions Finest 2012” mjini London mwezi Novemba mwaka jana
Moja ya ubunifu wa Jacquiline Kibacha uliohamasishwa na jadi ya Wamasai. 
Moja ya Ubunifu wa Anna Luks. Picha na Urban Pulse

Sunday, February 17, 2013

SPORAH SHOW NA KAMPENI YA FISTULA

MPITA NJIA

PADRI WA KANISA KATOLIKI AUWAWA ZANZIBAR


TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE TOKA VISIWANI ZANZIBAR,INATUHABARISHA KUWA PADRI EVERIST MUSHI (PICHANI) WA KANISA KATOLIKI HUKO ZANZIBAR,AMEPIGWA RISASI YA KICHWA NA WATU WASIOJULIKANA NA KUFARIKI PAPO HAPO ASUBUHI HII WAKATI AKIELEKEA KWENYE IBADA KATIKA KANISA LA MTONI,ZANZIBAR.

SABABU ZA KUPIGWA RISASI KWA PADRI HUYO BADO HAZIJAFAHAMIKA MPAKA SASA. 

MASHUHUDA WA TUKIO HILO WANASEMA KUWA WATU HAO WALIOFANYA TUKIO HILO WALIKUWA NI WAWILI NA WALIKUWA WAMEPAKIZANA KWENYE PIKIPIKI AINA YA VESPA WAKATI PADRI HUYO ALIKUWA KWENYE GARI LAKE AMBALO BAADA YA KUTOKEA KWA TUKIO HILO NALO LILIACHA NJIA NA KWENDA KUGONGA NYUMBA MOJA ILIYOKUWA JIRANI 



KWA HISANI YA MICHUZI BLOG





Raisi Kikwete Atoa Tamko

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Evarist Mushi wa Parokia ya Minara Miwili ya Kanisa Katoliki mjini Zanzibar, mauaji yaliyotokea Zanzibar.
Rais Kikwete anawapa pole nyingi na rambirambi za dhati ya moyo wangu Baba Askofu Augustino Shayo wa Jimbo Katoliki, Zanzibar, maaskofu wote nchini na waumini wote wa Parokia ya Minara Miwili kwa msiba huo mkubwa uliowakuta.
Rais kikwete amemwambia Baba Askofu Shayo. ”Napenda kuwahakikishia kuwa tupo pamoja katika kuomboleza kifo cha Mpendwa Marehemu Padri Evarist Mushin a kuwa msiba huu ni wa kwetu sote.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Nimeligiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”
“Aidha, nimewaagiza Jeshi la Polisi washirikiane na vyombo vingine vya Usalama nchini na mashirika ya upepelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji haya.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Nataka ukweli wake ujulikane ili kama kuna jambo lolote zaidi liweze kushughulikiwa na kukata mzizi wa fitina.”
Vile vile, Rais Kikwete amewataka waumini wa Kanisa katoliki na wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali inashughulikia suala hili na kuwa hakuna mtu wala watu ama kikundi cha watu kitachoruhusiwa kuvuruga amani ya nchi yetu.




































Friday, February 15, 2013

KALUNDE BAND YASHEREKEKEA MIAKA 7 SIKU YA WAPENDANAO


 Rais wa Kalunde Band, Deo Mwanambilimbi akikata keki kwa pamoja na Meneja wa benki hiyo, Deborah Nyangi ambaye pia ni Muasisi wa Band hiyo.
Deborah Nyangi akiandaa keki  kwa ajili ya kuwalisha baadhi ya wadau. Kushoto ni Rais wa Band hiyo, Deo Mwanambilimbi na Mwapani Yahya
Meneja wa Kalunde Band, Deborah Nyangi akiandaa akimlisha kipande cha keki, Rais wa Band hiyo, Deo Mwanambilimbi wakati wa sherehe za kutimiza miaka saba tangu kuzaliwa kwa band hiyo.
Deo kama anasema; Tumetimiza miaka saba na tunasonga mbele.
Rais wa Kalunde Bande, Deo Mwanambilimbi akimlisha keki, Meneja wa band hiyo, Deborah Nyangi wakati wa sherehe ya kutimiza miaka saba tangu kuanzishwa kwa bendi hiyo.
Kiongozi wa Wanamuziki, Bob Rudala akilishwa keki.
Wanamuziki wa Kalunde Band wakiwajibika jukwaani wakati wa Valentine Day.
Othman Amri King Majuto - Bass Guitar na Rajab Nyunyusa - Tumba
 Meneja wa Band, Deborah Nyangi.
Frola Bambucha
 Queen Vero (kushoto) na Flora Bambucha wakicheza sambamba na Kalunde Band wakati wa sikukuu ya valentine iliyokwenda sambamba na band hiyo kutimiza miaka saba.
Siku ya Valentine ni muhimu kwa Kalunde kwani ndiyo siku ambayo band hii  ilianzishwa. Band ilianzishwa tarehe 14.02.2006. Hapa rais wa Band hiyo, deo Mwanambilimbi akiweajibika jukwaa leo katika kiota cha maraha cha Trinity Oysterbay.




HAPPY BIRTHDAY

 ya kutimiza miaka saba ya Kalunde Band ilikwenda sambamba na sherehe za siku ya wapendanao ambapo mashabiki wake walipata barudani ya kukata na mundu katika kiota cha maraha cha wapendanao cha Trinity maeneo ya  Oysterbay jijini Dar es salaam karibu na Ubalozi wa Uganda.
 



Kundi zima la bendi hiyo kama ifuatavyo.

Deo Mwanambilimbi - Rais wa Band - Muasisi wa Band
Debora Nyangi - Meneja - Muasisi
Bob Rudala - Kiongozi wa wanamuziki
Bony Kaprobo - Solo Guitar - Band Stage Leader
Shehe Mwakichui - Keyboard Player / Mwimbaji - Muasisi wa band
Edson Allen (Eddy) - Solo Guitar
Othman Amri Majuto - Bass Guitar
Rajab Nyunyusa - Tumba
Alfa - Drummer
Mackie Fanta - Mwimbaji
Devotha, Mwapwani Yahya, Shila, Amina, wote hawa ni waimbaji