.

.

.

.

Friday, December 26, 2008

ALIBADILI KUSOMWA KATIKA KABURI LA AMINA CHIFUPA


Mtoa habari hizi ni BaBa wa Amina, Hamis Chifupa ambaye amesema kuwa dua hiyo itasomwa kwenye kaburi la marehemu huyo, lililopo kwenye Kijiji cha Lupembe, Njombe, Iringa.Mzee Chifupa alisema kuwa pamoja na dua hiyo kuwalenga wabaya wa Amina, pia kisomo hicho kitakuwa na dhumuni lingine ambalo ni kumrehemu Amina ili Mungu amsamehe makosa yake aliyoyafanya akiwa duniani.Aidha, mzee huyo aliweka wazi kwamba shabaha nyingine ya kumsomea dua hiyo mwanaye ni kumuenzi kwa tabia yake ya kupenda kuwa karibu na Mungu kwa kusali na kuomba dua enzi za uhai wake.“Hivi sasa nipo njiani naelekea kijijini kwa ajili ya dua hiyo, kama kuna mambo ya ziada basi nitakuja kueleza baada ya kurudi,” alisema Mzee Chifupa na kuongeza:“Hii ni dua kubwa, ni dua ya mwaka ya kumuombea marehemu Amina. Tutakuwa na wataalamu wetu wa dua pamoja na ndugu wengine, yote kwa yote ni kumkumbuka mtoto wetu tuliyempenda.”Katika hatua nyingine, Mzee Chifupa alisema kuwa bado dhamira yake ya kuwataja vigogo waliokuwa ‘wanamkorogea sumu’ mwanaye ipo pale pale, ingawa alisita kidogo kutokana na sababu ambazo hakutaka kuziweka wazi.Alilisema hilo, baada ya kupigwa swali na mwandishi wetu kwamba kuna madai kuwa alishindwa kuwataja vigogo hao licha ya kutangaza kufanya hivyo kutokana na kupewa kitu kidogo ili afumbe mdomo.“Nini! Siwezi kuhongwa, kifo cha mtoto wangu kiliniuma sana. Ngoja nikitoka kijijini, nitakuja kueleza hili jambo kwa kirefu,” alisema Mzee Chifupa.Gazeti hili, liliwahi kumkariri Mzee Chifupa akisema kuwa atataja majina ya vigogo wote waliokuwa na ‘bifu’ na marehemu Amina.Amina alifariki dunia Juni 26, 2007 baada ya kusumbuliwa kwa muda na ugonjwa shinikizo la chini la damu na sukari kabla ya kuzikwa siku mbili zilizofuata.


SOURCE: Gazeti la Ijumaa

No comments:

Post a Comment