.

.

.

.

.

.

Sunday, February 07, 2016

NYUMBA ALIOSHI RAIS MSTAAFU JK MIAKA YA SABINI MJINI SINGIDA

 Mwenyekiti wa CCM, Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipiga picha na mke wake Mama Salma Kikwete, majuzi, mbele ya nyumba ambayo Aliishi  mjini Singida mwaka 1975, wakati huo akiwa katibu Msaidizi wa  TANU  wilaya ya Singida mjini Hivi majuzi.

Tuesday, February 02, 2016

MH. WAZIRI MKUU MJINI MOSHI Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipokea picha aliyopewa na Askofu Mkuu Mpya wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli,Askofu Frederck Shoo katika ibada ya kumuingiza kazini askofu huyo ilyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
 Baadhi ya waalikwa walioshiriki katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheli Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016. 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizunguza katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo iliyofanyika kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
 Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akisalimiana na Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa katika ibada ya kumuingiza kazini Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania, Askofu Frederick Shoo kwenye kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Askofu Mkuu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Askofu Frederick Shoo (kulia) na Askofu Mkuu wa KKKT Mstaafu Alex Malasusa baada ya ibada ya kumuingiza kazini Askofu Shoo iliyofanyika kwenye Kanisa Kuu la KKKT mjini Moshi Januari 31, 2016.

(PICHA NA OFISI YA WAZIRI MKUU)

Tuesday, January 26, 2016

WANAOPENDA RUSHWA WAWEKWA KIKAANGONI


 Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola akizungumza na wanahabari.
 Kaimu Mkurugenzi Mkuuwa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru), Kamishna Valentino Mlowola (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini jijini Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu mikakati mbalimbali ya taasisi hiyo ya kupambana na rushwa nchini hasa kwa watendaji wa Umma na kesi zinazochunguzwa ili watuhumiwa wafikishwe mahakama wakati wowote baada ya kukamilika kwa uchunguzi wake.
 Wanahabari wakichukua taarifa hiyo. Kulia ni John David wa Gazeti la Majira.
 Mwendeshaji wa Mtandao wa Fullshangwe, John Bukuku (kulia), akiuliza swali katika mkutano huo.
Baadhi ya wakurugenzi wa Taasisi hiyo wakiwa katika mkutano huo.


Na Dotto Mwaibale

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa Nchini (Takukuru), imetoa onyo kwa taasisi nyeti nne hapa nchini ikiwemo wanaohusika na matumizi ya fedha za Umma kufuata sheria, taratibu na kanuni.

Pia,Takukuru inashughulikia kukamilisha kesi kubwa 36, zinazowahusu watumishi wenye ushawishi na hadhi kubwa hapa nchini ambapo kati ya hizo zipo zilizokamilika na kupelekwa kwa Mkurugenzi wa Mashtaka.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo , Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi hiyo, Valentino Mlowola alisema kumekuwepo na malalamiko mengi kwa wananchi kuwajulisha matendo ya rushwa na ufisadi yanayoendelea hapa nchini.

Alisema kutokana na hali ya wananchi kuona nia ya serikali ya awamu ya tano katika kushughulikia matatizo ya rushwa na ufisadi hapa nchini ametoa onyo kwa maofisa wa umma wanaofanya rushwa na ufisadi kuwa sehemu yao ya kazi na miradi ya kuwaingizia kipato.

"Natoa onyo kwa maofisa wa umma ambao wamefanya rushwa na ufisadi kuwa ni sehemu ya kazi zao na miradi ya kuwaingizia kipato, wajitafakari kabla hawajaamua kujihusisha na vitendo vya rushwa,"alisema.

Alisema  hawatasita kuchukua hatua kali za kisheria kwa watumishi watakaojiingiza katika kulihujumu taifa na wananchi kwani wananchi wanakiu ya kupata maendeleo na maisha bora na kuwataka watambue wananchi wa jana si wa leo kwani wamedhamiria kuunga mkono juhudi za serikali yao.

Mlowola alitoa ovyo kwa maofisa maduhuli na watekelezaji wa jukumu la kukusanya kodi za wananchi kwa kutomuonea mtu haya kwa atakayejihusisha na ubadirifu wa fedha na mali ya umma.

"Wakusanye kodi halali ya serikali kwa kufuata sheria, taratibu na Kanuni zinazowaongoza kukusanya kodi, tutachukua hatua stahiki pale kutakapokuwa na ukiukwaji wa sheria, taratibu na kanuni zilizopo,"alisema.

Pia, Mlowola alitoa onyo kwa watakaohusika kwenye matumizi ya fedha za umma kwamba wafuate sheria, taratibu na kanuni  zinazowaongoza kwani taasisi hiyo haitawavumilia watakaokiuka fedha za serikali isiyo halali.

Mbali na hilo, pia Kaimu huo alitoa onyo kwa watumishi wa umma wenye jukumu la kuhudumia mahitaji ya umma kwa kutojihusisha na rushwa kwa kutekeleza majukumu yao katika muda uliotakiwa, weledi na uaminifu.

Alisema taasisi hiyo haipo kwa lengo la maslahi ya watu wabadhilifu wa mali ya umma kwani uchunguzi wa kesi ya kuisababishia hasara serikali shilingi bilioni 8.5 kutokana na ukwepaji wa kodi wa kampuni ya Mafuta ya Lake Oil kwa kufanya udanganyifu kuuza mafuta ndani ya nchi Petrol lita 17,461,111.58 kwa kudanganya zilisafirishwa umefikia hatua nzuri.

"Takukuru imekamilisha shauri hili na mtuhumiwa wamepewa miezi miwili kurejesha mikononi fedha zote na kuwarudisha mahakamani endapo watashindwa kurejesha kiasi hicho,"alisema.

Alisema mbali na shauri hilo, wapo kwenye hatua nzuri ya kukamilisha uchunguzi wa kesi ya hati fungani ya malipo yaliyolipwa na kampuni ya Enterprise Growth Markert Advisor (EGMA), kiasi cha dola 6,000,000 kwa lengo la kuisaidai Tanzania kupata mkopo wa dola 600,000,000.

"Takukuru imebaini fedha hizo dola 6,000,000 zilitakatishwa na watumishi wa umma wasio waaminifu wakishirikiana na baadhi kutoka sekta binafsi huku wakijua fedha hizo wamezipata kwa njia haramu,"alisema.

Akizungumzia hatua aliyochukua rais, Dk. John Magufuli kwa kutengua uteuzi wa aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa RAHCO, Mhandisi Benhadard Tito kwa tuhuma zinazomkabili tayari wanachunguza shirika hilo la reli.

Alisema kulikuwepo na ukiukwaji wa kuwapata wazabuni kwenye ujenzi wa reli ya kisasa ya kimataifa(Standard Gauge) unaosimamiwa na Shirika la Hodhi la Reli Nchini(RAHCO), wanamekamatwa ikiwemo raia wa Kenya aliyekuwa kwenye mchakato huo, Kanji Muhando.

Kaimu huyo alisema shauri la kesi ya mabehewa ya kokoto 25 ya shirika la reili nchini (TRL), ya kukiuka sheria ya manunuzi ya umma Na.21/2004 pamoja na kanuni zake kutoka kampuni ya Hindustha Engineering and Industries Limited limekamilika.

"Uchunguzi umekamilika na tumeshapeleka kwa mkurugenzi wa Mashtaka kuomba kibali cha kuwafikisha watuhumiwa waliobainika kujihusisha na matendo ya rushwa na ukiukwaji wa sheria, taratibu na kanuni za ununuzi wa umma mahakamani,"alisema.

Alisema rais alijipa kazi ya kutumbua majipu hivyo aliwasihi watumishi wa taasisi hiyo kutumikia wananchi kwa eledi huku akibainisha tayari wanatekeleza azma na dhamira ya rais ya kupambana na rushwa.

Akitolea ufafanuzi swala la kumsubiri rais kutumbua majipu ndio taasisi hiyo ifanye ufafanuzi, Mlowola alisema taasisi hiyo imejipanga vilivyo tangu Novemba 20 mwaka jana wakati rais alipohutubia bungeni alipoonesha dhamira ya na nia ya dhati ya kupambana na rushwa na ufisadi bila kumuonea mtu haya.

"Nitoe rai kwa wananchi kutoa taarifa ili tuweze kujua kabla hatujapigwa, tukiweza kuisaidia serikali kuokoa fedha kabla hatujapigwa zitasaidia wananchi  kutoa elimu bure, upatikanaji wa dawa na mishahara mizuri,"alisema.

Alisema tayari wameshaanza kuchunguza madai ya aliyekuwa mkurugenzi wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), kwani tayari wapo hata viongozi wakubwa.

"Siwezi kusema kuwa kulikuwa na ulegevu, na hatua zimechukuliwa nchini imefikisha mahakamani mawaziri ila nchi ipo kwenye ufagio mpya hivyo tumeweka nguvu zaidi na hali zaidi,"alisema. 

Akizungumzia maofisa takukuru waliofukuzwa kazi na rais baada ya kukiuka maagizo ya rais ya kupata kibali cha kusafiri nje, alisema maofisa hao walikwenda kwenye mkutano wa taasisi za kupambana na rushwa uliofanyika Congo-Kinshasa.

Sunday, January 24, 2016

ISHA MASHAUZI JIJINI MWANZAHAIKUWA rahisi kuamini, lakini hivyo ndivyo ilivyokuwa. Mwimbaji nyota wa kikundi cha taarab cha Mashauzi Classic, Isha Mashauzi, hivi karibuni aliwaacha hoi mashabiki wake mjini Mwanza baada ya kutinga stejini akiwa na viwalo vya kileo.

 Uvaaji huo wa Isha ulikuwa tofauti na mavazi anayovaa awapo stejini, ambapo ni kawaida yake kuvaa magauni marefu ya kumeremeta kama ilivyo kwa waimbaji wengi wa taarab nchini.

Lakini siku hiyo Isha alivalia trucksuit nyeusi, raba na kofia nyeupe kichwani, mavazi yaliyomtoa vilivyo na kumfanya aonekane kama mwanamke kutoka majuu.

Isha alitinga na mavazi hayo stejini wakati wa onyesho la Baba na Mwana, kati yake na Mzee Yussuf lililofanyika kwenye ukumbi wa Villa Park mjini Mwanza.

Katika raundi ya kwanza ya onyesho hilo, Isha alivaa gauni la kawaida, kabla ya kubadili mwonekano raundi ya pili kwa kuvaa full trucksuit nyeusi na kuufanya ukumbi ulipuke mayowe ya kumshangilia.Picha kwa Hisani  ya MASHAUZI BLOG

Thursday, January 14, 2016

MANJANO DREAM MAKERS YATUA JIJINI MWANZA

Mradi wa Kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia Tasinia ya Urembo ujulikanao kama Manjano Dream Makers  hatimaye umefika Mwanza.Wataalamu wa Maswala ya biashara na Urembo Wataendesha Mafunzo Wiki ijayo Traehe 18.01.2016 Kwenye Ukumbi wa  Rock city Mall  Jijini Mwanza,Wanawake 35 wa jiji la Mwanza Watanufaika na mafunzo ya ujasiriamali kupitia vipodozi vya LuvTouch Manjano. 
Wanawake Wakazi wa jiji la Mwanza Mwanza Wanaopenda Kunufaika na Mradi huo  Wanaombwa Kujitokeza Kwa wingi Kujiandikisha siku ya Kesho Tarehe 15.01.2016 kuanzia saa Mbili Asb kwenye Ukumbi wa Rock  City Mall .
Mafunzo  yana Lengo la  kumsaidia mjasiriamali mwanamke kujikwamua. Awamu ya kwanza ni kumfundisha maswala ya Biashara namna ya kuibua na kubuni miradi mbalimbali namna ya kuandika Mpangilio wa Biashara ikiwemo Matumizi sahihi ya Rasilimali Muda, Fedha, Muda na pia namna ya kujitunzia akiba itokanayo na Biashara yake.Baada ya Wanawake hawa kuhitimu Mafunzo haya Taasisi ya Manjano Foundation inatoa Mikopo kwajili ya kuwawezesha Kuanzisha Biashara wakiwa chini ya Uangalizi Maalum wa taasisi hiyo kwa Lengo la Kuhakikisha kila Mhitimu wa Mafunzo haya anapiga hatua na kuweza Kujitegemea .
Wasiliana nasi kwa Simu namba +255 658 741 711 au +255 715 832 420

Tuesday, January 12, 2016

Diamond Platnumz - Utanipenda Behind The Scene Episode 2

Diamond Platnumz - Utanipenda Behind The Scene Episode 1

JULIANA KANYOMOZI ......

Black clothes are my favorite - Juliana KanyomoziSongtress, Juliana Kanyomozi reveals when it comes to fashion or any wardrobe related issues, she sides with black all the way naming it among her favorite colors.
It’s been certain of Juliana centering her fashion mostly around black and red colors. She also claims her love for black will force her to wear it every time she gets a chance to, which confirms why majority of her public and stage appearances were mostly made in black.
“My love for black though, I will wear it every time I have the chance.” the singer revealed to her fans.

I love wearing black clothes - Juliana Kanyomozi
I love wearing black clothes - Juliana Kanyomozi

Sunday, January 10, 2016

HATIMAYE MSANII WASTARA AOLEWA

WASTARA XIII
Mwigizaji Wastara na mume wake Sadifa Khamis Juma.
Wastara kapost picha kwenye account ya Instagram na kuandika haya >>’Nilikuwa kwenye usingizi mzito nimeshtuka nikakumbuka ni vizuri kuwapa asante wale wote walipiga goti kuniombea siku moja nipate faraja au tulizo la moyo ama stara kwa mwanamke wa kiislam kama dini inavyosema.. Japo kwangu nilikuwa nimeweka nadhiri ya miaka 3 ikipita basi ridhki ya mume ikija milango iko wazi alhamdulilah imekuja wakati muafaka na siku muafaka baada nadhiri yangu kutimia. Mungu ni mwema sana namuamini sana na ananipenda sana ndio maana kaniumba anavyojua yeye tumshukuru mungu kwa hili, najiombea na wale wenye nia njema na mim tuwe pamoja, iwe yenye neema ndoa hii aliyoipanga mungu pekee yeye ndie mwenye mamlaka juu ya hili barka, rehma, stara, uvumilivu ridhiki, upendo uwe juu yetu na bi mkubwa niliyemkuta aliyenipokea kwa mikono miwili kma mke mwenziwe msiumize vichwa tunajuana tunaheshimiana.’- @wastara84
Hizi ni baadhi ya picha zake nyingine alipost Wastara kwenye tukio zima la ndoa yake.
WASTARA II WASTARA III WASTARA IV WASTARA V WASTARA VI WASTARA

Monday, January 04, 2016

MH.RAISI JPM ATEMBELEWA NA VIONGOZI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Profesa Mussa Juma Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali CAG Profesa Mussa Juma Assad Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Abubakar Zuber Ally Ikulu jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mufti Mkuu wa Tanzania,  Sheikh Abubakar Zuber Ally, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania MheshimiwaDkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mkurugenzi wa Mashtaka DPP Bw. Biswalo Eutropius Mganga Ikulu jijini Dar es Salaam. 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Alhaji Abdallah Bulembo aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi ya Chama cha Mapinduzi CCM Alhaji Abdallah Bulembo Ikulu jijini Dar es Salaam. 

Picha zote na IKULU

Monday, December 28, 2015

UCHAGUZI MKUU WA MARUDIO KUFANYIKA ZANZIBARKAMATI Maalumu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Zanzibar chini ya Mwenyekiti wake Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein imewataka wananchi na wanachama kujiweka tayari na hatimaye kujitokeza katika uchaguzi mkuu wa marudio.
Kwa mujibu wa taarifa ya Katibu wa Itikadi na Uenezi Zanzibar, Waride Bakari Jabu, wananchi wametakiwa kujiandaa kwa uchaguzi wa marudio na kuachana na propaganda zinazotolewa na watu wachache kwa lengo la kupotosha ukweli.
“Kikao cha Kamati Maalumu ya CCM Zanzibar kilichokutana hapa chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar, Dk Shein kimewataka wananchi, wanachama na wafuasi wa CCM kujitayarisha kwa uchaguzi mkuu wa marudio ambao tarehe ya kufanyika kwake itatangazwa na taasisi husika,” imesema taarifa hiyo ya Waride.
Matokeo ya Uchaguzi Mkuu wa Zanzibar wa Oktoba 25 ulifutwa na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar (ZEC), Jecha Salum Jecha kwa kile alichoeleza ni kuwepo kwa ukiukwaji wa kanuni na sheria za uchaguzi huru wa kidemokrasia.
Katika kikao cha jana kilichohudhuria pia na viongozi kadhaa wa kitaifa akiwemo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, kilijadili ajenda mbili ikiwemo hali ya kisiasa mara baada ya uchaguzi mkuu kwa upande wa CCM.
Katika taarifa hiyo, chama hicho kimesema kimeridhishwa na mwenendo wa hali ya kisiasa na kimewapongeza wanachama waliojitokeza kwa wingi kushiriki katika Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 25.
Aidha chama kimepongeza na kutoa baraka kwa mazungumzo yanayoendelea ya viongozi wakuu wa kisiasa yakiwa na lengo la kuleta amani ya kudumu. Kamati ya mazungumzo ya hali ya kisiasa Zanzibar yenye lengo la kusaka amani ya kudumu iliyovurugika kutokana na kufutwa kwa uchaguzi mkuu inaundwa na viongozi wastaafu wakiwemo marais, Dk Salmin Amour, Amani Abeid Karume, Balozi Seif Ali Iddi ambaye ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Seif Sharif Hamad na Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein.
Akizungumza juzi Ikulu, jijini Dar es Salaam, Rais wa Zanzibar, Dk Shein alisema mazungumzo hayo yanaendelea vizuri na taarifa kamili yatakapofikia tamati. Alipoulizwa kuhusu hatma ya CCM kama uchaguzi mkuu utarudiwa, Waride alisema chama bado kiko imara na hakijatetereka.


“Wapo wanaosema CCM imeyumba, si kweli wala CCM haijapoteza majimbo kwa sababu kura hazikumalizwa kuhesabiwa,” alisema.

Sunday, December 27, 2015

Britain Sends £1BILLION In Aid To The World's Most Corrupt Nations Every Year

Misery for the residents of towns swamped by flooding - but Britain still sends £1BILLION in aid to the world's most corrupt nations

Misery for the residents of towns swamped by flooding - but Britain still sends £1BILLION
York drowns in the tide of filthy floodwater that has devastated swathes of the North. The scenes of misery across Yorkshire and Lancashire triggered outrage last night over Britain sqaundering cash on foreign aid. Residents asked why they had been told there was no money for local flood defences when £12billion a year is spent on overseas aid - including, it emerged yesterday, £1billion to the 20 most corrupt nations

PICHA YA LEO

Thursday, December 24, 2015

LADY JAYDEE ATONYA JUU YA KUHAMIA UJERUMANI


jaydeeJudith Wambura Mbibo ‘Jide’ au ‘Lady Jaydee’.

Stori: Na Brighton Masalu

MOYONI nina majonzi, sina tofauti na mpofu! Judith Wambura Mbibo ‘Jide’ au ‘Lady Jaydee’ kwa sasa hana makazi maalum Bongo, amehamishia makazi na shughuli zake katika ardhi ya ‘Kansela’ wa Ujerumani, Angelina Merkel kwenye Jiji la Born.
Katika mazungumzo yake na mwandishi wetu kwa njia ya simu, Jumatatu ya wiki hii, Jide ambaye alidai kwa sasa yupo nchini kwa Sikukuu ya Krismasi (kesho), alisema sababu zilizomfanya akapige kambi nchini humo ni kuchoshwa na maneno ya watu ambao kazi zao ni kutazama nani kafikwa na baya ili waeneze sumu ya maneno.
Kwa sauti ya ‘kibabe’ na yenye mamlaka, Jide alisema: “Lakini ukiachana na Ujerumani, wakati mwingine natumia muda mwingi kuwa nchini Afrika Kusini (Sauzi) kwa mizunguko ya kimaisha na kupumzisha akili yangu.”
lady_jay_dee3UJERUMANI ANA NYUMBA?
Jide: “Kwa sasa naishi hotelini, lakini kuna marafiki na jamaa zangu ambao wako kule. Kwa hiyo sina shida. Muhimu ni kukaa mbali na maneno ya watu wafurahiao matatizo ya wengine.
Kila mtu anageuka adui, ukiwa na mafanikio makubwa, watu wanajisogeza karibu, ukipungukiwa na jambo, haohao wanaanza maneno na kukusema vibaya, maisha hayatabiriki.”
HATAKI KUSIKIA MAPENZI!
Amani: “Vipi kuhusu mumeo, Gardner Habash, una mpango wa kurejeana naye?”
Jide: “Sitaki kusikia kabisa mambo ya mapenzi. Sitaki na usiendelee kuuliza upuuzi kama huo tafadhali. Si tu kwa huyo mtu (Gardner), hata kwa awaye yeyote, sitaki kusikia.”
ASIULIZWE KUHUSU MALI ZAKE!
Amani lilimuuliza Jide kuhusu ukweli juu ya madai kwamba amefilisika na kufikia hatua ya baadhi ya nyumba zake kuwa katika hatihati ya kupigwa mnada.
Jide: “Sitaki kugusia mambo hayo. Hata hivyo, umebahatika sana kupokelewa simu na kuzungumza na mimi, licha ya kuwa umejitambulisha unatoka Global. Sipendi mazungumzo na waandishi, hususan nyie wadaku.”
KUHUSU MUZIKI?
Jide: “Siwezi kusema nimeacha muziki, nipo maana ndiyo kazi pekee iliyonitambulisha.
Nawaasa mashabiki wangu waendelee kiniunga mkono, nawapenda sana na bila wao hakuna Jide. Lakini kwa sasa kuna mambo nayaweka sawa nje ya muziki.”
YUPO DAR AU KWINGINEKO?
Jide: “Kwa sasa niko Dar (Jumatatu), lakini keshokutwa (jana
Jumatano) nitakuwa nyumbani Musoma kwa ajili ya Krismasi. Niko kwenye mapumziko maalum ya sikukuu hiyo, lakini baada ya hapo, nitaendelea na mambo yangu mengine, ikiwemo kurejea Ujerumani.”

CHANZO: GPL

Tuesday, December 22, 2015

TAMASHA LA KRISMASS WIKI HII KUPAMBWA NA REBECCA MALOPE

MWIMBAJI nguli wamuziki wa Injili Afrika, Rebecca Malope (pichani) anatarajia kuwasili nchini Desemba 24 tayari
kuja kuungana na waimbaji wengine wa ndani na nje kupamba Tamasha la KRISMASS litakalofanyikaDesemba 25 katika Ukumbi wa Diamond Jubilee, jijiji Dar es Salaam.
Akithibitisha hilo jana, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya Tamasha hilo la kimataifa, Alex
Msama, Malope atawasili katika uwanja wa Kimataifa wa Julius Kambarage Nyerere
majira ya saa tisa alasili. 
Msama alisema
ingawa Malope atawasili kesho, wasaidizi wake watatua nchini leo kwa ajili ya
kufanya maandalizi ya awali kuelekea tamasha hilo ambalo tayari limekuwa gumzo kubwa kwa
wapendwa, wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili.
Alisema, mwimbaji
Faustine Munishi kutoka Kenya,
aliwasili tangu jana usiku akitokea huku mwimbaji Sarah K pia kutoka nchini Kenya, naye akitarajia
kuwasili kesho majira ya saa 10 jioni.
Msama mwasisi wa
matamasha ya muziki wa injili tangu mwaka 2000, alisema Solomon Mukubwa anatarajia
kutua nchini Ijumaa asubuhi na kueelekea moja kwa moja ukumbini kufikisha
ujumbe wa neno la Mungu kwa Watanzania.
Aidha, Msama ametumia
fursa hiyo kutoa wito kwa Watanzania kujitokeza kwa wingi kwenye tamasha hilo ili kurudisha
shukrani kwa Mungu baada uchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani.
“Nawasihi wapendwa
wa Mungu, wapenzi na mashabiki wa muziki wa injili, wajitokeze kwa wingi katika
Ukumbi wa Diamond Jubilee tuburudike pamoja na kumrudishia Mungu shukrani baada
ya kuvuka salama katika Uuchaguzi Mkuu uliofanyika kwa amani na utulivu,”
alisema Msama.
Kwa upande wa viingilio
katika tamasha hilo, ni shilingi 50,000 kwa Viti maalum, VIP shilingi 10,000,
shilingi 5000 viti vya kawaida na shilingi 2000 kwa watoto.

“Viingilio
tulivyopanga vitasaidia wenye uhitaji maalum kama
yatima, walemavu, wajane na wengineo ambao wanahitaji msaada,” alisema Msama.
Waimbaji wengine
katika tamasha hilo ni Rose Muhando, Upendo Nkone, Jesca Honore, Christopher
Mwahangila, Joshua Mlelwa, Martha Mwaipaja, Christina Shusho, Sifael Mwabuka,
Kwaya ya KKKT  Yombo na Kwaya ya
Wakorintho wapili ambayo itazindua albamu yake ya Mchepuko sio dili.
Waimbaji wa nje ni
pamoja na Rebecca Malope (Afrika Kusini), Sarah K, Solomon Mukubwa na Faustin
Munishi ‘Malebo’  (Wote kutoka Kenya).Msama alisema mgeni rasmi katika tamasha hilo
ni Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnauye