Enzi hizo ukienda Rungwe Oceanic Beach Resort ya Mzee Mwakitwange ulikuwa unakuitana na majina kama vile DJ Ngomely, DJ Pop Juice na wengine. Ukiosea jirani na hapo Rungwe, yaani Silver Sands, unakutana na kina John Peter Pantalakis, Choggy Sly na Kalikali ambaye baadaye alihamia YMCA.Ukienda Africana ulikuwa huangalii simba aliyekuwa anafugwa hapo, bali pia DJ Mehboob, wakati ukishuka mjini hususan Motel Agip na baadaye New Africa hotel ghorofa ya saba kulikuwa na DJ Emperor (huyu Joseph Kusaga bosi wa Clouds 88.4 fmunaemjuea), Boniface kilosa a.k.a Bonny Love na DJ Jesse Malongo (wa Club Afrique, London).Baadaye kidogo ikaja Space 1900 iliyoanzia hoteli ya Mbowe na kuhamia YMCA, na kuleta ushindani mkubwa kwenye fani ya muziki ambapo disko lilifunika kabisa muziki wa dansa. Vile vile ikazuka New Vision ambako DJ Super Deo, DJ Paul MacGhee na Joe Johnson Holela walitengeneza majina sio kawaida, huku wakimpa darasa DJ Young Millionaire ambaye sasa anatamba Star TV ya Mwanza akiwa na jina lake halisi ya Jacob Msungu, kwenye kipindi chake cha TV cha Roving DJ.Baada ya Space 1900 discotheque kuhamia YMCA, disko la RSVP Discotheque likazaliwa Mbowe na Ma DJ wake walikuwa mkongwe Saidi Mknadara a.k.a DJ Seydou, akisaidiana na DJ Yaphet Kotto.Kwa ufupi, pamoja na kwamba DJ Eddy Sally na DJ Sweet Francis wa hoteli ya Keys mtaa wa Uhuru walikuwa juu kwa vyombo vya kwanza vya kisasa vya disko, lakini ni DJ Seydou na DJ Yaphet Kotto ambao ndio walikuwa vinara pale RSVP Mbowe. Yaani baada ya kuruka majoka kila sehemu uijuayo, lakini vijana wote wa Dar walikuwa wanakwenda Mbowe kumalizia usiku kwa DJ Seydou na DJ Kotto.Kwa ufupi huyu ndiye aliyekuwa baba wa disko Dar, sio pekee kwa uwezo usio wa kawaida wa kupanga muziki tu bali pia ngekewa ya kupata nyimbo mpya mpya kabla ya DJ yeyote nchini.
Comment by Ebbie Janson
Michuzi hapa patamu lakini kidogo nikupe somo la huyu mkongwe wetu.
DJ Seydou alianza shughuli hizi pale Sea View enzi za Sansui miaka ya katikati 70…akipewa muda mfupi sana kwani enzi hizo Afro 70, Safari Trippers walikuwa ndio ngome ya jiji ktk muziki. Maneno yote yalikuwa Princess pale mnazi mmoja.
Nakumbuka mwaka 1980 Dj Seydou akishirikiana na Eddy Sally na Choggy Sly walianzisha disco pale Key’s Hotel hapo mjomba hakuna YMCA wala Msasani isipokuwa Mbowe Dj akiwa Gerry Kotto (sio Yafet Kotto), Africana na Seaview.
Nakumbuka walifanya mashindano ya kucheza na mshindi alikuwa Golden hair (Abdallah) na Mosi Ally yule mkimbiaji wetu wa mita 100.
Mwkaa mmoja tu walisambaratika! Choggy na Eddy Sally walikwenda Silversand na Seydou pamoja na Gerry Kotto waliungana kuunda kikundio kipya cha Space 1900 pale YMCA. Hapo ndipo Joe Janson na Kalikali walikuja ibuka hata ilipofika mwaka 1982, Space 1900 walihamia Mbowe. Kule YMCA wakawa wanapiga disco la mchana kwa vijana wadogo. Space wakafungua tena sehemu mbili New Africa na huko Moshi pale YMCA ama Moshi Hotel..
Mwaka 1982 kweli madisco yalifunika kabisa miziki ya magita!.Msasani, Rungwe, Slversand,Italian club (clouds), Keys Hotel, Motel Agip, New Africa, Twiga Hotel, Dar Institute na sehemu nyingine kibao ambazo siwezi kuzimaliza.
Seydou alikuwepo Mbowe hadi 1985 wakati Freeman alipoamua kufungua RSVP kuwaondoa Space 1900 ambao walihamishia makazi yao sewhemu mbili New Africa Hotel na Pale Maggot.
Toka wakati huo Seydou hakuwa na mahala maalum kwani Space 1900 ilivunjika kutokana na matatizo ya ndani. Hata hivyo jina Space 1900 liliendelea kutumika na ndio vijana wengine akina Super Deo,Young Millionea wakaibuka.

Comment by Bob Sankofa
Shule hizo mbili zilizotangulia hapo juu ni historia tosha. Lakini BC, nitafurahi zaidi mkiweza kumtia DJ Seydo mkononi na kumpiga mahojiano, tusikie toka kwa perspective yake.Kutokana na wachangiaji wawili hapo juu inaonekana wegine tumezaliwa katika kipindi ambacho Disco lilikwisha poteza ile ladha ya “disco”, au naona hivyo labda kwa sababu sikuishi wakati halisi wa Seydo? Wengi siku hizi tunakwenda sana disco lakini hatuwajui ma-DJ wetu kama mnavyowafahamu wa kipindi kile. Maana kuwa na historia ya mtu fulani sio mchezo.
Comment by danieli
I’ve received this news with a mix of nostalgia, sadness and gratitude. Ni furaha kumuona huyu icon wa enzi zetu za disco bado anadunda–wengi waliokuwa kwenye fani ile walishadedi shauri ya fast life. Nostalgia kwa kutajwa hizo kumbi ambazo ukiingia ndani beats zinaubox moyo wako directly–wao,man gedanonit, geddannonit, whwatyagonado ifyoudon’wanna dance bystannndin’ on the waaall!Sadness kumuona seydou amekuwa kinyume sana na yule shupavu mkandamiza-santuri, ningependa kumuona pamoja na umri lakini yuko yuko kama trade ilivyo, kama mzee syke tumuonavyo na li-bike lake na hereni shingoni, get me
Comment by Juma Maringo
Ee bwana hapa BC mmeniacha hoi kwa furaha.Hiyo miziki imenikumbusha mbali sana.Enzi hizo ukisikia disco ni disco kweli.Habari na miziki namna hii poa sana.Keep it up guys!
Comment by muddy
‘keep it up’ baada ya DJ Seydou tupeni pia vitu vya Ma Djs wengine wakali wa enzi hizo wapo wapi na wanafanya nini kwa sasa!Comment by fidelis m tungaraza on August 31st, 2007 6:48 am[Image]
fidelis m tungaraza Says:
Mlionitangulia asanteni kwa michango yenu. Nami naomba nichangie kwa sababu disco era ndiyo ulikuwa wakati wa ujana wangu. Na ndiyo kilikuwa kipindi cha disco haswa kuanzia New York (Saturday Night Fever). Kati ya mwaka 1978 na 1985 baada ya hapo Break Dance baada ya Break Dance sijui la kusema…Safu ya Madj wa wakati huo kwa ninaowakumbuka miye walikuwa kina Justin Kussaga (SANSUI hadi BIRIBI/CLOUDS toka Sea View mpaka Italian Club). Eddy Sally(FM Disco), Gerald-Gerry Kotto- (Mbowe au kwa jina la utani wa wakati huo CHOONI), John Bure(Rungwe), Mehboo na Clemency/t?(Gogo Disco na Floating Bar, Africana), Abby Sykes(Blowout Disco, YMCA), Ebonite WooJack(Uptown, Disco YMCA)baada ya haya madisco mawili ndipo Sudi Mwarabu akaleta Space 1900 YMCA, Madj Gerry Kotto na Seydou. Madj hawa wawili walikuja na staili mpya kabisa ya kupiga chapati (santuri) na dawa za mbu (kanda) huku wakidansi behind the Dj desk. Kwa mtakao kuwa mnakumbuka mtakumbuka ndiyo waliokuwa madj wliokuwa wanachoreography dansi zao na wanaovaa sare ya kazi maovaroli. Jamaa walikuwa watamu sana.Ok Tuendelee, Msasani Beach lilikuwepo disco la Marehemu? Nassoro Born City (Nasikia alifariki mwaka jana sina uhakika). Hapa ndiyo walipoingia kina Choggy na John Peter na baadaye Nigger J na Kalikali. Au siyo?Kama sijakosea mwaka 1982 au 83 likavuma JeSet Disco na Dj Rusual na Baadaye Young Omar, Msasani Beach Club. Ninaweza kusema mpaka sasa hivi katika historia ya burudani ya muziki hakuna disko wala bendi lililowahi kutengeneza matangazo makali kama JetSet Disco. Kwa mnaokumbuka mtaweza kukubaliana nami. Nadhani kazi ile ya matangazo ilikuwa ni ubunifu wa Mzee Fred Jimmy Mdoe na mwenziye Bwana Bakari Omari. Jet Set hawakuwa na miziki mizuri lakini walijua kutengeneza aina ya wateja na mashabiki.Wakati wote huo Princess hotel kulikuwa na Parliament Disco la kina Joe na Eddo. Nilichokuwa nakizimia Parliament Disco ni mafunk beat waliyokuwa wanayabaruza. Halafu lilikuwa disko la watoto wa mjini sina maana mbaya katika hili lakini lilikuwa ni disco la watoto wa mjini kwa maana ya watoto wa mjini kweli.Bila kusahau Pango Disco, Rex Hotel Clock Tower na lile la Continental Hotel, Nkrumah Street.Zama ninayoizungumzia hapa mahoteli ya ukanda wa pwani ulikuwa bado umeshikwa na mabendi isipokuwa Rungwe Oceanic kwa Dj John Bure.Yakaja madisko ya maghorofani Motel Agip na New Africa Hotel. Madisko haya ndiyo yaliyokuwa ya mwisho mwisho na wateja wake zaidi walikuwa vijana wapya wapya, sina maana mbaya kwa kuwaita wapya wapya. Walikuwa wapya kwa sababu hawakuwa maaluatani wa jiji wengi wao walitokea mitaa ya ushuani na attitude za kiushuani. Kweli si kweli?Bendi zilizotamba wakati huo: Brass Construction, Con Funk Shun, Earth, Wind, and Fire, The Isley Brothers, The Jacksons, Osibisa, Ross Royce, Soul Brothers, Lakeside, Kool and the Gang, Commodores, Orchestre Veve, Super Mazembe, Le Mangelepa, TP Ok Jazz, The Parliament, Fela Ransome Kuti and Afro 70, Simba Wanyika, The Wagadugu, Bunny Mack, Third World, Zappow. Jamani, nisaidieni nimezeeka kumbukumbu inavia. Madisko ya wakati huo miziki ilikuwa mchanganyiko lakini miziki ya Kimarekani ilikuwa ndiyo inatawala.Mziki iliyotamba You can do it, Kulukuni, Moni afinda, Shakala, Sina makosa, Let me love you, Sweet mother, Easy dance, Ladies night, Sail on, Why you wanna try me, You give me fever(Love to love you darling), What you waiting for, Shake your body down to the ground, Lift up the roof, Holding on, Love’s got me dancing on the floor,This is reggae music, Night fever, Staying alive, na mingineyo mingi.Asante sana kwa kutukumbusha mbali.F M Tungaraza.Comment by julius. L on August 31st, 2007 11:12 am[Image]Kweli huyo mtaalam wa hapo juu, F M Tungaraza, amesema na mimi nimemsikia. Kwa kifupi kamaliza yote, “BC” mnatukumbusha mbali sana, kumbukumbu zenye kuleta furaha, na zile za majonzi kwa wakati ule “nilivyokuwa natoroka nyumbani kwenda Disko, mfukoni nikiwa na pesa ya kiingilio tu, sina pesa ya soda na wala sijui nitarudi vipi nyumbani” na nikifanikiwa kurudi nyumbani kwa kudandia lifti za washikaji, najitayarisha kupokea viboko kutoka kwa wazazi.
Keep it up BC Mnafanya kazi ya Pongezi.JL

Tungaraza, inabidi tuwasiliane..maanake umemaliza darasa zima la ma disco, duh mozo weee!
MD ukiwataka hawa jamaa wote wasiliana na mtu mmoja anaitwa Kim and the boyz at 255-78715560 Mtoto wa mjini atakupa data zote.
MD ukiwataka hawa jamaa wote wasiliana na mtu mmoja anaitwa Kim and the boyz at 255-78715560 Mtoto wa mjini atakupa data zote.
Comment by zungu
ningependa kukumbushia list kamili ya clouds enzi za motel Agip,bahari beach nk.MOTEL AGIP djs walikuwa DJ EMPEROR(Boss wa CLOUDS FM),DJ BABYFACE (Boss wa CLUB AFRIQUE LONDON)na DJ JT (Julius Tandau)BAHARI BEACH walikuwepo ma djs BONNY LUV pamoja na ALEX SHABA
Comment by f m tungaraza
Ebbie Janson,Umenistua na hiyo “..Mozo weee!..” Hiyo Mozo wee wape pia wakongwe wengine wa madisko kama kina Justin, Gamba na Joseph Kussaga, Super Deo, Deo Kiuno, Machumu Spear aka Alhadji Sulemain Ladha, Mkandaras i.e.Seydou, Siri,na Abdallah, Ray Mtimba, Kidai, Pius Ntare, na Bonny ‘Luv’ Kilosa wataielewa.Nilipomaliza kuandika nikakumbuka pia kulikuwa na Studio 55, Dj Ali Kayaya na baadaye Cool Joe. Halafu lilikuja Airbone disko la mafundi ndege au marubani wa ATC walitoka Holland kusoma lilikuwa pale Forodhani Hotel.Nikakumbuka pia JetSet nilisahau kumtaja Dj Ibrahim Killer. Gerald, Killer, na Karl(Mzungu) Maboblish walikuwa na show zao ya viatu vya magurudumu.Halafu madisko ya maghorofani lilikuwepo XTC Disco la kina David Kiango na Eddy Jackson Twiga Hotel. Hili lilikuwa disko la kibillahtiih haswa!Kumradhi, Julius L wewe Julius L yupi? Nikikupa hint ukazipatia basi tuwasiliane. Ok, wakati wa halftime Uliwahi kula chips dume na maembe ya Mzee John? Kunywa chai na chapati Girl Guide? Tangawizi na maandazi nje ya fensi ya shule? viazi mbatata vya Mzee Machale? Na aisi krimu za vifuko za kwenye madeli na chachamawa?
Nyumbani kwenu kulikuwa pale kona? Marehemu Juma mlikuwa mnaishi mtaa mmoja. Marehemu Adili mtaa kabla ya wa kwenu ukitokea shule? Kama ndiwe na ungependa tuwasiliane chukua mawasilano yangu kwa moderator BC.PS/ KUNA JAMBO NASHINDWA KULIELEWA..HIVI KWA NINI HADI HII LEO CLOUDS DISCO, MSONDO NGOMA, IKHWAN SAFAA NA THE TANZANITES HAWAJAPEWA TUZO YOYOTE KWENYE KILIMANJARO AWARDS KWA UTUMISHI WA MUDA MREFU KATIKA FANI YA MUZIKI TANZANIA? SANSUI-BIRIBI-CLOUDS DISCO WANAFIKISHA TAKRIBANI MIAKA 35, MSONDO MIAKA 45, THE TANZANITES MIAKA 40, IKHWANI SAFAA MIAKA 101, MIAKA MIA MOJA NA MOJA! NAWAOMBENI WAZEE MLIOKO UWANJA WA NYUMBANI HAMASISHENI HILI SUALA!F M Tungaraza

Comment by dj tom in japan
mhhh niko form one pale forodhani sec school,natoroka nyumbani na kurudi home kimya kimya tena kwa kuruka ukuta,dingi akinistukia basi halali na ananisubili the whole night akiwa na zana zote za kivita!!!!
unacheza disco pale maggot huku uliangalia saa usije ukalimiss UDA la mwisho,na likija limeshajaza lumbesa toka huko lilikotoka !!! mambo yenyewe ni kunin`ginia mlangoni kwenda mbele, mabasi ya UDA wakati ule yalikuwa hayana mlango wa kufunga ni open door style, konda akija unatoa kitambisho cha mwanafunzi kumbuka time hiyo ni saa tano usiku basi usubili vagi la konda!!!!!!
wee acha tu hayo ni mambo ya 80′s bwanaaa!!!!

Comment by Isaac Kibodya
Fidelis asante sana kwa kumbukumbu nzuri, kwa sababu nimezisoma habari zote za mwanzo na kuzifagilia sana ila moyoni nikawa nasononeka kwa kuto ona habari za Disco Parliament. Hili hasa lilikuwa disco la watu wawili Eddo (baharia)mtafutaji na Joe Shawa mhangaikaji yeye hakusafiri alibaki nchi kavu kutesa.Wakati Eddo alipokuwa akija nchini basi alikuwa anashika shika vyombo na yeye lakini shughuli hasa ilikuwa ya Big Joe na DJ Slaughter!
NA wala hukukosea Fidelis pale uliposema hili lilikuwa disco hasa la watoto wa mjini kwani hata Fabulous Four wakina Sabrina wakitoka Rungwe lazima wapite Parliament kabla ya kwenda kulala! Na hili ndilo trupu la shoka kwani Joe alikuwa na wasaidizi wengi na wote watu wa shughuli hasa hasa magorofani Lumumba na wasichana wote waliokuwa wakija Princess.Man! mmenikumbusha mbali mno..nami bado mwana Parliament ndani ya moyo wangu!Comment by stambuli on September 6th, 2007 1:28 am[Image]Nawafagilia washkaji wote(Vijana wa Nyerere) waliotupa History ya huku nyuma kwetu ni somo tosha kwa sisi vijana wa(Mzee Ruksa),ama kweli mli enjoy ujana wenu,Naona kama ndio ukimwi ungekuwa umeshika kasi kama kipindi hiki asingebaki mtu,watu wangepukutika kama senene,kwa maana nasikia Disco lilikuwa halinogi bila totoes pembeni.Wakongwe kuna hawa ma-dj wa siku nyingi Chris Phabby na Rachy Kutty (Rafa). Nakumbuka Rachy Kutty alikuwa JetSet Disco kule Msasani Beach Club. Inabidi kamati ya Kilimanjaro Music Awards ianzishe zawadi ya watu waliotoa mchango mkubwa katika fani ya disko na muziki Tanzania.

Comment by Kikolo
Wachangia hoja mmenifurahisha sana kwani ma – Dj hawa walipokuwa wakivuma, vijana wa sasa wengi walikuwa wadogo. Wengine tulikuwa tukitoroka hata shule kwenda kwenye disco kwa Kalikali, Seydou na wengineo bila hata kuwajua sawasawa! Michuzi umenifurahisha sana kwa kusema Young millionaire ndiye Jacob Usungu wa Star Tv Mwanza.Endelea kutupa historia kama hizo.
Comment by Exuperius
Yaani,wadau mmenitoa chozi kwa kutukumbusha hayo ma-disco na ma-DJ wa enzi hizo za ujana wetu.Unatamani kama kungekuwa na uwezekano kurudisha wakati nyuma ili kwenda kuyarudi ma-funkies tena lakini wapi!!
Tunashukuru kwa kutukumbusha tulikopitia. Ndugu zangu mmenipatia changa moto ambayo imenisimua ile mbaya kwa kunikumbusha enzi za ma DJ wa wakati ule. Pale Mbowe kulikucha na haswa akina DJ Seydou na wenzake walipokuwa wanatoa ngoma kama ile ya CHAKA KHAN (Ai’t No Body); basi stage ilikuwa inafurika kwa namna yake. Tusisahau na ngoma 3 za kupakatiana (Blues)na hapo Seydou alikuwa ni hodali kwa kukutangazia kwamba asiye na mwana aeleke jiwe. Doo! kweli ulimwengu ni mdogo!! Nakumbuka I used to admire Dj Seydou’s hair dooo (Afro). Keep up a work BC

.Comment by gasto
BWANA MDOGO FIDE TUNGARAZA NAONA HUJAMBO KWA HISTORIA, ILA UMESAHAU KAMA MBOWE KABLA YA KUJA SPACE 1900 DISCO KULIKUA NA DISCO AMBALO SIKUMBUKI JINA LAKE NA LILIKUA HALITANGAZWI GAZETINI WAKATI HUO BIRIBI LIKO MOBILE NAMAANISHA LILIKUA MARA LINAPIGA MUHIMBILI PARAMEDICAL NA NURSING PALE MBOWE KIPINDI HICHO ALIKUEPO MTU MZIMA DJ FRACO UKIPENDA UTAMWITA FRANCO SAFARINO B, BIRIBI IKAFIFIA IKAZILIWA CLOUDS DISCO PALE SALEDER BRIDGE,NDIPO SPACE 1900 IKAJA MBOWE MA DJ WAKIWA SEYDOU NA GERALD(JERRY KOTTO) KABLA HALIJA GAWANYIKA MZEE SEYDOU AKACHUKUA SPEAKER ZAKE NA KWENDA KUANZISHA DISCO LAKE AKIPIGA PALE CBE, NA SUDI SPACE AKAUNDA NEW SPACE PALE MBOWE MA DJ ALIKUWA GERALD NA JOE IKAJA VISION PALE USHIRIKA CLUB(MAGOT)
Comment by mambo za zamani
jamani vipi wa zamani mmewasahua wengine kina dj lukehawa nao wa zamani sana nao enzi zao zilkuwa sio kawaidComment by mambo za zamani on March 17th, 2009 7:33 pm[Image]Ma dj wanzee kina kali kali luke chogi sly kina bony love kina kusaga .. Amani watu wanatoka mbali
Comment by Bilal
Mzee Tungaraza umenikumbusha zamani sana lakini mbona umewasahau THE GAP BAND II hawa walikuwa ndio wazee wa mafunk pia umemsahau DJ mmoja kwa jina Master Funk Rasheed alikuwa anapiga disco la Biribi enzi hizo yMCA vile vile umenikumbusha akina Richard Mazula akipiga na Joe Johnson Mbowe tulikuwa tunapaita Club enzi hizo ukiondoka nyumbani unawaaga wazee kuwa unakwenda Club means disco la Mbowe,halafu vile vile likaja disco laRSVP likichezwa club Maggot pale napo palikuwa ni kiama si watoto hao utafikiria mvua ya masika,ilikuwa ni raha tupu enzi zetu,tumecheza disco na akina marehemu Abby Senga na akina Miriam Jogi na akina Ceci na Dada yake Bupe kina mzee Becken wa Kariakoo na wote akina Senga na akina Mwamed Mbange na rafiki yake Edga Fongona watoto waIlala wote akina marehemu Franco na akina Bolt na akina Robert Rwebangira na halafu sundays tulikuwa tunamalizia Masaki Beach watu wanajimwaya na maredio cassetes yaani enzi hizo sijui la kusema ilikuwa ni raha tupu,jumatatu utakutana na wakali wote wanajimwaga coffee bar pale extelecom kupata cold coffee.Mimi nikimuona yuile Freeman Mbowe pamoja na ndugu yake Charles Mbowe huwa ninawaheshimu sana kwa kutuweka vizuri sana wnzi zetu hata baba Suma naye alikuwa akitupatia entertainment za comedy zake nasikia Ray Abdul kisha vuta siku nyingi sana,bado ninawakumbuka wakali wengi sana siku hizo mabaharia walikuwa kibao Mbowe kila anayeshuka ni lazima ashuke Mbowe kunuona mzee Makochela (Jaws)na mpiga picha wetu alikuwa ni Spear hata hata kabla ya Michuzi zamani mpiga picha wetu mkubwa alikuwa ni Bob Spear akitembea narafiki yake Abdalla Golden Hair wa Stake in,hiyo ndiyo ilikuwa Dar sio hii ya leo sijui ya mapedeshee ni ushamba mtupu na ulikmbukeni.Willy
Toronto
Toronto
Comment by Kipara
Naam Ndugu Willy hapo umenena mambo yalikuwa enzi hizo halafu ukisha toroka nyumbani bila hata ya kuwa na shilingi moja mfukoni unasubiri kupigwa muhuri na washikaji ili uingie ndani tana unapita mbele ya yule mdogo wake na Seydou kwa jina ni Abby Johnson au Abdallah Mkandara ndiye akikaa mlangoni yeye na nzee Frem kama bouncer pale mbowe yule mzee alikuwa ni mnoko kishenzi usichezi naye halafu baadaye tunamalizia kwenye chips za masalad pale mtaa wa swahil kariakoo.nakumbuka kuna siku niling’ang’aniwa na mtoto mmoja wa kike nilipokwenda club Mbowe na hata hela ya kumnunulia drink nilikuwa sina mfukoni lakini mshikaji wangu Spear alinibeba kwa kuniunganishia ka ishirini moja ambazo enzi ile iliweza kusaidia sana mtoto akapata bia yake moja na chips na mishkaki,yaani Bob Spear siwezi kumsahau kwa hilo jambo baadaye nilibeba mwana hadi kwetu.Zamani kulikuwa ni kutamu sana
Comment by Kipara
Nyie kiboko kweli enzi hizo zilikuwa ni enzi za ubaharia sio unga ,watu walitengeneza maisha yao kupitia njia za halali na wala sio za haramu,pesa zilikuwa zinajitengeneza kiukweli hakuna uuzaji wa bangi au unga wenu ka ilivyo siku hizi ,utamu wote wa starehe umekwisha mambo yalikuwa ni enzi hizo jamani leo mmeamsha mshipa mkubwa wa damu mwilini mwangummenipeleka enzi zangu wakati hata ndevu zilikuwa bado kuniota enzi za ubitozi ,tukishindana na mabitozi wa Tambaza na kariakoo na gerezani ndio walikuwa mabrazamen wa enzi hizo Mbowe disco halichezeki bila watu kutoka sehemu hizo kuwepo ndani ya ukumbi wa mbowe mambo yalikuwa ni matamu sana tuli enjoy maisha kweli kweli hakuna cha ngoma wala ukimwi enzi hizo kila kitu bila uoga wowote ule ni starehe kwa mbele tu,hata dada zetu nao walikuwa ni wakali sana enzi hizo .Nakumbuka nilikuwa ninamuona HE JK raisi wetu akija kucheza madebe Mbowe enzi hizo hata pia colonel Kimbau yule wa JWTZ naye alikuwa hakosi Mbowe yeye na family yake wote hawa wakubwa tumecheza nao disco la Mbowe,huyu mtu JK ni vigumu sana kumshinda kwani yeye kajichanganya na umma siku nyingi sana ni mtu wetu kwa sana,kama kuna mtu haniamini basi muulizeni Abby Johnson Mkandara akupeni taarifa zote hizi nilizoziweka hapa.Pia mmemsahau DJ mmoja wa disco la The Parliament akiitwa AGI SHOW,kati ya madj’s wa kwanza waliokuwa wakiongozwa na mzee SAYDOU ,walikuwa akina GERRY KOTTO,JOEJOHNSON HOLELA,EBONITE WOO JACK RICHARD MAZULA,halafu wakaja akina KALIKALI NA MZEE MZIMA CHRIST PHABY siwezi kuendelea zaidi na story ya chuo kikuu cha discos nchini chini ya mzee SAYDOU MKANDARA kama mwalimu mkuu na proffessor wetu enzi hizo.Yaani mpaka najisikia kulia hivi sasa kwa jinsi kumbukumbu zilivyoniingia akilini mwangu.
Endeleeni kutoa vitu vya zamani hapa
Endeleeni kutoa vitu vya zamani hapa
Comment by Mtani
Kumbukeni kwanza kipindi hicho DJ Kalikali alikuwa bado anachoma nyama kule Uwani Mbowe wakati wazee wazima akina Saydou na Gerald Koto wakiyapiga madebe,yeye alianza kuachiwa achiwa kushika vyombo mara moja moja na baadaye akaibukia katika disco la marehemu Nassor Born City walianzia kupiga pale YMCA,enzi hizo watu tunaishi SIDO HOSTEL au Holiday INN Hotel tukifanya magam u ya kupata rizki ,wakali wote waliishi Holiday INN enzi hizo,nawakumbuka akina Rajab Katimba,Mohamed Kassim Juma,Bob Spear, David Kizito,Abdallah Mkandara,Holela hata naye Gerald alikuwa akiishi pale mara moja moja vile vile tulikuwa naye SOUD MWARABU aliyeanzisha SPACE 1900 yeye na Saydou enzi hizo,group lote hilo lilikuwa ni la watu kutoka Mwanza zamani sana mjini Dar vile vile nimemsahau Abdallah Golden Hair wa Stakeinn restaurant na ndugu yake Adamu Khan.ndugu zanguni enzi hizo ushirikiano ulikuwa ni wa hali ya juu sana,tulikuwa tunapeana deals kama mchezo bila roho mbaya yeyote ile.Ninamkumbuka mzee Saydou alikuwa anaingia na debe la Donna Summer na halafu baadaya hapo analimwaga chacha la Santana Black majic woman na Oye Comova,alikuwa hakai mtu chini hapo watu wote ni lazima kusimama kulicheza chacha,sina uhakika ka watoto wa kileo ka wanajua kulicheza chacha tuliokuwa tukilicheza wakati mzee mzima Saydou akituchengua na madebe yake utafikiria ilikuwa ni uchawi hivi yaani mpaka leo zile raha bado tunazikumbuka ,ilikuwa shughuli kubwa sana enzi zetu.Lakini tunabahati sana kama mchangiaji mmoja hapo juu kaandika kuwa ka ingelikuwa ni enzi hizi za ngoma tungeondoka wengi sana maana watoto walikuwa ni wa kumwaya ni kujichagulia mwenyewe tu.
Comment by Nyange
musiisahau vile vile na bendi yetu ya Barkeys wale watu walikuwa wanayacopy madebe copy right utafikiria ni wao ndio wameyatunga,starehe ilikuwa ni kubwa mno kipindi kile katika lists zenu msimsahau Vile vile Bob Ritchie kwa jina lingine la utani walimwita Richard Boom huyu alikuwa akiyafanya manjonjo yake Mbowe karibu kila siku ukienda pale Mbowe utamuona yupo yupo,Freeman alikuwa anatimu kubwa sana na kuna wakati nilikuwa ninamuona ka yeye ni Rocket scientist kumbe mchawi mwenyewe behind yote haya alikuwa ni mzee mwenyewe Saydou Mkandara ilikuwa si rahisi sana kumtambua nafasi yake kamili yeye alikuwa ni low profile sana ilikuwa si rahisi kujua kama yeye ndio mzee wa calculations zote alizo kuwa anazionyesha Freeman Mbowe,muda unakwenda sana mimi sugestions zangu ni kwamba huyo mzee Saydou ni vizuri kama angetafutiwa vyombo vya kileo na wenye uwezo wa kufanya hivyo na halafu afunguliwe ukumbi maalum kwa wazee wa enzi hizo hapo utaweza kuingia kwa membership tuu na usajili wake ni wa kulipiwa kwa wateja maalum tuu ,bila ya wewe kuwa ni member wetu basi huruhusiwi kuingia mpaka specialy kibaly tuu,ina sound kama kichekesho lakini hilo linawezekana kabisa kama kutakuwepo na ushirikiano mkubwa hata JK mwenyewe ninao uhakika kuwa atajumuika nasisi kwenye hilo jambo,i know that some people will start to cry foul that tunaleta ubaguzi nchini ,ni wazi kutofautisha class za watu ,sisi ni kizazi kingine kabisa,makulio yetu yalikuwa ni tofauti sana na haya ya leo,enzi hizo humkosi junior yeyote kutokuwa na novel ya James Hadley Chase mfukoni mwake,ninauhakika karibu kila kijana katika ujana wake ameisha soma zaidi ya Chase mia mbili na ushenzi,ni lazima tukubali kuwa sisi ni watu tofauti sana na wenzetu hii leo na we deserve something of our taste and our class,we are so hippie man ,kila siku mimi ninamweleza junior wangu kuhusu hilo na anaonekana kutonielewa vizuri sana wao ndio wanajiona wako hippie zaidi yetu pamoja na kuvaa suruali zinazo wateremka nyuma na kuonyesha matako yote wazi huo ndio ujanja kwao,naomba tuzidi shirikiana zaidi tumuibue upya huyu Nguli wa Disco nchini.mzee Nyange
NYC
NYC
Comment by Abu
THIS REAL REMINDS ME ON OUR GOOD OLD DAYS!!! HAKIKA MCHANGO WA DJ SEYDOU KTK FANI YA DISCO HAPA NCHINI NA EAST AFRICA KWA UJUMLA NI WA KUKUMBUKWA DAIMA..MENGI YAMEZUNGUMZWA NA WALIONITANGULIA LAKINI NAPENDA KUELEZA PASIPO KUUMA MANENO KUWA DJ SEYDOU NA WENZAKE WA ZAMA HIZO WALIKUWA NI WATU BRIGHT KWELIKWELI..:
1. WALITAMBUA KWAMBA DHAMANA YA STAREHE YETU VIJANA NA WAZEE WAPENDAO DISCO ENZI HIZO ILIKUWA MIKONONI MWAO.
2. WALIUKUBALI NA KUUHESHIMU WAJIBU HUO.
3. MARA ZOTE WAO (DJs) WALIKUWA WAKISHINDANA KURIDHISHA WAPENZI/MASHABIKI WA DISCO.
4. SIKUWAHI KUSIKIA BIFU ZA KIPUUZI BAINA YAO KAMA ILIVYO KWA WADOGO ZETU SASA HIVI. BIFU YAO KUBWA ILIKUWA NI KUWAHI KUPATA VIGONGO VIPYA ILI KUKONGA NYOYO ZETU. NA KWA HILI WALIFANIKIWA SANA TENA SANA.
5. KWA KUFIKIRIA HALI NGUMU YA MAWASILIANO BAINA YA TANZANIA NA NCHI NYINGINE DUNIANI KULINGANISHA NA SASA HIVI, NAAMINI UTAKUBALIANA NAMI KUWA WATU HAWA (DJs) WALIFANYA KAZI KWELIKWELI HIVYO KUTHIBITISHA PASIPO SHAKA BRIGHTNESS YAO.
6. WALIIPENDA, WALIIMUDU NA WALIIHESHIMU SANA FANI YA DISCO. MARA ZOTE WALIAMINI KUWA KUTUTUMIKIA SISI WAPENZI WA DISCO ILIKUWA NI WAJIBU WAO. NA KTK KUTEKELEZA WAJIBU WAO HUO KWA HAKIKA ILIWAJENGEA HESHIMA KUBWA, NA HATA LEO TUNAWAHESHIMU NA TUNAWAPENDA SANA.
7. KAZI ZAO ZILITUUNGANISHA VIJANA NCHI NZIMA. TUKAJUANA, TUKAPENDANA NA HATA WENGINE TUKAWA KTK UCHUMBA NA HATA LEO NI WANANDOA HALALI NA FAMILIA ZENYE KUHESHIMIANA NA KUHESHIMIKA. HAYA NI YA KWELI; HATA JOSEPH KUSAGA NA KAKA YAKE NI MASHAHIDI KWA HAYA NISEMAYO!! HON. FREEMAN MBOWE & KUSAGAS PLEASE CORRECT ME IF I’M WRONG!NAJUA KUWA HII PAGE NI KWA AJILI YA SEYDOU, LAKINI NAAMINI KUWA HUWEZI KUMZUNGUMZIA SEYDOU PEKE YAKE BILA KUWATAMBUA NA KUWATAJA DJs WENZAKE WA ZAMA HIZO.MWISHO, NAOMBA KUTOA USHAURI UFUATAO:
a) LIANDALIWE TAMASHA LA WAZI LA DISCO LA ZAMANI (KIPINDI CHA EARLY & MID 1980s) LIKIONGOZWA NA DJs WA ZAMANI – SEYDOU NA WENZAKE WALIO HAI (SIWEZI KUWATAJA KWASABABU SIFAHAMU NI KINA NANI WAPO HAI). ILA NAOMBA WAJI”ORGANIZE” NA KUFANYA KITU KAMA HICHO. HII, PAMOJA NA KUTOA BURUDANI, ITATOA FURSA KWA WADOGO ZETU KUWEZA KUJUA HALI YA DISCO ILIVYOKUWA JUU ENZI HIZO, HIVYO KUJIFUNZA NA KUWAJENGA ZAIDI.
KTK TAMASHA HILO, VIPIGWE VIGONGO VYA ENZI HIZO TUPU, KAMA VILE CONGA BEATS, RYTHM IS GONNA GET U, RYTHM OF THE NIGHT, ETC,ETC…b) WADOGO ZANGU (DJs WA SASA) JIFUNZENI KWA KAKA ZENU HAWA ILI MREJESHE HADHI YA DISCO NCHINI. NI HAZINA KUU KTK MEDANI.

Comment by kitwana
Yaani!!! hapo juu naweza kuwaita kina kaka,nakumbuka wakati ule tukienda disco Toto YMCA huyu bro Muhidini michuzi ndio alikuwa mpiga picha wetu maarufu hata baadhi ya picha alizowahi kunipiga ninazo nyumbani,alikuwa very professioner(talented) tokea kipindi kile,bila kupigwa picha na yeye hujafurahi ila kuna Dj mmoja ambaye amesahaulika ni MR A.huyu jamaa ndio alikuwa best dancer in tanzania baadae akapiga disco na John Bule pamoja na Kim pale Rugwe Ocean Hotel..MR A baadae akapiga Continental Hotel,Mr A katika anga za kucheza mziki kwa kipindi kile hakuna mfano wake mpaka sasa,yaani alikuwa fit, akicheza ilikuwa huwezi tofautisha na John Travolta huwezi…. nadhani video zake baadhi ya watu kama Said Hilaly (Bon City)ambaye ni kaka yake marehemu Nassor Boncity wanaweza kuwa nazo basi BC ijaribu kutuwekea katika window media video tuone mambo kidogo
.Comment by kitwana
!!! hapo juu naweza kuwaita kina kaka,nakumbuka wakati ule tukienda disco Toto YMCA huyu bro Muhidini michuzi ndio alikuwa mpiga picha wetu maarufu hata baadhi ya picha alizowahi kunipiga ninazo nyumbani,alikuwa very professioner(talented) tokea kipindi kile,bila kupigwa picha na yeye hujafurahi ila kuna Dj mmoja ambaye amesahaulika ni MR A.huyu jamaa ndio alikuwa best dancer in tanzania baadae akapiga disco na John Bule pamoja na Kim pale Rugwe Ocean Hotel..MR A baadae akapiga Continental Hotel,Mr A katika anga za kucheza mziki kwa kipindi kile hakuna mfano wake mpaka sasa,yaani alikuwa fit, akicheza ilikuwa huwezi tofautisha na John Travolta huwezi…. nadhani video zake baadhi ya watu kama Said Hilaly (Bon City)ambaye ni kaka yake marehemu Nassor Boncity wanaweza kuwa nazo basi BC ijaribu kuzifuatilia kama zitapatikana basi ziwekwe through window media video ili wadogo zetu waone jinsi gani disco lilivyochezwa wakati huo
.Comment by LRM
E bwana huyu mkongwe Seydou; ni hatari katika hii fani. Yuko kama unavyomuona katika hii picha na kwa sasa anafanya vitu vyake hapo: Madrid Pub; Tegeta.Siku ambayo hapigi muziki; Pub hainogi, na mimi ni moja wa wadau wakubwa katika pub hiyo bila yeye J5, Alhamisi, Ijumaa, Jumamosi na J2… wiki inakuwa haijaisha. Kwa kawaida huwa naanzia hapo, akimaliza ungwe basi ndio nashuka hizo sehemu zingine mnazozijua hapo DAR.Simu yake kwa sasa: +255784347414 mpigie umpe pongezi zake.
Shukran
Comment by BABU
Dj Edie Sally disco lake liliitwa EMTHREE DISCO ndio disco la kwanza kutumia CONSO, nawakumbuka kina Rehema Bint Baka, Mwajuma Sarahani, bila ya kusahau Ray Abdu mzee sunguma paka mie mamamia na majina yake kibao akipanda juu pale mbowe kuyataja anayeyakumbuka atuelezee, MWISHO kabisa ikaja PINK COCNUT dj Fuso Brown na Mau Makata na DJ CHULU .Nafurahi kumuona DJ wetu wa enzi,Dj seydou alikuwa akinitoa kwenye kiti kwa kila anachokipiga espicial wimbo mmoja uitwao You Dont Know-Serious Intention,asante sana issa michuzi,
AMARIDO JR.
AMARIDO JR.
Comment by Dennis law
Nimefurahi sana kuwasikia vijana wa zamani katika disco la bongo.Usisahau kuwa Nguli Saydou alishapiga disco pale Mji wa Moshi ,katika club pacha ya mbowe, enzi hizo ilikuwa inaitwa ‘Kilimanjaro Hotel” kama sikosei, ipo mkabala na Libert hotel kwa wale wonaoufahamu mji wa moshi watapaelewa.Alikuja na Dj KKAALLII(kalikali)lakini kalikali apashindwa moshi akarudi Bongo mzee mzima akaendelea peke yake makamuzi yake. Nampa hongera sana
.Comment by Nice guy
Ebwana mimi nakubali kabisa hawa madj sayduu na jerry kotto hakuna wa kuwafikia.alafu dar hakuna watu siku hisi wamebaki mapedeshee washamba. yaani mimi huwa nalia wakati mwingine tulivyokuwa tunakula maisha tukingia disco wasafili kibao sio siku hizi wabolibo kibao hata majuu wabolibo kibao wewe acha tu.mimi huwa nasikitika mno yaani madisco hayana hazi tena washamba wamekuwa wengi mno dar,hata majuu wamejaa wao tu.
Comment by J4
Ni kweli mzee madj wa zamani walikuwa na vipaji na walikuwa wanaeheshimu kazi ya udj sio madj wa siku hizi hawajue ndio maana kila mtu dj.Alafu kuhusu watu wa zamani wapo,ila wapepoa hawatoki sana kila sehemu wamejaa hao mapedeshee.na unajua tena watu wa zamani waliokuwa wanacheza madisco ndio waliokuwa watoto wa dar.ndio maana wanaombo wafungue sehemu ambayo watakuwa wanapiga debe za zamani na madj wawe wale wa zamani,utawaona watu wa zamani watoto wa dar.siku hizi dar kumeingiliwa na mapedeshee washamba.
Comment by kindie on January 2nd, 2010 9:32 pm[Image]ok,let me take you back,just follow me.mambo yote yalianza bilibi,i was too you to go there,but my bother used to there.mara ka kwanza naenda disco ilikuwa africana,dj alikuwa clements,at the same time msasani ilikuwa inafunguliwa,na dj alikuwa idi sally na choge sly.jumapili tulikuwa tunapiga rungwe,kule dj alikuwa john bure,i dont remember the second dj.i want to say roma pop juice.anyway mbowe kama kawaida,seydour & gerald.likafunguliwa disco jingine silver sand,chogi na john peter walikuwa madj.at the same time mashindano ya disco yalikuwa yanaanza,ahmed,bob rich,titto(who end up to be a dj(tnt jackson).mid 80′s madj walikuwa wanatamba walikuwa,seydor,gerald,ebonite,joe jonson,young ray(stuwart)tnt jackson(titto)kalikali,nigger jay,ibra wa jet set. but kulikuwa na mdjs ambao walikuwa hawana majina makubwa lakini walikuwa wakali kishenzi. mdjs wa blu sky,nimewasau majina yao.
jesse(babyface) wa clouds,beni wa makumbusho,cool joe wa studi 45.sijamaliza,ngoja nienda nikakumbuke zaidi.Msimsahau marehemu Joseph Kuo ,kwa wale watu wa mambo fulani.
Comment by ADAM R.S.FUNDIKIRA on March 27th, 2010 6:37 am[Image]Kwa kweli wengi mna kumbukumbu nzuri ni za kweli sina umuhimu wa kurudia,kwani nami nimeshiriki (kwa kucheza mashindano ya mitindo mbalimbalikama robot,breakdance,chacha n.k)madisco yote hayo na hadi hivi sasa ni mshabiki mzuri wa fani hiyo,namshukuru M.Mungu nipo salama.tena kwa kuwakumbusha dj jerry kotto alipenda pia kucheza na rollerskirt zilivyoingia,na mabaunsa kina wandiba na wenzake walikuwa wanapiga watu ovyo,lakini siku moja wakakosea mtu wa kumpiga wakampiga mjeshi wa kenya,aliwapa kibano wote hadi mapolisi waliingilia kati!Comment by Joey Galinoma on June 6th, 2010 3:19 pm[Image]Kama wenzangu wote wa miaka hiyo walivyoelezea historia yote ya wakati huo sina la kuongeza zaidi ya kuelezea kuguswa kwangu moyoni. Charle Mbowe ni rafiki yangu sana tangia 1978 tukiwa jeshini. Baada ya jeshi tulirudi mjini na hatimaye Mbowe disco. Wote hawa Spear, Seydo, Kotto wananikumbusha mbali sana!Kama mkazi wa Upanga West Biribi tuliianzisha sisi tena kule Muhimbili Nursing School, baadae ikawa Salende Bridge Club na baadaye kupanda chatihatimaye kuwa Clouds (Justin Kusaga ndio alibuni jina CLOUDS) na mimi nilikuwa nawachorea picha za matangazo gazetini(Daily News tuu). Baada ya hapo wengi wetu tuliondoka nchini kutafuta kisomo.
Ninamengi ya kusema ila muda mfupi ila tusimsahau DJ Paul Seme (alipenda sana Brass cOnstruction), mnakumbuka BT Express? Ohio Players? LTD Exchange? Earth Wind and Fire? Commodores? Sister Sledge? Le Chic?Joey Galinoma

Comment by Zomba on July 12th, 2010 11:43 pm[Image]Duh, jamani mmemsahau DJ Yunayat, ambae enzi hizo karudi ubaharia na rekodi zake mpya, huyu ni kaka yake DJ Meb, kule Africana na Bahari, yeye ndie aliemrithisha DJ Meb na ndie alikuwa DJ akishirikiana na Clemens/t. Mwengine ambae alikuwa na DJ Seydou pale Mbowe (part time) ni ka handsome ka kiarabu (enzi hizo) DJ Femmy (Fahmi).
[Image]nakumbuka wakati wanafunguwa disco toto mbowe yali fanyika mashindano ya break dans walio shinda ni omali break dans na dulla kimchuji na abdaladigadiga hao ndio washindi wa break dans bongo kwa enzi hizo walikuwa na umbli wa kama ivi 13.14 namkubuka dj.seydou alimuowa msichana kutoka gerezani ni dada yake zuhura badae walihamamia magomeni. long time natena kama kawaida yetu tulikuwa hatu pandi tax wala bus kama una tokea kariyako au upanga jangwani gerezani nikwamguu tu halafu iki fikaa mitaaa ya sasa sita usiku uki kutana na mapolis kazi ni kukimbia
KWA HISANI YA BONGO CELEBRITY

No comments:
Post a Comment