Warembo wanaoshiriki katika shindano la Vodacom Miss Tanzania jana wamenusurika kifo baada ya boti waliyokuwa wakisafiria kupinduka katika bahari ya hindi na kusababisha tafrani kubwa jijini Dar es salaam hapo jana.
Mkuu wa itifaki Kamati ya Miss Tanzania Bwana Albert Makoye amethibitisha kutokea kwa tukio hilo ,amesema ilikuwa umbali wa kama mita 150 kutoka nchi kavu wakati boti hiyo ilipopinduka, hata hivyo warembo walikuwa wamevaa Life jacket wakati wa tukio hilo na waliokolewa na kutoka Salama kabisa na hakuna hata moja aliyejeruhiwa wala kupelekwa Hospitali kwa matibabu. Inadaiwa warembo hao walikuwa wakienda katika kisiwa cha Mbudya katika kutekeleza programu za kawaida za kambi ya Vodacom Miss Tanzania, lakini kutokana na tukio hilo safari hiyo iliahirisahwa na kuwaruhusu warembo kurejea kwenye kambi ya0 iliyopo kwenye Hoteli ya Giraffe Ocean View Kunduchi jijini Dar es salaam. Shindano la Vodacom Miss Tanzania linatarajiwa kufanyika Oktoba 11 kwenye ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam huku mshindi wa shindano hilo akiibuka na zawadi ya gari aina ya Hyundai i10 na fedha taslimu shilingi milioni 10.
No comments:
Post a Comment