RAIS Mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, jana amejikuta katika wakati mgumu baada ya mtu asiyejulikana kuvamia jukwaa alipokuwa na kumzaba kibao shavuni.Tukio hilo ambalo halikutarajiwa lilitokea jana majira ya saa 12:20 hivi wakati rais huyo mstaafu alipokuwa akihutubia Baraza la Maulid kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW) lililohudhuriwa na Waislam wengi katika Ukumbi wa Diamond Jubilee.Alhaji Mwinyi alikuwa akizungumzia masuala ya afya na namna ya kujikinga na ugonjwa wa Ukimwi ndipo alipojitokeza mmoja wa waumini aliyekuwa amevalia shati na suruali na kupanda jukwaani kisha kujifanya kama vile anamsalimia Mufti Sheikh Mkuu Issa bin Simba.Kwa kuwa imezoeleka shughuli za kidini kama ile huwa ni za amani basi waliokuwa karibu na mtu huyo wala hawakuwa na shaka naye ndipo mtu huyo akarudisha kibao kwa nguvu na kumzaba Mzee Mwinyi.Mtu huyo alijifanya kama anataka kumsalimia Kaimu Mufti, Sheikh Suleyman Gorogosi.Kwa kuwa imezoeleka katika shughuli za kidini kutawaliwa na amani, watu waliokuwa karibu na mtu huyo hawakuwa na shaka naye ndipo mtu huyo akarudisha mkono ghafla na kumzaba kibao Mzee Mwinyi."Sisi tulishangaa kuona yule jamaa akipanda jukwaani na kujifanya kama anasalimiana na Mufti. Lakini cha kushangaza tukaona akageuka na kumzaba kibao Mzee Mwinyi... sisi tulishikwa butwaa," alisema Hussein Kauli mmoja ya watu waliohudhuria sherehe hizo.
No comments:
Post a Comment