.

.

.

.

Sunday, March 29, 2009

WANAWAKE WALIOKUFA KWENYE AJALI YA KIBAJAJI



Hawa ndio wanawake waliogongwa na Andrew Chenge na kufa hapo Ijumaa iliyopita. Beatrice (juu) na Vicky ( chini)
SAKATA la ajali ya gari la Andrew Chenge ambalo limesababisha vifo vya wanawake wawili, limeingia katika sura mpya baada ya ndugu wa wasichana hao kudai kuwa Chenge alikuwa akimfahamu mmoja wa marehemu.Chenge ambaye alikuwa Waziri na Mwanasheria mkuu wa zamani wa serikali, aliingia matatani baada ya gari alilokuwa akiendesha kugonga "bajaji" usiku wa kuamkia juzi na kuua wanawake wawili ambao ni Beatrice Costantine ambaye ni mfanyabiashara wa Mwanza na mmiliki wa saluni ya kike na Vicky George Makanya.Wakizungumza kwa nyakati tofauti jijini Mwanza baadhi ya ndugu waliohojiwa na Mwananchi Jumapili akiwamo mama mzazi wa Vicky, walisema wanafahamu Chenge kuwa alikuwa akimjua ndugu yao Vicky.

No comments:

Post a Comment