.

.

.

.

Tuesday, June 23, 2009

INJINIA AKUTWA AMEKUFA

MFANYAKAZI wa Casino ya Grand Harbour View, Piet Bruwer, amekutwa amefariki dunia huku akiwa kifua wazi na pembeni kukiwa na chupa ya pombe aina ya Value, glasi ya maji na dawa za kulevya. Mwili wa Bruwer (35) raia wa Afrika Kusini, uligundulika baada ya mfanyakazi mwenzake, Emmanuel Malik (29), aliyempitia kwa ajili ya kumpeleka kazini. Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba, mbali ya kukuta vitu hivyo pia Polisi walikuta kucha nane za bandia zinazodaiwa kutumika kupimia dawa za kulevya. Alisema kuwa wakati Malik alipompitia Bruwer ambaye ni injinia wa Casino hiyo, alimkuta akiwa amelala kifudifudi na kuamua kutoa taarifa. "Mwili wa marehemu ulikutwa umelala kifudifudi, pembeni kwenye stuli kulikuwa na pombe ya Value ikiwa imebaki robo, soda na maji kwenye glasi. Pia kulikuwa na kiberiti na sigara," alisema Kamanda Kova. Hata hivyo, Kamanda huyo alisema uchunguzi wa awali, ikiwa ni pamoja na kumhoji mke wa marehemu aitwaye Linde, umebaini kuwa alikuwa akitumia dawa za kulevya aina ya cocaine. Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa uchunguzi zaidi.

No comments:

Post a Comment