.

.

.

.

Wednesday, July 21, 2010

MAJIMBO YA DAR MOTO MKALI

WAGOMBEA 38 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania ubunge katika Wilaya ya Kinondoni, yenye majimbo matatu ya Ubungo, Kawe na Kinondoni, kati ya majimbo hayo Jimbo la Ubungo linatarajiwa kuwaka moto.

Mchuano mkali unatarajiwa kujitokeza kwa baadhi ya wagombe ubunge ambapo Nape Nnauye na Shamsa Mwangunga wanatarajia kuumana vikali ndani ya chama huko Ubungo, huku wakikabiliwa na upinzani mkali kutoka kwa mgombea ubunge kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mnyika.

Katika hali isiyo ya kawaida, mgombea mmoja wa ubunge anayewania Jimbo la Kinondoni, Mateo Kanela, jana aliwashangaza baadhi ya viongozi wa ofisi za CCM, wilaya ya Kinondoni, baada ya kushindwa kutaja namba ya kadi yake ya uanachama kwa madai kuwa kadi ameisahau nyumbani.

Akizungumza wakati anahojiwa na Mkurugenzi wa Uchaguzi, Godfrey Tondo, ambaye pia ni Katibu wa chama hicho wilayani hapo, Kanela alisema: “Siyakumbuki majina ya viongozi wa chama changu kwa sababu huwa sikai Dar es Salaam nakaa Kahama.

“Nikipata kazi hii ya ubunge nitaanzisha kiwanda, kwa sasa hivi nafanya biashara ya kuuza duka Magomeni. Nimeidhinishwa na Serikali, naamini kuwa sina kipingamizi katika jimbo hili, nina hakika nitapita, kwani Serikali imeniidhinisha yenyewe.”

Wagombea ubunge waliojitokeza katika
Jimbo la Ubungo ni Nape Nnauye, Dk. Apollo Kissai, Slaus Mwishemba, Kanali Gaspar Hiza, Alfred Nchimbi, Peter Msuya, Hawa Mg’humbi, Assumpta Nalitolea, Michael Lupiana, Perpetua Haule, Eliona Nkya na Shamsa Mwangunga.

Jimbo la Kawe

Faustin Kikove, Mahamoud Madenge, Nicodemus Chengula, Eric Suma, Omari Wahure, Biton Mwenisongole, Harold Maruma, Dk. Malima Bundara, Jumaa Pijei, Margaret Lema, Japhet Robi, Angela Kizigha, Dk. Petronilla Ngiloi, Elias Nasera, Zainuddin Adamjee na Kippi Warioba.

Jimbo la Kinondoni
Iddi Azzan, Mustafa Muro, Kakolwa Mbano, Shy-Rose Bhanji, Issa Omary, Godwin Kabisa, Mpoki Mwambulukutu, Bakari Maige, Mateo Kanela na Mackdonald Lunyilija.

Waliochukua fomu za Ubunge Viti Maalumu Mkoa

Zarina Madabida, Tatu Malyaga, Margaret Kimambo, Grace Mtesigwa, Amina Israel, Mossy Mbwando, Hadija Kopa, Joyce Kajula na Nuru Kaku.

Waliochukua fomu za Udiwani Viti Maalumu Wilaya ya Kinondoni tarehe 19/7/2010

Jimbo la Ubungo

Sophia Fitina, Joan Mazanda, Elukaga Minango, Angela Mfinanga, Asnath Mambo, Florence Masunga, Tatu Mnekeya, Angela Halla, Theresia Chihota, Zuena Abdallah, Grace Kabigi, Salama Lusogo, Ningile Kapange, Ester Mkandawile, Omega Masawe, Nuru Kaku na Rehema Mayunga.

Jimbo la Kawe

Hilda Rwebangira, Kulthum Sagamiko, Everly Hatibu, Bernadette Ritti, Mwanaisha Sudi, Rozina Urio, Renata Semitende, Julia Hoza, Leah Onyango, Asha Majura na Basilisa Sawere.

Jimbo la Kinondoni

Grace Mwashala, Hilda Rwezaura, Kimwana Sherally, Lilian Mchaa, Florence Ndege, Subira Kondo, Huba Hassan, Tiba Hamisi na Fatma Salim

Kwa upande wake, aliyekuwa Mbunge wa Ukonga, Dk. Makongoro Mahanga (CCM), fomu zake zimekataliwa na Katibu wa CCM, Wilaya ya Ilala, Haroun Mkalimoto, baada ya mbunge huyo kushindwa kujaza kipengele kimoja katika fomu hizo.

Fomu hizo zilikataliwa jana saa 6.17 mchana, baada ya Dk. Mahanga kuziwasilisha kwa Katibu huku zikiwa hazikujazwa katika kipengele anachotakiwa kusaini Katibu Mkuu.

Kabla ya tukio hilo lililoonekana kuwashangaza waandishi wa habari waliokuwa ofisini hapo, Dk. Mahanga aliingia ofisini hapo kwa mbwembwe huku akimtania mmoja wa wagombea wa Jimbo la Ukonga, Brighton Mzungu, aliyekuwa akichukua fomu ya kuwania jimbo hilo.

“Jamani safari hii Jimbo la Ukonga linagombewa kama mpira wa kona, haya bwana, kila la kheri,” alitania Dk. Mahanga.

Alipomaliza kusema hayo, Dk. Mahanga ambaye juzi alichukua fomu za kugombea ubunge katika Jimbo la Segerea, alikaa kwenye kiti na kuwasilisha fomu hizo kwa Katibu wa Wilaya ya Ilala.

Baada ya Katibu kuzipitia, aligundua kuwa, nafasi ya Katibu Mkuu ambayo inatakiwa kusainiwa na Katibu wa Tawi aliloko mgombea wa ubunge, ilikuwa haikujazwa.

“Kwa hiyo, nenda ukarekebishe kasoro hii maana muda bado upo,” alisema Mkalimoto na kumfanya Dk Mahanga aanze kumpigia simu Katibu wake wa tawi ili waone namna ya kusaini sehemu hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya tukio hilo, Mkalimoto alisema utaratibu wa kuwarudishia wagombea fomu zao na kuwataka wakarekebishe kasoro zilizoko ni wa kawaida kwa kuwa muda wa mwisho wa kupokea fomu haujafika.

Hadi kufikia jana mchana, wagombea 26 walikuwa wamechukua fomu kugombea ubunge katika majimbo matatu yaliyoko Wilaya ya Ilala ambayo ni Ukonga, Sgerea na Ilala.

Jimbo la Ukonga

Injinia John Kengere, Kamishna (mstaafu) Aziza Mursali, Manga Selelya, Isaya Christabela, Hamza Abdallah, Chacha Wambura, Godwin Barongo, Magesa Magesa, Sande Mnozya, Beatrice Moses, Eugen Mwaiposa, Ramesh Patel na Brighton Mzungu.

Jimbo la Ilala

Ni aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, Mussa Hassan Zungu, Jafari Juma, Juma Chikoka na Blandina Mluzya.

Jimbo la Segerea

Dk Makongoro Mahanga, Salusian Kato, Kiomon Kibamba, Glorious Luoga, Zahoro Yasuka, Paul Mahodo, John Jambele, Joseph Kessy na Venance Victor.

Waliorejesha fomu hadi kufikia jana katika
Jimbo la Ukonga ni Mwaiposa na Manga Selelya. Ilala ni Zungu na Jafari Juma, wakati Segerea ni Kessy, Luoga Kato na Dk Mahanga ambaye fomu zake zilikataliwa.

Katika hatua nyingine, Mkalimoto alisema leo jioni wagombea wote watakuwa na kikao cha pamoja kupewa masharti ya kushiriki uchaguzi huo.

Hadi kufikia jana alasiri wanachama 26 walikuwa wamechukuwa fomu za kuwania ubunge, ambapo 16 watawania Jimbo la Kigamboni, akiwamo mbunge mtetezi wa jimbo hilo, Abdulrahiman Msomi na aliyekuwa mbunge wa Jimbo la Temeke kipindi cha awamu ya tatu, John Kisabo, wakati Jimbo la Temeke waliochukuwa fomu ni 10.

Jimbo la Kigamboni

Joseph Ngwasho, Dk. Faustine Dungulile, Mariam Kambi, Issa Mohamed, Ahmed Shabani Mbegu, Briggen Haroon, Amindi Kichilingulo, Siaga Kiboko, Phares Magesa, David Shaba, Thadeus Musembi, Mwinchoum Abdulahman Msomi (mbunge wa sasa), Athuman Mbwana, Petter Gabriel, Enock Temu, John Kibaso na Pius Joseph.

Jimbo la Temeke

Ni Mbunge wa Jimbo hilo, Abasi Zuber Mtemvu, Benedicto Likwembe, Hadija Kasola, Amani Johnson, Salum Khamis Salum, Mohamed Msham, Richard Tambwe Hizza, Mohamed Nassoro Nondo, Peter Nyalali na Inayat Mohamed.

Jimbo la Muleba Kusini

Waliochukua fomu ni Mkurugenzi wa Shirika la Makazi Duniani (UN-HABBITAT) Profesa
Anna Tibaijuka, mbunge wa sasa Wilson Masilingi na Kamishina (mstaafu) wa Polisi Alfred Tibaigana.

Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki

Naye mgombe wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi, Mzeru Paulo, ameiomba Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) kuhakikisha inazuia mianya ya rushwa ambayo inaweza kujitokeza kwa wagombea mbalimbali hapa nchini.

Jumla ya wagombea 11 wamejitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya kugombea Ubunge katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki ambao ni yeye Mzeru Paul, Amani Kondo, Jamila
Mohamed, Salumu Makwaya, Semindu Pawa, Gabriel Mkwawe, Amani Mwenegoha, Lucy Nkya, Kassim Hegeka na John Nkundi.

Uwakilishi Zanzibar

Waliochukua ni Naibu kiongozi ambaye pia ni Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Ali Juma Shamhuna (Donge), Waziri wa Kilimo, Mifugo na Mazingira, Burhani Haji
Saadati (Kikwajuni), Hamza Hassani Juma (Kwamtipura), aliyekuwa ameshikilia wizara iliyopo chini ya Waziri Kiongozi, Waziri wa Mawasiliano na Uchukuzi Machano Othman Said (Chumbuni), na Waziri anayeshughulikia Fedha na Uchumi, Dk. Mwinyihaji
Makame (Dimani).

Mawaziri wengine waliojitokeza ni pamoja na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Vikosi vya SMZ, Suleiman Othman Nyanga (Jang’ombe), Waziri wa Maji, Ujenzi, Nishati na
Ardhi, Mansoor Yussuf Himid, Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Sultan Mohamed Mugheir (Mji Mkongwe) na Waziri Kiongozi Shamsi Vuai Nahodha (Mwanakwerekwe).

Makada wengine waliojitokeza kuchukua fomu za uwakilishi ni pamoja na Ali Denge Makame (Amani), Kamal Basha Pandu, (Rahaleo), Ibrahim Ali, Abdullatifu Jusa Sadiq (Amani), Sharrif Shashi (Chumbuni) Perera Ame Silima (chumbuni) na Simaio Mohamed Said (Mji Mkogwe).

Wengine waliojitokeza kuchukua fomu hizo za Uwakilishi ni Asma Ali Mussa (Kwamtipura), Nassor Salum Ali, Enzi Talibu, Zaharani (Rahaleo), Ali Salum Haji (Kwahani), Mussa Khamis
Silima (Uzini), Sharifa Abeid Salum (Koani), Bimkubwa Khamis Janja na Mshihiri Ali Faki (Fuoni), Issa Haji Issa (Chwaka) na Omar Gulam (Dole).

Ubunge Zanzibar

Wanachama walijitokeza kuchukua fomu za kuwania nafasi ya Ubunge ni pamoja na Waziri Ulinzi na Usalama Dk. Hussen Mwinyi (Kwahani), Ameir Haji (Magomeni), Kanal Fara (Rahaleo), Mussa Hassan Mussa (Amani), Parmuki Hogan Sing (Kikwajuni) na Ali Abeid Khamis (Kwamtipura).

Wengine ni Issa Khamis Issa (Mpendae), Ali Hassan Omar (Jang’ombe), Salehe Ramadhani Ferouzi (Kikwajuni), Omari Said Ameir (Mpendae), Dk. Ahmada Hamad Khatib (Koan), Mohamed Muhsin Simba (Fuoni), Sylvester Massele Mabumba (Dole), Alsha Si Said (Kwamtipura), Rahma Rashid (Magomeni) na Abdalla Mabodi (Rahaleo),

Viti Maalum Mkoa wa Dodoma

Waliochukua fomu hizo ni Mbunge wa sasa wa Viti Maalum,
Felister Bura, Mary Chihoma, Catherine Ndahani, Christina
Cylil, Sara Mwaga, Maram Mfaki, Salome Kiwaya, Stella Fweda na
Mary Mbogo.

Wengine ni Dk. Salma Chande, Catherine Mgogoro, Juliana
Manyerere, Dokilia Bashemeko, Winfrida Andrew, Edna Ndejembi
na Rachel Temba.

Jimbo la Mpwapwa

Mbunge anayetetea jimbo, George Lubeleje, Gerigori Teu, Yona Mtema, David Lusa, Dk. Mombo Kamwaya na Rehema Harahara.

Jimbo la Kibakwe

Mbunge anayetetea jimbo George Simbachawene, Paulo Geyanga, Dk. Federick Kasanga, Omari Tuwakali, Lawrian Ndimbo, Solomon Mgiliule na Akrey Muyanga.

Jimbo la Dodoma Mjini

Hadi jana mchana walikuwa wameongezeka wanachama wawili, akiwemo mbunge wa sasa Ephraimu Madeje na Reginald Mavere. Wanachama hao wamefanya idadi ya waliouchukua fomu katika jimbo hilo kufikia 14.

Jimbo la Kibaha Mjini

Dk. Zainabu Gama (mbunge anayemaliza muda), Silvester Koka, Charles Makunga, Hamis Masasa, Dk. Rose Mkonyi, Profesa Samweli Wangwe, Eusibius Mvuoni na Kibindu Yohane.

Nafasi za madiwani Viti Maalum kupitia (UWT) mpaka sasa fomu zimechuliwa na wagombea 15 akiwemo Mwandishi wa Habari wa Uhuru na Mzalendo, Selina Wilson. Udiwani kupitia kata wamefikia 40.

Katibu wa CCM Mkoa wa
Pwani, Sauda Mpambalioto, alisema kuwa mpaka sasa kuna jumla wagombea wa nafasi ya ubunge 47 ikiwemo Rufiji (saba), Mafia (watano), Kibiti (saba), Kisarawe (wawili), Chalinze (watano), Mkuranga (watatu) na Bagmoyo (watatu) huku kundi la umoja wa Vijana waliojitokeza ni wanne.

Udiwani Tanga

Mkulima maarufu wa Chai wa Kijiji cha Nkelei kilichopo Kata ya Tamota, wilayani hapa, Bakari Banda (70) amechukuwa fomu ya kugombea Udiwani katika Kata hiyo kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.

Mhifadhi Samaki aina ya Silikanti (Kishapu) na Katibu wa Umati
Wilaya ya Tanga, Mwanaisha Shabani, ametangaza nia ya kuwania
udiwani viti maalum tarafa ya Chumbageni Tanga.

Viti Maalum UVCCM

Ofisa Habari wa Tume ya Kudhibiti Ukimiwi Tanzania (TACAIDS), Gloria Mzirai, ametangaza nia ya kugombea ubunge wa Viti Maalumu kupitia Jumuiya ya Umoja wa Vijana, UVCCM Mkoa wa Morogoro. Amechukua fomu jana.

Jimbo la Karatu

Dk. Wilbald Lorry

Huko Singida

Aliyekuwa mkuu wa wilaya katika wilaya mbalimbali hapa nchini, Hawa Ngulume, amekanusha vikali uvumi ulioenea kuwa ametumwa na Waziri Mkuu (mstaafu), John Malecela kugombea ubunge katika Jimbo la Singida Mjini.

Kutoka Kigoma

Aliyekuwa Meya wa Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa tiketi ya CHADEMA, Kitita Magonjwa, amekihama chama hicho na kuchukua fomu ya kuwania udiwani wa Kata ya Rusimbi kwa tiketi CCM jimbo la Kigoma Mjini.

Katika hatua nyingine, jumla ya wanachama watatu wa CCM wamechukua fomu kuomba kuteuliwa kugombea ubunge kupitia chama hicho katika
Jimbo la Kigoma Mjini, akiwemo Mbunge wa sasa jimbo hilo, Peter Serukamba. Wengine waliochukua fomu juzi ni pamoja na Mwenyekiti wa CCM Wilaya Kigoma Mjini, Nashon Bidyanguze na Mhasibu Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Adam Mgoi.

Jimbo la Muhambwe

Felix Kijiko, Jamal Tamim, Emanuel Bwegenyeza, Brighton Gwamagobe, Richard Kigaraba, Barakabise Mbogoyo, Dk.Chrispine Shami, aliyewahi kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira), Arcado Ntagazwa, Regina Kayabo na Salome Choma.

Jimbo la Buyungu

Hadi tunakwenda mitamboni Naibu Waziri wa Kilimo na Umwagiliaji, Christopher Chiza pekee ndiye aliyechukua fomu katika jimbo hilo.

Jimbo la Mvomero

Marcus Mgweno, Amos Makalla na Sadiq Murad

Moshi Mjini

Justin Salakana

Jimbo la Arumeru Magharibi

Loy Thomas Sabaya na Robinson Meitinyiku.

Jimbo la Arumeru Mashariki

William Sarakikya na Anthony Musani.

Jimbo la Arusha

Mbali na Dk. Batild Burian aliyechukua juzi, jana ameongezeka mbunge wa Jimbo hilo, Felix Mrema.

Jimbo la Ngorongoro

Mathewtak Ole Timan, Saning' Ole Telele, Fidelis Ole Kashay, Godfrey Laliya, Williamu Ole Nasha, Pius Sanai,Peter Metele, Vincent Mbirika, Patrick Gwedig.

Jimbo la Bunda

Tembe Nyaburi, Emmanuel John Phales, Ginche Kisase, Yeremia Kulwa Maganja, Samwel Mgaya Tumaini,
Jeremiah John Wambura na Stephen Wassira.

Jimbo la Mwibara
Kangi Alphaxad Lugola, Bartazar Ryamongo, Mtangazaji wa Channel Ten, Cyprian Msiba, Chrphord Kajana, Emmalieza Chilemeji, Bitulo Paschal Kazeli na mwanamke pekee ambaye ni Mwalimu wa Shule ya Msingi, Bahati Misana.

Jimbo la Simanjiro

James ole Millya, Christopher ole Sendeka (mbunge anayemaliza muda) na Lewnganasa Soipey.

Udiwani Dar es Salaam

Mbunge wa Bunge la Afrika ya Mashariki, Dk. Didas John Massaburi, ametangaza nia ya kugombea udiwani kata ya Kivukoni kwa tiketi ya CCM.

Mchakato wa kuchukua fomu hizo na kurudisha unaendelea mpaka leo kabla ya saa 10:00 jioni ambapo kampeni zitaanza kupigwa Julai 22 hadi 28 ndani ya chama na kura za maoni kwa
wagombe zitapigwa Agosti Mosi katika matawi yote ya CCM.


Habari hizi zimeandikwa na Maregesi Paul, Mussa Katuga, Herrieth Benny, Audax Mutiganzi, Rose Chapewa, Grace Shitundu, Rachel Mrisho, Debora Sanja, Gustaphu Haule, Sussan Uhinga, Rose Chapewa, Prisca Libaga, Nathaniel Limu, Iddi Risasi, Eliya Mbonea, Ahmed Makongo, na Mwanaidi Abasi wa DSJ.

No comments:

Post a Comment