.

.

.

.

Friday, July 09, 2010

TAMASHA LA ZIFF LAANZA LEO

Tamasha la 13 la filamu limepangwa kuanza leo tarehe 10 Julai 2010 katika uwanja wa Ngome Kongwe ulioko mji mkongwe mjini Zanzibar. Tamasha hili lenye msisimko linatazamiwa kuhudhuriwa na zaidi ya wageni 200,000 likishirikisha zaidi ya nchi 43, hivyo kuwa tamasha kubwa lenye msisimko wa aina yake. WAGENI WATAKO UPAMBA UFUNGUZI WA TAMASHA HILI NI: STEVEN KANUMBA EVONNY CHERRY YAKUB (MONA LISA) VICENT KIGOSI Zaidi ya Filamu100 zitakazoonyeshwa mwaka huu katika tamasha linalotazamiwa kukoma tarehe 18 July 2010. Filamu ya ufunguzi Filamu itakayo fungua pazia la tamasha hilo Mwaka huu ni Youssou N’Dour: I Bring What I Love Iliyoongozwa na: Elizabeth Chai Vasarhelyi Filamu itaonyeshwa 10th July, Old Fort, Kuanzia saa 3:00 usiku baada ya ufunguzi rasmi. Filamu hiyo ya ufunguzi, ni filamu yenye tunzo nyingi. Filamu hiyo inayo muhusu mwanamziki maarufu Youssou N’Dour, I Bring What I love (Naleta nachokipenda), inayozungumzia imani na amani. (addresses the themes of religious tolerance, harmony and peace.) ina lengo la kuhamasisha, inaonysha safari ya kimziki, yenye ushuhuda wa nguvu ya sauti ya mtu mmoja kuhamasisha mamilioni. “I Bring What I Love” imedhaminiwa na SIGNIS. FILAMU NYINGINE KUBWA ZITAKAZO ONYESHWA MWAKA HUU NI: Nipe Jibu: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza . Filamu ya kwanza ya kuchanganya Muziki na kuigiza Muongozaji Nadine Louise Fasera. Nipe Jibu ni filamu nzuri ya Kiswahili yenye kuchanganya muziki iliyotengenezwa kwa mtazamo wa kisasa na kitamaduni kwa simulizi iliyochangamka juu ya binti yatima anayeishi kwenye maisha ya ndoto. My Policy: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza. Kijana mdogo mfanya biashara anapigwa risasi kwenye siku yake ya kuzaliwa akiwa anarejea nyumbani kwake akitokea kwenye tafrija yake kusherehekea siku hii muhimu akiwa na mchumba wake, Victoria. Wiki chache baadae, Yule aliyempiga risasi amjia na kumchoma kisu hadi kufa. Kwa kupagawa na pigo hili, Victoria aamua kuhama Montreal na kuanza maisha mapya, Lakini muuaji amjia nay eye pia.... Muongozaji: Phad Mutumba Motherland: African premiere - Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Afrika Ana’s Playground: - kuonyeshwa kwa mara ya kwanza Afrika Lamu’s Maulid: Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza kidunia: world premiere Inside Life: : Kuonyeshwa kwa mara ya kwanza kidunia: world premiere Pumzi: East Africa’s first ever science fiction film A sneak preview of Twiga Stars

No comments:

Post a Comment