TA-UK ikishirikiana na TAWA waliandaa semina ya akina mama iliyofanyika:
Nyumbani kwa Balozi wa Tanzania Uingereza, Jumamosi, 21 Mei 2011.
Mgeni Rasmi alikuwa Mama Pinda Mke wa Waziri Mkuu, Tanzania.
Mada ya Semina ilikuwa “Wanawake kama Wakala wa Mabadiliko” na mkazo zaidi kwenye - Mwamsho kuhusu Waafrika waishio Uingereza wanaoishi au walio adhirika na UKIMWI” “HIV and AIDS Awareness Seminar: for African communities affected by HIV and AIDS in the United Kingdom.
Kusudu na Mategemeo ya Semina
Makusudi ya semina yalikuwa: kuwakumbusha/mwamko kuhusu Ukimwi, kuzungumzia maswala ya stigma, ubaguzi, watu kutokukubali (denial), kukubali na kuweza kujitokeza. Inategemewa hatimaye kuweza kuwa na vikundi vya kusaidiana baini ya Waafrika hususani Watanzania waishio Uingereza.
Objectives:
The seminar aims to: Raise HIV and AIDS awareness, discuss issues of stigma, discrimination, denial, acceptance and disclosure of HIV status, training needs, develop support and social network groups among the African communities living in the UK.
Semina ilikuwa katika sehemu mbili:
Sehemu ya kwanza ilikuwa kwa Kiingereza na wazungumzaji wakuu walitoa changamoto kuhusu:
- Akina Mama kama Wakili wa Mabaliko: Akina mama walikumbushwa kwamba afya ni jambo la mhimu kwa kila mtu. Maendeleo au mabadiliko yeyote yale yana leletwa na watu wenye afya nzuri. Kwa hiyo ni vema mama kujali afya yako ikiwa ni pamoja na kuungalia mwili wako kama vile kwenda hospital na kupimwa kwa magonjwa mbali mbali, kubadilisha mwenendo wako. Mama akiweza kujali na kubadilisha mwenendo wake yeye atakua mfano na kuwa taa kwa watu waliokaribu naye – familia pamoja na jamii kwa ujumla.
- Kuishi kwa mategemeo –“Living positively with HIV” – Hii ilikuwa changamoto sana kwa wajumbe, watu walielezwa kuwa ukiwa na UKIMWI siyo mwisho wa maisha. Mtoa mada kwanza aliuza swali hivi nani anaweza kumtumbua mtu aliyeaidhirika kwa Ukimwi yuko vipi au unaweza kumtambua vipi? Jibu hakuna mtu ambaye anaweza kutambua labda mtu akiwa mahututi kitandani. Jibu ni kwamba mtu ye yote Yule anaweza kuwa ana Ukimwi lakini hakuna anayejua. Mtoa mada alisema kuwa yeye ameadhirika tangu akiwa mdogo lakini sasa hivi ameolewa na ana watoto. Amesoma na anafanya PhD na anaishi maisha ya furaha kama watu wote. Fundisho jamani ukiwa na UKIMWI siyo mwisho wa maisha. Lakini unaweza kufanikiwa kuishi haya maisha kama utapimwa na ikajulikana mapema kuwa umeadhirika ili ukapata msaada.
Sehemu ya pili:
Mama Balozi alimkaribisha Mama Waziri Mkuu. Mama Pinda alisema kuwa amefurahishwa sana na kitendo cha akina mama kukutana na kuwa na semina nzuri sana iliyoelimisha, kufumbua watu kuelewa mambo zaidi. Vile vile alimshukuru Mama Balozi kwa kuweza kuwakaribisha wanawake nyumbani kwake.
Aliahidi kuwa endapo atapata nafasi ya kuja Uingereza tena atajihidi kukutana na akina mama. Semina za uamusho kwa
Vile vile wakati huu wajumbe walipata nafasi ya kupata changamoto nyingine toka kwa mtu ambaye vile vile amejitokeza kuwa yeye ameadhiriwa na Ukimwi, alisema siyo jambo rahisi kujitokeza kwani kuna mambo mengi sana kama vile– dharau, kukataliwa na ndugu, kuogopa kuondolewa etc. Alisema ameweza kufika hapa kwa sababu alitambua mapema kuwa ameadhiriwa. Kwa hiyo changomoto ilikuwa jamani tujitahidi kupimwa mara kwa mara.
Kusudu na Mategemeo ya Semina
Makusudu ya semina yalikuwa: kuwakumbusha/mwamko kuhusu Ukumwi, na kuzungumzia maswala ya stigma, ubaguzi, watu kutokukubali (denial), kukubali na kuweza kujitokeza na na hatimaye kuweza kuwa na vikundi vya kusaidiana baini ya Waafrika hususani Watanzania waishio Uingereza.
TA-UK itaendelea kuandaaa hizi semina kwa kushirikiano na vikundi mbali mbali vya Kitanzania, Africa Mashariki vilivyop nchini Uingereza. Hizi Semina zinadhaminiwa na msaada kutoka Commonwealth Secretariat.
No comments:
Post a Comment