.

.

.

.

Saturday, May 12, 2012

QUEEN SPEAR YA AUNT FIFI IKO NJIANI


MWIGIZAJI na mtayarishaji wa filamu nchini Tumaini Bigilimana ‘Aunt Fifi, anatarajia kuachia filamu yake mpya inayokwenda kwa jina la Queen Spear, imefahamika. Akizungumza jijini Dar es Salaam hivi karibuni, Aunt Fifi alisema kuwa tayari kazi ya uhariri imeshakamilika hivyo ameanza mchakato wa kuiingiza sokoni. Alisema anaamini mashabiki wa filamu wataipenda kazi hiyo iliyozingatia mila na desturi za Kitanzania kutokana na kukamilika kila idara kuanzia hadithi, upigaji picha, hadi washiriki waliohusika. Fifi ambaye ni mahiri katika utunzi wa filamu za kibongo huku akijaaliwa pia kuzitendea haki kazi zake alisema kuwa mwaka huu amepania kutayarisha filamu bomba zaidi ili kuweza kuwapa burudani zaidi mashabiki wa bongo Muvi. Aidha, Fifi ambaye ndiye mtunzi wa filamu ya Senior bachelor filamu iliyomletea tuzo kadhaa msanii Jacob Stephen ‘JB’ kupitia filamu hiyo ambayo, pia alipata kutayarisha filamu yake ya aliyoipa jina la Kizungumkuti na kufanya vizuri. Kama hiyo haitoshi Fifi alipata kutamba katika filamu mbalimbali zikiwemo Copy, Sound of Death, Senior Bachelor, I Deserve It, Kaburi la Mapenzi, Fake Smile, Daddy, Cross My Sin na nyinginezo.

No comments:

Post a Comment