.

.

.

.

Saturday, March 22, 2014

RAIS JK KUKUTANA NA WATANZANIA HAPA UINGEREZA JUMAPILI YA TAREHE 30 MACHI 2014

Ubalozi wa Tanzania London - Uingereza, unafuraha ya kuwatangazia Watanzania wote waishio Uingereza kuwa Mhe. Dr. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, atakutana na Watanzania siku ya Jumapili tarehe 30 Machi 2014.

Mkutano huo utafanyika katika ukumbi wa Sattavis Patidar Centre, Forty Avenue, Wembley Park, London, Middx, HA9 9BE, kuanzia saa 10 jioni (16:00).

Katika Mkutano huo, Mhe.Rais Kikwete atazungumzia maendeleo ya nchi yetu na pia kutumia fursa hiyo kusikia masuala yanayogusa maslai ya wanadiaspora. 

Mhe. Rais atakuwa nchini Uingereza kuanzia tarehe 30 Machi hadi 2 April 2014 kwa ziara ya kikazi kwa mwaliko rasmi wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Mhe. David Cameron.

Ubalozi unapenda kuchukua fursa hii kuwaomba Watanzania wa maeneo ya Uingereza na nchi jirani kujitokeza kwa wingi kumkaribisha Rais kwenye Mkutano huu adimu.


Kwa Taarifa zaidi:
Simu: 0207 569 1470
Email: balozi@tanzania-online.gov.uk

Ahsanteni sana- Ubalozi wa Tanzania – London

No comments:

Post a Comment