.

.

.

.

Monday, September 21, 2015

MSIBA ATHENS UGIRIKI NA DAR TANZANIA
Familia ya Marehemu George na Mama Rhoda Malongo wa Upanga, Dar es Salaam, wanasikitika kutangaza kifo cha binti yao mpendwa Esther Glory Malongo (pichani) kilichotokea ghafla tarehe 16/09/2015 kule Athens, Ugiriki. (1 Timothy 4: 7 Nimevipiga vita vilivyo vizuri, mwendo nimeumaliza, Imani nimeilinda.)
Esther ataagwa na jamii ya Watanzania waishio Ugiriki siku ya Kesho Jumanne tarehe 22 September 2015. Halafu anategemewa kusafirishwa kutokea Ugiriki siku ya Alhamisi, tarehe 24 September 2015. Mazishi yanatarajiwa kuwa Jumamosi ya tarehe 26 September 2015 jijini  Dar es Salaam Tanzania. 
Tunatanguliza shukrani nyingi kwa upendo na ushirikiano wenu, Mungu na awabariki sana

No comments:

Post a Comment