.

.

.

.

Wednesday, October 29, 2008

JARIBIO LA KUMUUA OBAMA

WIKI moja ikiwa imesalia kabla ya kufanyika kwa uchaguzi wa rais nchini Marekani, idara za usalama zimetangaza kuzima jaribio la kutaka kumuua mgombea wa urais kupitia chama cha Democrats, Seneta Barack Obama.
Uchaguzi wa rais wa Marekani umepangwa kufanyika Novemba 4 na upinzani mkali ni baina ya wagombea wa vyama vikuu viwili, Republican ambacho kinata kuendelea kushikilia madaraka kwa kumsimamisha John McCainn, na Democrats, ambacho kimemsimamisha Obama ambaye amekuwa mgombea wa kwanza mweusi wa kiti cha urais.
Uteuzi wa Obama umefanya watu wenye siasa kali za kibaguzi kukerwa na polisi imeeleza kuzima jaribio la kumuua seneta huyo wa jimbo la Illinois ambaye amekuwa na mvuto mkubwa kwa wananchi wa Marekani.

No comments:

Post a Comment