.

.

.

.

Wednesday, October 29, 2008

MANJI AUGUA GHAFLA

SIKU moja baada ya timu ya Yanga kuifunga Simba bao 1-0 katika mechi ya Ligi Kuu iliyopigwa Jumapili Uwanja Mkuu wa Taifa Dar es Salaam, Mfadhili Mkuu wa klabu hiyo, Yusuf Manji ameugua ghafla na kukimbizwa hospitali. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega, Manji aliugua ghafla juzi saa 3.30 asubuhi, wakati wakijiandaa kwenda ofisini kwake, lakini kabla ya kutoka alijisikia vibaya, ambapo alianguka na kukimbizwa hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam. "Alipofikishwa hospitali madaktari walimpima na kugundua amepatwa na malaria, ambayo ilipanda kichwani, lakini hata hivyo walimpatia matibabu na kumtaka apumzike," alisema Madega. Hata hivyo, Madega alisema baada ya Manji kupatiwa matibabu, jana asubuhi alitoka nyumbani na kwenda kutembea viwanja vya Gymkhana, akiwa peke yake kitu ambacho wasaidizi wake walimwahi na kumrudisha nyumbani kwake. Alisema wasaidizi wake walilazimika kumfuata kwa kuhofia hali yake kutokuwa nzuri, kwani bado alitakiwa kupumzika kutokana na mlolongo wa mawazo na uchovu aliokuwa nao. Madega alisema hali hiyo ilichangiwa zaidi na uchovu na mawazo yaliyotokana na mechi ya Yanga na Simba iliyochezwa Jumapili, lakini hata hivyo amewataka wana-Yanga kutokuwa na wasiwasi kwani hali ya mfadhili wao inaendelea vizuri.

No comments:

Post a Comment