.

.

.

.

Wednesday, October 15, 2008

RAHA 2008 TAARABU


Manywele Entertainment kwa kushirikiana na Jahazi Modern Taarab wana (Nakshi nakshi) imeandaa onyesho la Taarabu lililopewa jina la Raha 2008 linalotarajiwa kufanyika katika Hotel ya Traveltine Magomeni siku ya jumapili 19/10/2008.akizungumza kwenye ukumbi wa idara ya habari maelezo Maimartha Jesse Mratibu wa onyesho hilo amesema vikundi vingine vilivyoalikwa kwenye onyesho hilo ni East African Melody, Khadija Kopa na Hammer Q.Pia onyesho hilo ni kwa ajili ya kusaidia kikundi cha vijana kinachoitwa Welawela cha Kinondoni, onyesho hilo litaanza saa tatu usiku na kiingilio kitakuwa shilingi 5000 tu wapenzi wote wa Taarab mwakaribishwa sana siku hiyo.

No comments:

Post a Comment