.

.

.

.

Monday, May 18, 2009

MAUAJI YA KINYAMA MARA

Unyama wa aina yake umetokea jana baada ya watu wenye silaha kali za kijadi kuvamia katika ofisi moja ya Serikali, kumtwaa mtu aliyekuwamo ndani na kumchinja kabla ya kumkata sehemu zake nyeti na kutimua nazo.
Tukio hilo la kusikitisha, limetokea mishale ya saa 3:00 asubuhi huko katika Kijiji cha Nyakiswa, Kata ya Kyanyari, Wilaya ya Musoma Vijijini mkoani Mara.
Na aliyeuawa baada ya kuchomolewa ofisini na watu hao, amefahamika kwa jina la Msafiri Tangazo, mkazi wa Kijiji cha Nyakiswa.
Imedaiwa na mmoja wa mashuhuda kuwa waliofanya tukio hilo, ni baadhi ya wananchi wa Kata ya Kangetutya wilayani Bunda, ambao walifika kwenye ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Nyakiswa wakiwa na silaha na kumchomoa marehemu kabla ya kumuua kwa kumchinja.
Inadaiwa kuwa walitekeleza azma hiyo ya kinyama baada ya kumtuhumu marehemu kuwa anahusika na wizi wa ng'ombe wa mwananchi mwenzao mmoja.
Awali, marehemu alikuwa ameshikiliwa ndani ya ofisi hiyo kwa tuhuma za kushirikiana na mwizi wa ng'ombe huyo aliyesababisha kizaazaa.
Baadhi ya mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa kuwa uzembe wa Polisi katika kushughulikia taarifa za kutaka kutokea kwa mauaji hayo umesababaisha kifo cha mtuhumiwa Tangazo.
Wakadai kuwa hapo kabla, Polisi wa kituo kidogo cha Kiabakari walijulishwa juu ya hali iliyokuwapo, lakini askari wakadaiwa kuhofia kwenda eneo la tukio kwa wakati.

No comments:

Post a Comment