.

.

.

.

Tuesday, July 14, 2009

LIYUMBA NGOMA BADO NGUMU

Mahakama ya Hakimu Mkazi ya Kisutu, leo tena imeahirisha kesi inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Amatus Liyumba hadi Julai 28 mwaka huu.
Wakili wa Serikali Justuce Mulokozi aliiomba mahakama hiyo kupanga tarehe nyingine wakati wakiendelea na maandalizi ya kuwasomea maelezo ya awali.
Awali mbele ya Hakimu Mkazi Eva Nkya, wakili wa upande wa utetezi, Hudson Ndusyepo, aliomba upelelezi wa kesi hiyo uharakishwe
Liyumba anakabiliwa na kesi ya matumizi mabaya ya ofisi na kuisababishia Serikali hasara ya zaidi ya Sh. Bilioni 221.
CHANZO: ALASIRI

No comments:

Post a Comment