.

.

.

.

Monday, July 13, 2009

MAHAKAMA YA KADHI

Mufti wa Tanzania, Sheikh Mkuu Issa bin Shaaban Simba ameunda kamati maalumu ya Masheikh 25 ambao watakaa na wataalamu wa serikali kuandaa mfumo wa uendeshaji wa mahakama ya Kadhi nchini.Uteuzi huo ni utekelezaji wa makubaliano ya kikao kilichofanyika wiki iliyopita kati ya waislamu wa madhehebu yote nchini walioongozwa na Mufti Simba na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwa niaba ya serikali.Kaimu Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu(Bakwata) Suleiman Lolila, katika taarifa yake leo, alisema kamati hiyo ambayo iko chini ya uenyekiti wa Mufti Simba, ina wanasheria wa kiislamu, mawakili wa kujitegemea na wataalamu wa fani za jamii.

No comments:

Post a Comment