.

.

.

.

Thursday, July 02, 2009

NGONO YAUA PWANI

JESHI la Polisi mkoani Pwani linamshikilia Godfrey Mapunda (36) kwa ajili ya kumhoji na pia kunusuru maisha yake, baada ya mwanamke anayedaiwa kuwa mke wa mtu kufa walipokuwa wakifanya tendo la ndoa. Imeelezwa mwanamke huyo mwenye umri wa miaka 44 (jina linahifadhiwa) ni mke wa mtu, hata hivyo, alikuwa na uhusiano batili na Mapunda ambaye ni rafiki wa karibu wa mumewe.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani Absolom Mwakyoma, alithibitisha kutokea kwa tukio juzi, saa moja usiku. Alisema mwanamke huyo aliaga kwa mumewe kuwa anakwenda kufungua mgahawa wa familia uliopo Picha ya Ndege. Mwakyoma alisema kwa mujibu wa taarifa zilizofikishwa polisi, badala ya kwenda kwenye biashara hiyo, mwanamke huyo alikwenda kwa Mapunda. Kamanda Mwakyoma alisema wakati wawili hao wakiwa kwenye tendo la ndoa, ghafla hali ya mwanamke ilibadilika, jambo lililomfanya Mapunda kuwaita wapangaji wenzake ili kumpa msaada. Alisema wapangaji walilazimika kumwita mjumbe wa Serikali ya Mtaa aliyetajwa kwa jina moja la Kimali, ambaye aliamuru awahishwe kwenye hospitali ya Tumbi kwa uchunguzi. Kamanda Mwakyoma alisema wakati mwanamke huyo akipelekwa hospitali, Kimali aliamua kumjulisha mume wa marehemu juu ya tukio hilo, ambaye alifika na kuthibitisha kuwa ni mkewe.

Imeelezwa kuwa, Mapunda ni rafiki wa karibu na mume wa marehemu (jina linahifadhiwa), ambaye pia amekiri kuwa mtuhumiwa ni rafiki yake na ameshangazwa na kilichotokea. Kutokana na tukio hilo, Mapunda anashikiliwa na polisi kwa ajili ya uchunguzi kuhusu tukio hilo na pia kunusuru maisha yake kutokana na wananchi kutaka kumdhuru.

No comments:

Post a Comment