.

.

.

.

Tuesday, February 16, 2010

SS HAMADI AKABIDHIWA TUZO HAPA UINGEREZA


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Wananchi (CUF) Maalim Seif Sharif Hamad ametunukiwa nishani na Wazanzibari waishio nchini Uingereza kwa juhudi zake za kutafuta ufumbuzi wa migogoro ya Zanzibar.
Kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari, nishani hiyo alikabidhiwa juzi nchini Uingereza yenye kigae na alama ya visiwa viwili vya Unguja na Pemba, ikiashiria kuzaliwa kwa kizazi kipya cha Wazanzibar.
Kabla ya kuanza kwa mkutano uliondaliwa na jumuiya ya wazanzibari waishio London (Zawa), Maalim Seif alipokewa na kuvishwa shada la maua katika mkutano huo uliofanyika eneo la Earlham Grove mtaa wa Forest Gate, jijini London.
Tumekabidhi tuzo hii maalim Seif kwa kuwa tunajua amejaribu sana kutafuta ufumbuzi wa matatizo ya Zanzibar na amekuwa mstari wa mbele katika masuala kama hayo kwa hivyo sasa sisi Wazanzibari tumefurahi sana. Anajenga Zanzibar mpya,kilisema chanzo chetu cha habari kilichoshuhudia sherehe hizo.

Akijibu maswali mbalimbali katika mkutano huo kuhusu maridhiano yake na Rais Karume, Malimu Seif alisema yametokana historia inaonyesha wazanzibari wameishi katika miongo mingi bila ya kuelewana na hakuna sababu ya msingi ya wananchi hao ndugu kutoishi kwa umoja na mshikamano.

Wakati huo huo Maalim Seif katika mahojiano yake na kituo cha radio ya DW Ujerumani, alielezea hatua zitakazofuata katika kuendeleza maridhiano yake na Rais Karume kwamba mwisho wake ni kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa nah ii itakuwa baada ya kufanyika kwa kura ya maoni.

Maalim Seif alizitaja hatua nyingine ni pamoja na kuundwa kwa kamati ya watu sita ambayo itasimamia kura hiyo ya maoni na kuwekwa kwa masharti katika upigaji wa kura hizo za wananchi, kuingia katika kampeni na hatimaye kupiga kura na kutolewa matokeo ya kura hizo juu ya wananchi kutaka au kukataa kuundwa kwa serikali hiyo.

Mambo mengine ni kurekebishwa kwa daftari la kudumu la wapiga kura ambalo litakubalika na wadau wote wa uchaguzi na kuandaliwa mswaada wa kuundwa kwa serikali ya umoja wa kitaifa na kuweka vifungu vya masharti.

No comments:

Post a Comment