.
.
Wednesday, May 19, 2010
MASAUNI NJIA PANDA
JOTO la kisiasa ndani ya Umoja wa Vijana wa CCM sasa limefikia nyuzi 100, baada ya naibu katibu mkuu wa jumuiya hiyo visiwani Zanzibar, Nassoro Moyo, kuamua kujiuzulu, huku mwenyekiti wake, Hamad Yusuph Masauni, akiwa amekalia kuti kavu.
Tangu juzi, vijana hao wa CCM wamejichimbia mjini Iringa kwa ajili ya mkutano ho muhimu wa baraza kuu, ambao ulitanguliwa na semina na kamati ya utekelezaji lakini ukiwa umegubikwa na msuguano ambao unakiweka chama katika wakati mgumu katika kipindi cha kuelekea uchaguzi mkuu wa Oktoba.
Kabla ya kwenda Iringa, tayari wajumbe walishaingia kwenye vita baada ya kusambazwa waraka uliokuwa ukimtaka Masauni ajiuzulu huku wajumbe wengine kutoka kambi ya mwenyekiti huyo nao wakimtaka Moyo aachie ngazi.
Hadi jana jana jioni, hali ilikuwa ni ya wasiwasi baada ya kufanyika kikao cha kamati ya utekelezaji ambacho inaelezwa Moyo aliandika mwenyewe barua ya kujiuzulu kwa maslahi ya umoja huo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ndani ya kikao hicho, Moyo aliandika barua hiyo ikiwa ni sehemu ya kunusuru jumuiya katika kipindi hiki ambacho imekumbwa na mparaganyiko mkubwa.
Wakati wote jioni, ukumbi wa Siasa ni Kilimo ulikuwa umedhibitiwa vema na polisi wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) wakishirikaina na wana usalama wengine.
Habari zinasema kuwa Masauni alitakiwa na katibu wa CCM, Yusuf Makamba ajiuzulu kwa hiari yake, lakini aligoma na kujitetea dhidi ya kashfa inayomkabili ya kughushi umri wakati anagombea nafasi hiyo mwaka 2008.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment