.

.

.

.

Wednesday, August 04, 2010

VIGOGO 61 WAANGUSHWA CCM

BAADA ya vigogo wengi kuanguka katika kura za maoni kwenye mchakato wa kuwateua wanaowania ubunge na udiwani kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), baadhi ya wana-CCM wamesema wembe ni ule ule na kwamba wasiokubalika bado wataendelea kunyolewa.

Wanachama hao wamesema wapo baadhi ya wananchi ambao wamekuwa wakijiuliza kwanini vigogo wengi wamebwaga lakini, wamesema, ukweli ni kwamba hawakuwa na faida kwa CCM na wameotesha mizizi inayozidi kukimaliza chama.

Wamedai kuwa kutokana na hali hiyo wamekuwa wakiteseka kwa muda kutokana na maisha magumu.

Wamesema wapo baadhi ya viongozi ambao wameongoza kwa muda mrefu na wameweka watu wao ili waje wawarithi.

Wamesema kuanzishwa kwa utaratibu huu kunaweza kusaidia wagombea wanaoteuliwa kuacha tabia ya kutotembelea majimbo yao na kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili wananchi.

Baadhi ya vigogo 61 waliobwagwa katika kura za maoni ni pamoja na Juma Ngasongwa, Mwichoum Msomi, John Shibuda, Joel Bendera, Adam Kimbisa, Wilson Masilingi, Bakari Mwapachu, Joseph Mungai, Jackson Makweta.

Wengine ni Mwantumu Mahiza, Shamsa Mwangunga, Aloyce Kimaro, Mgana Msindai, Ibrahimu Msabaha, Prof. Idrisa Mtulya.

Wengine ni Zainabu Gama, Tabu Ntimizi, Felix Mrema, Monica Mbega,William Shelukindo, Lucas Selelii, Mohamed Yakub, Muhidhir Muhidhir.

No comments:

Post a Comment