.

.

.

.

Wednesday, September 29, 2010

MISS WETU HUYOOO .............

Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel akiwa ameshikilia bendera ya Tanzania mara baada ya kukabidhiwa rasmi leo tayari kwa safari yake ya kuelekea nchini China katika jiji la Sanya ambako shindano la Miss World 2010 linatarajiwa kufanyika Oktoba 31 mwaka huu nchini humo. Mrembo huyo ataondoka kesho kwa ndege ya Shirika la ndege la Quatar Airways akipitia Uarabuni, Mongolia na kisha Sanya nchini China.
Esther Mkwizu ambaye ni Mwenyekiti wa Sekta Binafsi na aliyekuwa mgeni rasmi katika hafla ya kukabidhi bendera ya taifa kwa Vodacom Miss Tanzania Genevive Emmanuel akikabidhi bendera hiyo huku wazazi wa Genevive wakishuhudia kulia ni baba yake Bw. Emmanuel Mpangala na kushoto ni mama yake Mary.

Hisani ya fullshangwe blog

1 comment:

  1. I love her very much....anavutia and i wish her all da best

    ReplyDelete