.

.

.

.

Friday, March 13, 2009

MSANII SAJUKI NA MCHUMBA WAKE WAPATA AJALI MBAYA


msanii wa kundi la maigizo la Kaole ambaye pia ni muigizaji wa filamu nchini, Juma Kilowoko pamoja na mchumba wake ambaye pia ni msanii aitwaye Wastara (pichani juu) wamepata ajali na kuumia vibaya...

Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa nne asubuhi katika maeneo ya Tabata jijini Dar es Salaam baada ya kugongwa na gari wakati wawili hao wakiwa wamepakia kwenye pikipiki.
Imeelezwa kuwa, Wastara amekatika mguu huku Sajuki akiwa ameumia vibaya na wote wamepelekwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa matibabu.Ajali hiyo mbaya imetokea ikiwa imebaki miezi michache wawili hao kufunga ndoa baada ya kuwa katika uchumba kwa muda mrefu.Sajuki na mpenzi wake huyo wamejipatia umaarufu mkubwa kupitia filamu yao inayokwenda kwa jina la ‘Mboni yangu’ ambapo mpenzi wake huyo naye alishiriki.Akiongea kwa shida Sajuki alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kueleza kuwa, bado anapatiwa matibabu katika hospitali hiyo ya Taifa.

6 comments:

 1. Jamani cute girl amekatika mguu, Mungu awajalie nafuu haraka na awape nguvu ya kuendelea kushikamana pamoja

  ReplyDelete
 2. I'M SO SORRY! DAMN PEOPLE HOW ARE YOU GUYS DOING NOW

  ReplyDelete
 3. jamani poleni kabisa msikate tamaa huyo atakuwa ni shetani tuy

  ReplyDelete
 4. sory God hatawalinda mtapona tu ni mitihani

  ReplyDelete