.

.

.

.

Monday, October 18, 2010

MELI YA TIBA KUTUA KESHO BONGO


balozi wa China Tanzania Liu Xinsheng (katikati)akizungumza na waandishi wa habari idara ya Maelezo.Wengine ni Mkurugenzi msaidizi idara ya habari Sozy Mahmoud na mwingine Naibu Mkuu na Mshauri wa masuala ya siasa ubalozi wa China nchini Fu Jijun (kulia).
Wananchi wa Mombasa wakitibiwa katika meli hiyo
Katika picha inaonekana " Peace Ark " ikisindikizwa na meli mbili za vita za China "Weishanhu" na " Lanzhou " wakati wa mazoezi katika ghuba ya Aden hivi karibuni
------

WAKAZI wa Dar es Salaam wanatarajiwa kupata huduma za kinga na tiba kutoka meli maalumu ya tiba ya Jeshi la China ambayo itapiga nanga Oktoba 19, mwaka huu.Meli hiyo yenye madaktari na wauguzi takribani 428 itatoa huduma hizo bure. Akizungumza na waandishi wa habari Jijini, Balozi wa China nchini Tanzania, Liu Xinsheng alisema, huduma hizo zinatarajiwa kutolewa kwa siku tatu kuanzia Oktoba 20, 21 na 22.

“Tunawataka wananchi wenye matatizo mbalimbali kujitokeza katika meli hiyo na kupatiwa matibabu kwa matatizo mbalimbali yanayowasumbua,“ alisema Xinsheng.
Alisema meli hiyo itatoa huduma za vipimo, ushauri, tiba ya asili kutoka China pamoja na tiba ya kisasa na upasuaji mkubwa na mdogo.

Alisema meli hiyo inayoitwa ‘Ark Peace’ ina vitanda 500 na vyumba vya upasuaji vinane kwa ajili ya kutoa huduma ya kulaza wagonjwa watakaoonekana kuwa wanahitajika kupewa huduma hiyo na kwamba huduma zote zitafanyika ndani ya meli.

Meli hiyo kwa sasa ipo kwa majirani zetu Kenya na imekuwa ikiwasaidia wananchi wa huko.
Serikali ya Kenya has applauded the visit of the Chinese navy hospital ship 'Peace Ark'.

Katika picha inaonekana " Peace Ark " ikisindikizwa na meli mbili za vita za China "Weishanhu" na " Lanzhou " wakati wa mazoezi katika ghuba ya Aden hivi karibuni

No comments:

Post a Comment