.

.

.

.

Sunday, December 05, 2010

HAFLA YA UWF


Mkurugenzi wa Prime Time Promotions Ltd,Juhayna Ajmi Kusaga ambaye pia ni mmoja wa wanachama wa UWF akifafanua jambo kuhusiana na maadhimisho ya miaka mitano ya chama chao,alipokuwa akifanya mahojiano mafupi na Clouds TV kwenye hafla iliofanyika ukumbi wa Kibo wa hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar.
Meza kuu pamoja na wanachama wa UWF . Walioketi toka kulia ni Waziri wa Nishati na Madini Mh. William Ngereja, akifuatiwa na Gavana wa Benki Kuu Profesa Benno Ndullu na mgeni rasmi Mama Margaret Chacha
Mkurugenzi Mkuu wa Benki ya Wanawake Mama Chacha akiwa na wana UWF mara baada ya kuzindua tovuti yao.
Mfano wa picha ya kuchorwa ikipigwa mnada ukumbini humo kwa ajili ya mradi wa SOMKI
Wageni waalikwa mbalimbali wakiserebuka ukumbini kwenye hafla hiyo.
Baadhi ya wanachama wa UWF wakijiachia mara baada ya shughuli nzima kufana kwa kiasi kikubwa.
Dj Too Shoot akiwarusha wageni waalikwa kwa mangoma ya nguvu kabisa na kufanya ukumbi kuchangamka mno.
Wageni waalikwa mbalimbali wakijimwaya mwaya usiku wa kuamkia leo wakati wa kusherehekea miaka mitano ya umoja wao kwenye hafla iliyofana sana katika ukumbi wa Kibo wa hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar.
Wasanii mahiri kutoka THT,Amin na Linah wakitumbuiza mbele ya wageni waalikwa usiku wa kuamkia leo kwenye hafla hiyo iliyofana kwa kiasi kikubwa.
Mratibu wa UWF,Mariam Shamo akimkabidhi mshindi wa simu ya Nokia na muda wa maongezi wa shilingi 50,000 mara baada ya kushinda bahati nasibu.Pichani kati anayepiga makofi ni Mkurugenzi mawasiliano na mahusiano kutoka kampuni ya bia ya Serengeti (SBL).Teddy Mapunda
Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya Clouds Media Group Bw.Joseph Kusaga akisoma mshindi wa bahati nasibu iliyochezesha usiku huo kwenye hafla ya kutimiza miaka mitano ya chama UWF.
Mgeni rasmi, Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Wanawake Mama Margaret Chacha akitangaza washindi wa bahati nasibu iliyochezeshwa usiku huo.Wakishuhudia pichani kulia ni Mwenyekiti wa UWF ,Mwate Madinda na kushoto kwake ni Mratibu wa UWF ,Mariam Shamo huku shughuli nzima ikiongozwa na Mtangazaji wa Choice FM,Baby Kabae.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Wanawake Tanzania (TWB),Mama Margaret Chacha akizindua tovuti ya UWF kwenye hafla hiyo usiku wa kuamkia leo,kulia kwake ni Mwenyekiti wa UWF Mwate MadindaMratibu wa UWF,Mariam Shamo akiwakaribisha wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo akiwemo sambamba na mgeni rasmi ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Wanawake Mama Margaret Chacha.
Bahati nasibu ikianza kuchezeshwa mbele ya Wageni waalikwa usiku wa kumkia leo kwenye hafla ya kutimiza miaka mitano na pia kuchangia mfuko wa kusomesha mtoto wa kike (SOMKI) iliyoandaliwa na Unity of Women Friends (UWF).
Wageni waalikwa mbalimbali kwenye hafla hiyo.
Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mkurugenzi mkuu wa Benki ya Wanawake Mama Margaret Chacha (katikati) akibadilishana mawazo na wagini waalikwa.

Wageni waalikwa mbalimbali waliofika kwenye hafla hiyo usiku wa kumkia leo ya kutimiza miaka mitano na pia kuchangia mfuko wa kusomesha mtoto wa kike (SOMKI) iliyoandaliwa na Unity of Women Friends (UWF),iliyoafana sana katika ukumbi wa Kibo wa hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es salaam ..

No comments:

Post a Comment