.

.

.

.

Tuesday, May 10, 2011

MULA OMAR AANZA KUSAKWA




VIKOSI maalumu vya Marekani na Pakistani, vimeanza harakati za kumsaka kiongozi wa wanamgambo wa Taliban,Mullah Omar, baada ya kupata taarifa mpya kuhusu mahali alipo kiongozi huyo.Taarifa za kiupelelezi zinadai kuwa, kiongozi huyo mwenye jicho moja, anadaiwa kuwa amejificha katika mji uliopo Magharibi mwa Pakistani, Quetta, karibu na mpaka wa Afghanistan.

Mtandao wa makachero wa Pakistan (ISI), unasema kuwa, kikosi hicho kimepania kumkamata kikiwa cha kwanza baada ya kusononeshwa na oparesheni ya Marekani, ambayo ilisababisha kifo cha kiongozi wa Al Qaeda, Osama Bin Laden.

Imeelezwa kuwa, timu hiyo ya kikosi cha Marekani imeamua kuanzisha msako dhidi ya Omar, baada ya kukusanya taarifa nyingi kutoka nyumbani kwa Bin Laden, katika mji wa Abbottabad.

Mbali na Mullah, kikosi hicho cha Marekani kinataka kuwahoji wake watatu wa Bin Laden ambao wanashikiliwa nchini Pakistan waliokutwa naye wakati akiuawa.

Hata hivyo, Omar(52), ambaye alikuwa akimlinda Bin Laden nchini Afghanistan, wakati wa shambulizi la Septemba 11,2001, anasemekana kuwa, amezungukwa na mamia ya wapiganaji wenye silaha na inatarajiwa watakuwa wakifuatilia kuhusu kushambuliwa.

Mmoja wa makachero waandamizi kutoka ISI ambaye alithibitisha kuanza msako wa kumsaka Mullah, amesema kuwa: "Kuna hatua kubwa za kijeshi zitakazochukuliwa hivi karibuni katika mji wa Quetta.

"Uamuzi huo umechukuliwa kabla ya Marekani kupata nafasi ya kurudia mpango iliyoufanya dhidi ya Bin Laden. Tujaribu kumpata akiwa hai, lakini endapo ataleta upinzani, tutamuua," amesema ofisa huyo.

Omar ambaye alikuwa mtu wa karibu na mlinzi mkuu wa Osama nchini Afghanistan wakati wa shambulizi la Septemba 11,2001, pia ametangaziwa dau la dola milioni 25, endapo utapata kichwa chake.

Mchakato huo pia ni wa kumsaka naibu kiongozi wa al-Qaeda, Ayman Al-Zawahiri, ambaye anasemekana kuwa, yupo Pakistan.

No comments:

Post a Comment