.

.

.

.

Sunday, July 10, 2011

YANGA YAIFUNGA SIMBA NA KUCHUKUA KOMBE LA KAGAME


Timu ya Yanga Africans ya Tanzania imechukua ubingwa wa michuano ya klabu bingwa Afrika Mashariki na Kati baada ya kuichapa Simba Sports club pia ya Tanzania kwa goli 1-0.

Mbali na kuchukua kombe, Yanga pia imezawadiwa dola elfu 30 za Kimarekani.

Bao hilo la pekee na la ushindi lilifungwa na Kenneth Asamoah, mchezaji wa kulipwa kutoka Ghana. Mara baada ya dakika tisini kumalizika kwa timu hizo kutoka suluhu ya bila kufungana, dakika 30 ziliongezwa na ndipo Goli hilo la ushindi kwa Yanga likapatikana katika dakika ya 108.

Timu hiyo imekabidhiwa kombe lake kizani mara baada ya umeme kukatika nazo juhudi za kuurejesha umeme huo kushindikana.

Mchezo huo wa fainali ulichezwa katika Uwanja mpya wa Taifa jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment