.

.

.

.

Saturday, October 08, 2011

CABO SNOOP KUTUMBUIZA JIONI HII LIDAZ CLUB

Cabo Snoop

Herieth Makwetta
JUMLA ya wasanii tisa, wanatarajia kumsindikiza mkali wa muziki wa staili ya Kuduro, Ivo Manuel Lemus a.k.a Cabo Snoop kutoka nchini Angola atakayetumbuiza katika siku ya familia (Family Day) leo katika viwanja vya Leaders Club jijini.

Muangola huyo ambaye amejichukulia umaarufu kutokana na vibao vyake vya Prakatatumba na Windek alianza kufanya tamasha hilo jana mjini Morogoro, kabla ya kuhamia jijini Dar es Salaam.

Cabo Snoop ambaye alianza kufanya ziara Afrika Mashariki wiki iliyopita katika tamasha la Tusker All Stars jijini Nairobi, atasindikizwa na wasanii kama Asley, Dogo Janja, Godzilla, Barnabas, Linah, Twanga Pepeta, Bob Junior na Diamond.

Waandaaji wa tamasha hilo Prime Time Promotion wamesema kuwa tamasha hilo limepangwa kufanyika siku mbili mjini Morogoro na Dar es Salaam.

"Tamasha litaanzia mjini Morogoro na baadaye jijini ambalo litakuwa ni la kifamilia zaidi. Tamasha litaanza mchana na linatarajiwa kumalizika mapema" walieleza.

Cabo Snoop ambaye amejizolea umaarufu mkubwa Afrika na nje ya Afrika kwa sasa, ana albamu yenye nyimbo 14 zenye mahadhi ya Kuduro. Baadhi ya nyimbo hizo ni pamoja na “Pracatatumba”, “Vamos lá”, “Slow motion”, “Windeck”, “Walalipo” na “Zangala Guduma”

No comments:

Post a Comment