.

.

.

.

Friday, October 14, 2011

MUSTAPHA SABODO AMWAGA MAMILLIONI KWA CHADEMA

Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa (kushoto) akimsaidia Kada wa CCM, Mustafa Sabodo kunyanyuka kwenye kiti nyumbani kwa kada huyo Upanga, jijini Dar es Salaam jana. Picha na Michael Jamson


Geofrey Nyang’oro
KADA wa CCM, Mustafa Sabodo ameahidi kuchimba visima 200 katika majimbo yote ya wabunge wa Chadema nchini, huku akieleza kuwa angependa kuona upinzani unachukua nchi mwaka 2015.Sabodo ambaye ni kada wa CCM tangu enzi za Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyarere, alitoa kauli hiyo jana alipokuwa akipokea mpango wa uchimbaji visima hivyo kutoka kwa Katibu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa.Kauli hiyo ya Sabodo ambaye tayari katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka jana aliisaidia Chadema Sh100 milioni za kampeni, imekuja kipindi ambacho CCM, inakabiliwa na mpasuko kutokana na siasa za makundi.

Wakati CCM ikikabiliwa na kipindi hicho kigumu kisiasa, jana Sabodo ambaye aliahidi kuendelea kukisaidia Chadema, alisema “Ningependa kuona upinzani ukichukua nchi mwaka 2015”.

Jana Saa 4:00 asubuhi, Dk Slaa akiongozana na Mkurugenzi wa Mambo ya Bunge wa Chadema, John Mrema walifika nyumbani kwa Sabodo kwa lengo la kukabidhi mchakato wa utekelezaji wa mradi huo wa visima na pia kumshukuru kada huyo wa CCM kwa m
isaada yake kwa chama hicho.

Katika mazungumzo hayo, Sabodo alimhakikishia Dk Slaa kwamba ataendelea kusaidia chama hicho katika miradi mbalimbali, inayohusu wananchi hususani suala la maji na elimu.

Sabodo alisema elimu ni muhimu katika maisha ya binadamu, lakini maji pia ni uhai, kwakuwa bila maji hakuna mtu anayeweza kufanya chochote.

Mradi wa Sh2.5 bilioni
Sabodo alisema ametenga Sh2.5 bilioni kwa ajili ya kuchimba visima vya maji virefu na vifupi 700 katika maeneo yenye ukame, huku visima 200 kati ya hivyo vikielekezwa katika majimbo 23 wanakotoka wabunge wa Chadema na Jimbo la Igunga. Chadema kina jumla ya wabunge 48 na 25 kati yao ni wa Viti Maalum.

Alifafanua kwamba anatoa msaada wa maji kwa sababu anatambua umuhimu wa huduma hiyo kwa jamii huku akisisitiza kwamba maji siyo anasa bali ni hitaji la lazima.

No comments:

Post a Comment