.

.

.

.

Thursday, October 06, 2011

PRECISION AIR KUUZA HISA ........

Bodi ya Wakurugenzi wa shirika la ndege la Precision Air Services Plc inapenda kuwataarifu kwamba mpango wetu wa Uuzaji wa Hisa katika Soko la Awali (IPO) na kuorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es salaam (DSE) imepatiwa vibali vyote husika na sasa ipo tayari kwa hatua zinazofuata.

Kilichoidhinishwa ni ratiba ya matukio ya utaratibu mzima wa mchakato huu:

Tarehe ya Ufunguzi wa Ofa
Oktoba 7 2011 ; 0300 asubuhi
Tarehe ya Kufungwa kwa Ofa
Oktoba 28 2011 ; 1000 jioni
Kutangazwa kwa matokeo ya Ofa
Novemba 11 2011
Kuingiza hisa katika akaunti za CDS, kutoa risiti/cheti za malipo na marejesho ya hundi
Novemba 25 2011
Kuorodheshwa na kuanza biashara ya kununua na kuuza katika Soko la Hisa la Dar es Salaam (DSE)
Desemba 8 2011

Kampuni itatoa jumla ya hisa 58,841,750 kwa ajili ya ununuzi kwa bei ya 475 kwa kila hisa. Huku idadi ya chini ya kuanza kununua hisa ambayo mtu ataruhusiwa kununua itakuwa ni hisa 200.

Nakala ya waraka wa matarajio ya kampuni ambayo pamoja na mambo mengine, maelezo maalumu ya ufafanuzi na ununuzi wa hisa zinapatikana katika tovuti ya Precision Airwww.precisionairtz.com tarehe 4 Oktoba 2011.


Kwa niaba ya Wakurugenzi ya Bodi, utawala na wafanyakazi wote napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa wateja wetu kwa mchango wao na ushirikiano yakinifu ulioweza kufanikisha maendeleo na ukuaji wa shirika la ndege hili tangu kuanzishwa kwake mwaka 1993.


Michael N Shirima

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi

No comments:

Post a Comment