.

.

.

.

Thursday, January 19, 2012

IDARA YA UHAMIAJI KUPANGULIWA

WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Shamsi Vuai Nahodha, amesema ndani ya wiki mbili atafanya mabadiliko makubwa katika Idara ya Uhamiaji Makao Makuu kwa lengo la kuboresha 
utendaji kazi. 

Aidha, alisema ametoa wiki moja kwa Ofisa Uhamiaji wa Mkoa wa Tanga kuondoshwa na 
kupelekwa makao makuu baada ya wananchi wa mkoa huo kulalamika kutoridhishwa naye. 

Nahodha alisema hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kupokea msaada wa magari 11 na boti tatu kutoka Serikali ya Japan kwa ajili ya kuimarisha doria katika kukabiliana na wahamiaji haramu. 

Alisema anachohitaji ni viongozi wachapa kazi na waadilifu, hivyo atakayekwenda kinyume 
atamchukulia hatua kwa mujibu wa taratibu zilizopo. 

“Mimi napenda kufanya kazi kwa uwazi, hivyo niwaambieni, kwamba ndani ya wiki mbili nitachukua hatua na kufanya mabadiliko Idara ya Uhamiaji, kila ninapoona tatizo au ninapoletewa tatizo nalifanyia kazi ndiyo nachukua hatua, sitaki kuambiwa nafanya ubabe,” 
alisema. 

Aliendelea: “Mnafahamu kwamba Zimamoto palitokea wizi, sasa nimewaondoa viongozi wote pale mkitaka mwende mkahakikishe, Tanga nako nimeagiza Ofisa Uhamiaji wa Mkoa aondolewe aletwe makao makuu, pia kama kuna mahali hamridhiki na utendaji wa mtu, 
leteni taarifa nitazifanyia kazi na kuchukua hatua”. 

Alisema haridhiki na jinsi Idara ya Uhamiaji inavyoshughulikia wahamiaji haramu na kuwataka kutumia vikundi vya Ulinzi Shirikishi na Polisi Jamii, ambavyo vinafanya kazi na Jeshi la Polisi katika kukabiliana na uhalifu ili kukomesha uhamiaji haramu. 

“Wahamiaji haramu kama ni watu wabaya, wanaweza kufanya mambo ya hatari sana na 
kudhuru watu, pia wanapoingia nchini kuwasafirisha ni gharama kubwa na tunatumia fedha za 
Serikali, sasa kwa nini tutumie fedha zetu kuwasafirisha? 

Uhamiaji wajipange upya kushughulikia tatizo hili,” alisema. Alisema pamoja na kwamba 
mipaka ya nchi ni mikubwa ameagiza helikopta ya Jeshi la Polisi itumike kufanya doria 
mipakani, ili kukabiliana na wahamiaji hao ambao wamekuwa wakipita nchini kwenda Afrika Kusini na nchi za mbali kwa ajili ya kujitafutia maisha. 

Nahodha aliishukuru Japan kwa misaada ambayo imekuwa ikiitoa na kuwataka waliopewa 
kuitumia kwa uangalifu kwa malengo yaliyokusudiwa katika kukabiliana na wahamiaji 
hao. 

Kwa upande wake, Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada, alisema msaada huo wameutoa kwa ajili ya kusaidia doria katika mikoa ya Mbeya, Mtwara, Lindi na Tanga ambayo mara nyingi wahamiaji wamekuwa wakipitia

No comments:

Post a Comment