.

.

.

.

Thursday, January 12, 2012

MACHANGUDOA WALALAMIKIA KUTOLEWA KWA SIMBA NA YANGA

KITENDO cha kutolewa Simba na Yanga kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi kimewaudhi kwa akinadada wanaojiuza maarufu kama (Changudoa) waliokuwa wamejazana katika hoteli mbalimbali visiwani Zanzibar.

Wakizungumza  kwa nyakati tofauti Machanguduo hao walisema kufungwa kwa timu hizo kumeharibu mipango yao na kufanya biashara zao kuwa ngumu.Angel Charles maarufu kama (Miss Money) alisema alianza kunufaika na mashindano hayo kwani kila Simba na Yanga zilipocheza aliweza kuingiza zaidi ya Sh 200,000.

“Sikiliza kaka  yangu unajua hapa ni Zanzibar sio kwetu sisi tunakaa hoteli tunalipa kila kitu na lengo lilikuwa ni kuwapata wateja ambao ni mashabiki wa hizi timu za Simba na Yanga, sasa zote zimetolewa unafikiri tukiendelea kuishi hapa tutaishi vipi, maisha ya Unguja ni magumu, pili hapa kuna Macd kibao kila kiwanja unachojaribu kwenda wamekaba kote,”alisema Angel.

Sofia Rashid Zuberi maarufu kwa jina la Cash alisema yeye alipanga katika hoteli iliyopo maeneo ya Uwanja wa Amaan akiwa na wenzake wawili na kazi yao ni kwenda uwanjani siku ambazo Simba na Yanga zinacheza na kutafuta mashabiki waliofika Zanzibar kwa ajili ya kuangalia mpira na baada ya mechi wanakwenda kulala katika vyumba hivyo.

“Ingawa sio wote wanaokubali kulala kwa sababu tayari wanakuwa wameshapanga hoteli zingine pamoja na wenzao na hasa ukizingatia kwamba hoteli nyingi za Zanzibar ni 'Self Container' hivyo watu wa aina hiyo tunakuwa nao mchana na wale wasiokuwa na vyumba ndio tunawalaza katika vyumba vyetu usiku, ”alisema Cash.

Akifafanua juu ya kuwahifadhi hao wateja wao alisema wakati mwingine wanafanya mawasiliano nao kabla ya hawajafika Unguja na wakati mwingine wanaenda kuwasubiri bandarini ili wasiweze kukata tiketi ya kurudi kwa sababu siku ambazo kuna mechi baadhi ya meli za usiku zinasubiri hadi mechi imalizike hivyo wanawakamata mapema kwa sababu wana uhakika wa kupata mahali pa kulala.
   
Mwanadada mmoja aliyejitambulisha kwa jina moja la Mrs Manoti alisema, “Mimi nimepanga katika hoteli ya Uwanjani na pale ninakaa na wachezaji wa mpira wa netiboli ya Tanzania na wengine kutoka Uganda, lakini wenzangu walikuwa na bahati ya kupanga katika hoteli zilizofikiwa na timu za soka.

No comments:

Post a Comment