.

.

.

.

Wednesday, February 29, 2012

INJILI ILIOTABIRI KUJA KWA MTUME MOHAMED SAW YAPATIKANA UTURUKINakala ya Injili ya miaka 1500 iliyopita na ambayo imepatikana tena katika kanisa moja nchini Uturuki baada ya kupotea kwa muda wa miaka 12, ina utabiri wa kuja Mtume wa Uislamu, Nabii Muhammad SAW baada ya Masihi Issa yaani Yesu AS.

Vyombo vya habari vimeripoti kuwa, nakala hiyo ya zamani sana ya Injili imeandikwa kwa lugha ya Kiarami na vyombo vya habari vinasema kuwa, ilikuwa imefichwa kwa muda wa miaka 12.

Tayari viongozi wa Vatican wameonesha hamu kubwa ya kuipata Injili hiyo na Papa Benedict wa 16 ametoa mwito wa kufanyiwa uchunguzi maandishi ya Injili hiyo.

Kwa upande wake, Waziri wa Utamaduni wa Uturuki, Ertuğrul Günay amesema kuwa, bei ya Injili hiyo ni dola milioni 22 za Kimarekani na kwa vile utabiri wa kuja Mtume Muhammad SAW unapatikana kwenye Injili hiyo yenye lugha ya Nabii Issa AS, ilikuwa imefichwa ili watu wasiione.

Amesema maneno yaliyomo kwenye Injili hiyo ya miaka 1500 iliyopita yanafanana sana na maneno ya Qur'ani Tukufu na kiujumla maneno yake yanakaribiana sana na mafundisho ya Uislamu.

Sehemu moja ya maneno yaliyomo kwenye Injili hiyo yanamtaja Yesu kuwa ni mwanadamu na kumnukuu Nabii huyo wa Mwenyezi Mungu akisema kuwa, Mtume atakayekuja baada yake anaitwa Muhammad. Sehemu ya maneno ya Injili hiyo ya miaka 1500 iliyopita yana maana isemayo: Kuhani mmoja alimuuliza Masihi Yesu kuhusu mtu atakayekuja kuchukua nafasi yake na Yesu akajibu: "Muhammad (SAW) ndilo jina lake lililobarikiwa, anatoka katika kizazi cha Ismail, baba yangu Mwarabu."

Waziri wa Utamaduni wa Uturuki pia amesema, tayari Papa Benedict wa 16 ametuma maombi rasmi ya kutaka wapatiwe Injili hiyo iliyopatikana kwenye visiwa vya Uturuki vilivyoko kwenye bahari ya Mediterranean. Imeelezwa kuwa watu waliopatikana na Injili hiyo walikuwa wana nia ya kuiuza kimagendo na hivi sasa wanashikiliwa katika mahakama za Uturuki.

Wakati huo huo kasisi Ihsan Uzbek, mmoja wa viongozi waandamizi wa Kikristo nchini Urutuki amesema kuwa Injili hiyo ni ya zama za mtakatifu Barnaba aliyeishi na Nabii Issa na ambaye alikuwa mfuasi wake wa karibu.

Huko nchini Uturuki nako kumetolewa mwito wa kufanyika uchunguzi wa kitaalamu wa kuweza kujua tarehe hasa ilipoandikwa Injili hiyo.CHANZO :http://swahilispeakers.blogspot.com/

1 comment:

  1. my godness! it's very interesting issue. ok let us wait the truth.....

    ReplyDelete