.

.

.

.

Saturday, March 24, 2012

AONYA WANAOKUZA MAKALIO ( WOWOWO)

WANAWAKE wanaotumia dawa au kuchoma sindano kuongeza makalio na viungo vingine vya mwili wametahadharishwa kuwa wanaweza kupata ugonjwa wa saratani. Aidha, wanawake wanaotumia mashine kutaka kusimamisha matiti wametahadharishwa huenda wakashindwa kunyonyesha watoto baadaye wakati wanaotumia vifaa maalumu kuridhisha hamu zao za kimapenzi wameelezwa kuwa wataathirika kisaikolojia. Daktari Ali Mzige akizungumza na HabariLeo Jumapili katika mahojiano maalumu yaliyozaa habari hii, alisema anashangazwa na wanawake na mabinti wa Kitanzania wanaohangaika kunywa dawa na kuchoma sindano kwa lengo la kuongeza makalio au sehemu zingine za viungo vya miili yao huku wakihatarisha afya zao, ikiwa ni pamoja na kupata saratani bila kujua. Mzige alisema wako wanawake wengine wanatumia vifaa maalumu ili kujiridhisha kimapenzi na kwamba wanaotumia vifaa hivyo huathirika kisaikolojia bila kufahamu na ndio hao baadaye wanakataa hata kuolewa kwa sababu tayari wameathirika. “Wanawake hawafahamu wanaiga tu, huko Ulaya wanaofanya mambo haya ya ajabu ni waathirika wa dawa za kulevya au tayari unakuta wameathirika kisaikolojia, lakini sisi tunataka kuiga tu k la kitu badala ya kutumia vitu vya asili,” alisema. Dk. Mzige ambaye pia ni Mkurugenzi wa Hospitali ya IMTU, alisema haoni makalio makubwa yanawapa faida gani wanawake na kwamba uvutaji wa matiti una husisha uvutaji wa misuli inayoshikilia nyama za matiti na matokeo yake baadaye mhusika anakuja kushindwa kunyonyesha mtoto. “Wanawake msidanganyike na vidonge, sindano mnaweza kupata saratani. Hivi ukirefusha matiti, maziwa yatoka wapi ukitaka kunyonyesha, acheni kuharibu afya zenu bila sababu,” alisema. Aliwataka wanawake kuacha kufanya mambo hayo kwa ajili ya kuridhisha watu wengine na kuharibu asili ya mwanamke wa Kitanzania na kuongeza kuwa kama wanawake wanataka kulinda uhalisia wao waache kutumia vitu vikali kama pombe, sigara na badala yake wale vyakula vyenye kujenga mwili. “Kama hutaki kuzeeka haraka acha kunywa pombe, kuvuta sigara, fanya mazoezi na kula vizuri. Ikumbukwe pombe na sigara hupunguza CD4… sijui kama watu wanafahamu kuna baadhi ya vitu ndani ya pombe au sigara mwisho hutumika kutengenezea dawa ya kuhifadhia maiti. “Haya mambo ya kutaka urembo kupita kiasi ndio yalisababisha mke wa Rais wa zamani wa Nigeria, Olesegun Obasanjo,Stella kufa hivi hivi akitafuta urembo wa bandia…unajiuliza mama kama huyu alikuwa na kila kitu amekwenda kufanya nini, ndio hayo ninayoeleza anakuwa tayari ameathirika kisaikolojia,” alisema. Mke wa Obasanjo alikufa wakati akifanyiwa operesheni nchini Hispania akipunguza unene. Alisema siku hizi wanawake wengi wanapopata ajali za magari unakuta ni kwa sababu ya ulevi na wengine ndani ya magari unakuta chupa za pombe kwa maana kwamba wanawake wanakunywa sana vilevi ambavyo baadaye vinaharibu afya zao na wanajiona kama hawapendezi tena na matokeo yake wanakwenda kujitengeneza kwa vitu bandia. Dk. Mzige alisema pia tatizo la umasikini limechangie wanawake kujiingiza katika mambo yasiyofaa, ikiwa ni pamoja kuingiliwa kinyume cha maumbile, jambo alilolielezea kuwa ni baya na linaathiri kwa kiasi kikubwa mfumo wa uzazi wa mwanamke. Alioonya mabinti kuacha kuendekeza umasikini na kujiingiza katika vitendo hivyo visivyofaa kwani madhara yake kiafya ni makubwa na sio utamaduni wa wanawake wa Kitanzania. Hivi karibuni gazeti moja liliripoti kuwepo kwa huduma ya kusimamisha matiti inayofanyika katika Saluni mmoja iliyopo Sinza, jijini Dar es Salaam na mteja hulipia kuanzia Sh 150,000. Habari hiyo ilitaja amshine hiyo kuwa inatiwa ‘Beauty Machine’ na kwamba ina uwezo wa kusimamisha matiti ya kila saizi na kwamba kazi kubwa ya mashine hiyo ni kuamsha misuli ambayo hushikilia nyama za matiti.

1 comment:

  1. HAHAHAA,,,MBUTA NANGA...hivi kisa cha kuanza kuongezea makalio ni nini hasa???? yani nashindwa kulitambua rembo hili la kujiengezee mzigo..yani NINGEPENDA KUMFAHAM ALOWEKA ILI ANIJIBU SWALI LANGU...anyway ,MAISHA NA MARADHI NI YAO ..NA ASOSIKIA LA MKUUU..........!!!

    ReplyDelete