.

.

.

.

Sunday, March 18, 2012

AUNT EZEKIEL AANGUKA NA KUZIMIA !!!


NYOTA wa filamu za Kibongo, Aunt Ezekiel ‘Gwantwa’ (pichani) amepatwa na maswahibu makubwa baada ya kukumbwa na ugonjwa wa ajabu uliomfanya kuanguka na kupoteza fahamu huku akitokwa na mapovu mdomoni. Tukio hilo limetokea usiku wa Jumatano mjini Morogoro ambako Aunt na mastaa wengine walikuwa wakirekodi filamu. Mmoja wa watu waliokuwepo katika tukio hilo, aliyejitambulisha kwa jina moja la Vivian ameliambia amesema kwamba, walipokuwa katika harakati za kurekodi, walimsikia Aunt akitoa sauti kubwa kisha akaanguka, mapovu yakamtoka mdomoni na baadaye akapoteza fahamu. Vivian aliendelea kusema kuwa, baada ya kutokea kwa hali hiyo, wasanii wote walipigwa na bumbuwazi, wakasimamisha shughuli zilizokuwa zikiendelea na kumsaidia mwenzao kumpeleka hospitali ya Mkoa wa Morogoro. “ Tulichanganyikiwa, hakuna mtu ambaye anaweza kukuambia kitu kilichotokea kwa ufasaha na hatujui Aunt amekumbwa na nini, ilikuwa ni kitendo cha ghafla sana,” alisema Vivian kwa majonzi. Kwa mujibu shuhuda huyo, Aunt alipata matibabu katika hospitali hiyo ya mkoa kwa kuchomwa sindano mbili na kutundikiwa dripu tatu ambazo zilimfanya aweze kuzinduka na kuongea. “Kwa kweli tulichanganyikiwa maana alikuwa hafumbui macho, anaongea kwa tabu, alikuwa akiuma meno huku povu likimtoka mdomoni lakini baada ya kupata huduma hiyo alitulia na akafumbua macho,” alisema. Usiku wa siku hiyo, Aunt alitolewa hospitali na utaratibu wa kumrudisha Dar ulikuwa ukiandaliwa. Auntalipigiwa simu na Risasi lakini ilipokelewa na Vivian ambaye alimpatia msanii huyo aliyekuwa akiongea kwa tabu. “Ni kweli naumwa, ila ningeomba nipumzike nitaongea muda mwingine,” alisema Aunt


 CHANZO: RISASI

No comments:

Post a Comment