.

.

.

.

Tuesday, April 03, 2012

BARCELONA YATINGA NUSU FAINALI YA MABINGWA WA LIGI YA ULAYA


BARCELONA usiku huu imetinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa mara ya tano mfululizo, baada ya kuilaza AC Milan mabao 3-1 katika Uwanja wa Camp Nou.
Shukrani kwao, Mwanasoka Bora wa Dunia, Muargentina Lionel Messi aliyefunga mabao mawili kwa penalti na mfungaji wa bao pekee kwenye fainali ya Kombe la Dunia mwaka 2010, Andres Iniesta.
Messi alifunga bao la kwanza dakika ya 11, baada ya yeye mwenyewe kuangushwa kwenye eneo la hatari, kabla ya Antonio Nocerino kusawazisha dakika ya 32.
Alessandro Nesta alimvuta Sergio Busquets na kumuangusha chini na Messi akaenda kufunga kwa penalti tena hilo likiwa bao lake la 14 kwenye michuano hiyo msimu huu.
Kipa Christian Abbiati aliibeba sana Milan, lakini akashindwa kumzuia Andres Iniesta kufunga bao la kuhitimisha ushindi dakika ya 53.
Ikumbukwe mchezo wa kwanza uliofanyika San Siro, Milan timu hizo zilitoka sare ya bila kufungana.

Wachezaji wa AC Milan walionekana kumlalamikiwa refa kwa mara kwa mara kwa maamuzi yake kana kwamba anaibeba Barca.
Katika mchezo mwingine, mabao mawili ya Ivica Olic yalitosha kuipeleka Bayern Munich Nusu Fainali kwa mara ya pili ndani ya miaka mitatu, wakiibwaga Marseille usiku huu mjini Munich.
Bayern iliyoshinda 2-0 kwenye mchezo wa kwanza, ilipata bao la kwanza dakika ya 13, baada ya mchezaji wa zamani wa Marseille, Franck Ribery kumtengenzea nyota wa Croatia nafasi nzuri ya kufunga. 
Olic akapiga la pili dakika ya 37 na kutengeneza ushindi wa jumla wa 4-0.

No comments:

Post a Comment