.

.

.

.

Wednesday, August 15, 2012

HOTUBA YA RAIS LEO MJINI DODOMA


HOTUBA YA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA, MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE AKIZINDUA AWAMU YA TATU YA MFUKO WA MAENDELEO YA JAMII (TASAF III) UWANJA WA JAMHURI, DODOMA, 15 AGOSTI 2012

-
Mhe. Spika;
Mhe. Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
 Mhe. Steven Wassira, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - Uratibu na Mahusiano,;
Waheshimiwa Mawaziri;
Mhe. Daktari Rehema Nchimbi, Mheshimiwa Steven Wassira (Mb);
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma;,
Mheshimiwa Dr. Rehema Nchimbi;
Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge;
Mhe. Katibu Mkuu Kiongozi;
Mwakilishi wa Benki ya Dunia: Tanzania, Uganda na Burundi,
Bwana Philippe Dongier;
Ndugu Peniel Lyimo, Mwenyekiti wa Kamati ya Taifa ya Uongozi wa TASAF;
Mwakilishi wa Benki ya Dunia;
Wawakilishi wa Ndugu Peniel Lyimo;
wWashirika  wetu wangine wa mMaendeleo; ,
Waheshimiwa Viongozi wa Vyama vya Siasa;
Waheshimiwa Wabunge
Viongozi mbalimbali wa vyama vya siasa nawa  Serikali;
Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF;
Wageni wWaalikwa;
Mabibi na Mabwana:;:

Shukrani
Ndugu Wananchi:
Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri Steven Wassira na Nndugu Ladislaus Mwamanga, Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) na Kamati yake kwa kunialika nije kushiriki nanyi kwenye uzinduzi wa Awamu ya Tatu ya TASAF.Tarehe 30 Machi 2000 tulizindua Awamu ya Kwanza ya Mfuko wa Kwa kuwa huko tulipotoka tumepata mafanikio ya kutia moyo, naomba nianze kwa kutoa pongezi na kuwashukuru wote walioshiriki kufanikisha utekelezaji wa awamu mbili za TASAF zilizotangulia. 
Pongezi
Ndugu Wananchi;     
Napenda kuishukuru kwa dhati Benki ya Dunia na Mwakilishi Mkazi wa Benki hiyo wa wao hapa nchini kwa kushirikiana na sisi kutekeleza miradi mbalimbali ya TASAF tangu mwaka 2000. Siku zote  Benki ya Dunia imekuwa mwenzetu muhimu na wa kutumainiwa na hii  inasikiliza hoja zetu na kuzingatia vipaumbele vya sSerikali na wananchi wa Tanzania yetu katika jitihada zetu za kupambana na umaskini na kujiletea maendeleo.  Tunafurahishwa sana na sera ya kusikiliza vipaumbele vyetu.  Jambo hilo Hali hii ndiylo limetuwezesha sisi kushirikiana nao kubuni mpango huu wa TASAF unaofadhiliwa na ubia mzuri wa maendeleo kati yetu Serikali na Benki ya Dunia, , kwa kushirikiana na wadau wengine wa maendeleo, Serikali zetu mbili na wananchi wa nchi yetu. 
Natoa ipongezai nyingi kwa sana Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF, chini ya uenyekiti imara wa Ndugu Peniel Lyimo, Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, kwa uongozi wake thabiti wa kusimamia vizuri shughuli za TASAF.  Aidha, nampongeza Katibu Mkuu, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa usimamizi wake thabiti.  Hali kadhalika  nNawapongeza pia viongozi na watendaji katika Halmashauri zote za Tanzania Bara , Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar kwa kazi nzuri waifanyayo ya usimamizi na utekelezaji wa miradi katika awamu iliyotangulia. Bila uongozi wao thabiti, mafanikio ya Awamu zya Kwanza na Pili yangekuwa ni ndoto. Kwa namna ya pekee nawapongeza wananchi wote walioitikia wito na kuchangia kwa hali na mali kufanikisha utekelezaji wa mpango huo wa kujiletea maendeleo yao wenyewe.
Nitakuwa mchoyo wa fadhila nisipoipongeza Kamati ya Dkt. Servacius Likwelile, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, kwa kazi nzuri ya kuandaa Awamu ya Tatu ya TASAF. Kazi hiyo wameifanya vizuri na kwa umakini mkubwa wahuku akikishirikiana na Bibi Ida Manjolo na wataalamu wengine wa Benki ya Dunia.  Tunawashukuru sana.
Mabibi na Mabwana;     
Kuna msemo wa Kiswahili usemao “ukiona vyaelea, ujue vimeundwa”. Na hivi ndivyo ilivyo kwa TASAF. Siri ya mafanikio yaliyopatikana katika utekelezaji wa Awamu ya Pili ni usimamizi mzuri unaofanywa na Menejimenti ya TASAF. Hivyo napenda kuchukua nafasi hii kuipongeza Menejimenti, Mkurugenzi Mtendaji, na wafanyakazi wote wa TASAF kwa kusimamia vizuri shughuli na miradi mbalimbali iliyotekelezwa katika Awamu ya Pili.  Ni matumaini yangu kuwa mtafanya vizuri maradufu katika Awamu ya Tatu tunayoizindua leo.
Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya TASAF
Ndugu Wananchi; 
 Utekelezaji wa Awamu ya Pili ya TASAF ulikuwa na mafanikio makubwa.  Jumla ya miradi 11,572 imetekelezwa na kati ya hiyo,  miradi  4,294  ilikuwa ya huduma za jamii;  miradi 1,405 ya ujenzi  na miradi 5,875 ya makundi maalum. Miradi hiyo imegharimiwa na serikali kwa kushirikiana na washirika wake wa maendeleo. Serikali imetoa Shillingi bilioni 32.2 na Benki ya Dunia ilitupatia mkopo wa masharti nafuu wa Shilingi bilioni 322. Washirika wetu wengine walituongezea nguvu kwa kuchangia Shillingi bilioni 72. Aidha, wananchi wametoa fedha, rasilimali na nguvu kazi ambazo thamani yake inakadiriwa kuwakwa ujumla ni  zaidi ya Shilingi billioni 20.2.  
 Miradi ya Huduma
Miradi ya Huduma za Jamii imeongeza na/au kuboresha madarasa 5,485; ofisi za walimu 150;  nyumba za walimu 152;, maabara kwenye shule za sekondari 157; majengo ya utawala katika shule za sekondari 20; mabweni ya wanafunzi 163; vyoo vya wanafunzi 705; madawati 22,946, viti 5,483, meza 4,354; vituo vya afya 63; zahanati 606,  nyumba za watumishi wa zahanati 301, vyoo kwenye zahanati 339, vichomea taka 182; vituo vya maji 2,198, visima virefu 192, visima vifupi 335 na matanki ya maji 205.
Miradi ya Ujenzi
Miradi ya ujenzi, yenyewe imeongeza au kuboresha barabara za vijijini 825; mabwawa madogo 78; mifumo midogo ya umwagiliaji 289; mifumo ya kuondoa maji ya mvua barabarani mita 4,593; maghala ya kuhifadhia nafaka 113; masoko 80; makaravati 901; madaraja ya watembea kwa miguu 64; na, miradi ya mazingira 608 yenye walengwa 566,938.
Makundi Maalum
Na miradi ya makundi maalum imetoa huduma kwa yatima 32,113; wajane 15,205; wazee 17,961; watu wenye ulemavu 7,840; watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI  52,316; na vijana wasio na ajira 36,859.  Vilevile, watu 2,083 wamehamasishwa kujikinga na ugonjwa wa UKIMWI.
Mabibi na Mabwana;
Mafanikio ya utekelezaji wa Awamu ya Pili ya TASAF  hayakuishia hapo. Vikundi 1,778 vyenye wanachama 22,712 vimeundwa kupitia Mpango wa Kuweka Akiba na Kuwekeza (COMSIP ) katika Halmashauri 44 zilizopo Tanzania Bara, Unguja na Pemba. Walengwa wote wamepatiwa mafunzo ya kuendesha vikundi vyao kwa ufanisi pamoja na vifaa. Vilevile, mafunzo ya usimamizi, utekelezaji bora wa miradi na fani mbalimbali katika ngazi ya vijiji, wilaya na taifa yametolewa kwa walengwa 27,373.
Serikali kupitia TASAF imefanikiwa pia kutekeleza Programu ya Kijamii ya Uhawilishaji Fedha kwa Kaya Maskini kwa majaribio katika Wilaya za Bagamoyo, Kibaha na Chamwino. Walengwa zaidi ya 13,000 kutoka kaya 6,000 maskini na zilizo katika mazingira hatarishi zilipatiwa ruzuku ya jumla ya shillingi bilioni moja na nusu.   Kaya hizo zimejengewa uwezo na watoto sasa wanapelekwa kwenye zahanati na vituo vya afya kwa ajili ya chanjo na kufuatiliwa maendeleo yao. 
Aidha, watoto 1,638 ambao hawakuweza kwenda shule kwa sababu ya umasikini sasa wameandikishwa na wanakwenda shule. Kati ya wanafunzi hao, 392 wamefaulu kwenda shule za sekondari za kata. Vile vile wazee 4,956 wamewezeshwa kupata huduma za afya na baadhi yao wamejiunga na bima ya afya ili kupata huduma kwa urahisi na uhakika zaidi.  Kufuatia mafanikio ya haraka ya programu hii, sasa maandalizi yanafanyika ili isambazwe kwenye Halmashauri zote katika utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya TASAF.
Ndugu Wananchi;
  Inafurahisha kuona jinsi suala la jinsia lilivyozingatiwa katika utekelezaji wa programu na miradi ya TASAF.  Wanaume na wanawake walishirikishwa sawa sawa katika hatua zote za utekelezaji wa miradi yao. Idadi ya wanawake katika kamati ya mradi ilipangwa makusudi ili isipungue asilimia 50 ya jumla ya wajumbe, na idadi ya walengwa wanawake katika miradi ya ujenzi nayo isipungue asilimia 50. Bahati nzuri akina mama waliokuwa wajumbe kwenye Kamati mbalimbali wameonesha uwezo mkubwa wa uongozi. Naomba ushirikishwaji huu uendelee kuimarishwa na akina mama wajitokeze kwa wingi kushiriki katika usimamizi wa miradi ya TASAF ya Awamu ya Tatu. 
Ni wazi kuwa siri ya mafanikio ya Awamu ya Pili ya TASAF ni ushiriki mzuri wa wananchi, utayari wao wa kumiliki maendeleo yao wenyewe na moyo wa kujituma kwao pamoja na uongozi na usimamizi mzuri wa miradi katika ngazi zote.
Changamoto Katika Utekelezaji wa Awamu ya Pili
Maendeleo ya Jamii (TASAF I) kule Mwanhuzi, Wilayani Meatu, Mkoa wa Shinyanga.

Vile vile tarehe 23 Mei 2005, tulizindua Awamu ya Pili ya Mfuko huu (TASAF II ) kule Wilayani Magu, Mkoa wa Mwanza.

Leo hii ninayo furaha kubwa kuja hapa Dodoma kuzindua Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III).
            
Tunazindua Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii kwa kuwa Awamu ya Kwanza na ya Pili zimetekelezwa kwa mafanikio makubwa.  Hivyo basi, naanza kwa kutoa shukurani na pongezi zangu za dhati kwa wote walioshiriki kufanikisha Awamu mbili zilizotangulia na walioshiriki kuandaa Awamu hii ya Tatu. 
            
Naishukuru Benki ya Dunia na ninamshukuru Mkurugenzi Mwakilishi wa Benki hii kwa nchi za Tanzania, Uganda na Burundi, Bw. Philippe Dongier.  Kwa hakika Bw. Dongier anaiwakilisha vyema Benki ya Dunia ambayo siku zote inasikiliza hoja na kuzingatia vipaumbele vya vita dhidi ya umaskini vinavyowekwa na Serikali yetu.  Mfano halisi ni Mfuko huu wa Maendeleo ya Jamii - TASAF.  Kwa usikivu huo, tumebuni ubia mzuri wa maendeleo kati ya Serikali yetu, Benki ya Dunia, Wadau wengine wa Maendeleo na Wananchi.  

Napenda pia, kuwashukuru washirika wengine wa maendeleo ambao wanashiriki Awamu hii ya Tatu ya TASAF hususan Serikali ya Uingereza kupitia Idara yake ya Maendeleo ya Kimataifa (DFID),   Serikali ya Hispania na Serikali ya Watu wa Marekani kupitia Shirika lake la Maendeleo ya Kimataifa (USAID).  
            
Ninawashukuru Wataalam wa Benki ya Dunia na Washirika wengine wa Maendeleo wakiongozwa na Bibi Ida Manjolo ambao walishirikiana nasi kwa karibu katika utekelezaji wa Awamu ya Pili ya TASAF na kuandaa  Awamu ya Tatu. 
           
 Naipongeza pia Kamati ya Taifa ya Uongozi ya TASAF ambayo mwenyekiti wake ni  Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, Ndugu Peniel M. Lyimo, pamoja na Kamati ya Maandalizi ya Awamu ya Tatu ya TASAF iliyoongozwa na Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Fedha, Dkt. Servacius B. Likwelile, kwa kazi nzuri.
           
Nawapongeza Viongozi na Watendaji katika Halmashauri zote za Tanzania Bara, Afisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar na wananchi wote kwa jumla kwa usimamizi na utekelezaji wa miradi ya jamii katika awamu zote mbili zilizotangulia. Wananchi wote waliitikia kwa moyo mkunjufu na ari kubwa kupokea mawazo ya Serikali katika utekelezaji wa mpango huo wa kujiletea maendeleo yao wenyewe.
    
Naipongeza pia Menejimenti ya TASAF, ikiongozwa na  Mkurugenzi Mtendaji, Ndugu Ladislaus J. Mwamanga na wasaidizi wake.  Nina imani kuwa wataendelea kufanya kazi nzuri katika Awamu hii ya Tatu. 

Tangu mwaka 2000 TASAF imekuwa ni kichocheo katika jitihada za wananchi kujiletea maendeleo.  TASAF haina miradi; miradi ni ya wananchi. Inachokifanya TASAF ni kuwawezesha tu wananchi kutekeleza vipaumbele vyao vya maendeleo.  
Awamu ya Pili ya TASAF iligharimiwa kwa kiasi kikubwa na mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia.  Mkopo huo ni kiasi cha Shilingi 322 bilioni  sawa na Dola za Kimarekani 215 milioni. Vilevile kwa utekelezaji mzuri wa TASAF, kumekuwa na Wahisani na Miradi mingine kupitishia fedha TASAF zenye jumla ya shilling 72 bilioni sawa na Dola za Kimarekani 45 milioni. Mchango wa Serikali yetu ulikuwa ni Shilingi 32.2 bilioni, na wananchi walichangia fedha rasilimali na nguvu kazi ambazo thamani yake ilifikia zaidi ya Shilingi 20.2 bilioni.
Ndugu Wananchi
Ushiriki wa wananchi, utayari wao wa kumiliki maendeleo yao na kujituma kwao pamoja na uongozi na usimamizi mzuri wa kitaifa na halmashauri husika ndio msingi wa mafanikio ya Awamu ya Pili ya TASAF.

Mafanikio hayo ni pamoja na :-
1.Jumla ya miradi 11,572 ilipitishwa na kupewa fedha; miradi 4,294 ikiwa ya Huduma za Jamii, miradi 1,405 ya Ujenzi  na miradi 5,875 ni ya Makundi Maalum.
2.Miradi ya Huduma za Jamii imeongeza na/au kuboresha madarasa 5,485, ofisi za walimu 150, nyumba za walimu 152, maabara kwenye shule za sekondari 157, majengo ya utawala katika shule za sekondari 209, mabweni ya wanafunzi 163, vyoo vya wanafunzi 705, madawati 22,946, viti 5,483, meza 4,354; zahanati 606, vituo vya afya 63, nyumba za watumishi wa zahanati 301, vyoo kwenye zahanati 339, vichomea taka 182; vituo vya maji 2,198, visima virefu 192, visima vifupi 335 na matanki ya maji 205.


3.Miradi ya ujenzi imeongeza au kuboresha barabara za vijijini 825, mabwawa madogo 78, na mifumo ya kuondoa maji ya mvua barabarani mita 4,593, maghala ya kuhifadhia nafaka 113, masoko 80, mifumo midogo ya umwagiliaji 289, makaravati 901, miradi ya mazingira 608 yenye walengwa 566,938 na madaraja ya watembea kwa miguu 64.
4.Miradi ya makundi maalum imetoa huduma kwa yatima 32,113, wajane 15,205, wazee 17,961, watu wenye ulemavu 7,840, watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI 52,316 na vijana wasio na ajira 36,859.  Vilevile, uhamasishaji juu ya kudhibiti UKIMWI umetolewa kwa watu 2,083.

5.Vikundi 1,778 vyenye wanachama 22,712 vimeundwa kupitia Mpango wa Kuweka Akiba na Kuwekeza (COMSIP ) katika Halmashauri 44 na Unguja na PembaWalengwa wote wamepatiwa mafunzo ya kuendesha  vikundi vyao kwa ufanisi pamoja na vifaa. 

6.Mafunzo ya usimamizi, utekelezaji bora wa miradi na fani mbalimbali katika ngazi ya vijiji, wilaya na taifa yametolewa kwa walengwa mbalimbali 27,373.

Ndugu wananchi,
7.Serikali pia kupitia Awamu ya Pili ya TASAF imefanikiwa kutekeleza Programu ya Kijamii ya Uhawilishaji Fedha kwa Kaya Maskini kwa majaribio katika Wilaya za Bagamoyo, Kibaha na Chamwino. Walengwa zaidi ya 13,000 kutoka kaya 6,000 maskini na zilizo katika mazingira hatarishi zilipatiwa ruzuku ya jumla ya shillingi bilioni moja na nusu (Sh. 1,500,000,000).   Kaya hizo zimejengewa uwezo na watoto ambao ndiyo walengwa wanapelekwa kwenye zahanati na vituo vya afya kwa ajili ya chanjo na kufuatilia maendeleo yao. 

8.Aidha, watoto 1,638 ambao hawakuweza kwenda shule sababu ya umasikini sasa wameandikishwa na wanakwenda shule. Kati ya wanafunzi hao 392 wamefaulu kwenda shule za sekondari za kata. Vile vile wazee 4,956 ambao ni walengwa wamewezeshwa kupata huduma za afya. Pia  Kaya za walengwa zimejiunga na mpango wa bima ya afya ili kupata huduma kwa urahisi na uhakika zaidi.  

9.Programu hii imekuwa na mchango mkubwa katika kuboresha hali ya maisha ya kaya za walengwa kwa muda mfupi sana. Mafanikio yake yamefanya sasa programu hii kusambazwa kwenye Halmashauri zote katika utekelezaji wa TASAF Awamu ya Tatu.  Haya yote yasingewezekana bila ninyi wananchi kukubali kwa pamoja kushiriki katika kurekebisha hali ya uchumi wetu, kwa kuwa muhimili mkuuwa maendeleo katika ngazi ya jamii.  
Ndugu wananchi,
Kwa kuwa TASAF imepanua uwigo wa kuwafikia walengwa masikini katika makundi mbalimbali ndani ya Tanzania Bara na Zanzibar na uzoevu wao wa zaidi ya miaka kumi na mbili; ni dhahili kuwa ni chombo pekee cha serikali chenye uwezo wa kutekeleza vizuri Mpango wa Kitaifa wa Kinga ya Jamii ( National Social Protection Framework) 

Awamu ya Pili ya TASAF imeimarisha uwajibikaji katika ngazi zote kwa kuhakikisha kuwa fedha zote zilizotengwa kwa ajili ya utekelezaji wa shughuli mbalimbali zinatolewa taarifa na wadau wote wanajulishwa mapato na matumizi yake. Kamati za usimamizi wa miradi ziliwajibika kutoa taarifa za utekelezaji hatua kwa hatua na matumizi ya fedha. 

Suala la jinsia katika utekelezaji wa miradi lilizingatiwa, na kuonekana wazi kuwa ni jambo la haki na la manufaa kila palipokuwa na mradi unaochangiwa na TASAF. Wanaume na wanawake walishirikishwa sawa sawa katika hatua zote za utekelezaji wa miradi yao. Idadi ya wanawake katika kamati ya mradi ilipangwa kwa makusudi isipungue asilimia 50 ya jumla ya wajumbe, na idadi ya walengwa wanawake katika miradi ya ujenzi nayo isipungue asilimia 50. Lengo ni kuhakikisha kuwa kipato kisichopungua asilimia 50 kinaelekezwa kwa walengwa ambao ni wanawake.  Matumaini yangu ni kuwa uwezo waliouonyesha wanawake waliokuwa kwenye kamati hizi utawasukuma wengi wao kuomba uongozi katika ngazi mbalimbali.


Ndugu wananchi;
Pamoja na mafanikio hayo ya kutia moyo, Wakati wa utekelezaji wa Awamu ya Pili ulikabiliwa na changamoto ya TASAF kumekuwepo na changamoto mbalilmbali.  Changamoto hizo ni pamoja na uhaba wa fedha kutokutosheleza kukidhi wezo wa Mfuko kutokidhi mmahitaji ya wananchi; uwezo mdogo wa kusimamia miradi katika ngazi mbalimbali za uongozi; na ya wananchi ambayo ni mengi, ukosefu wa huduma kwenye baadhi ya vituo vya kutolea huduma kama zahuhaba wa watumishi katika vituo vya kutoa huduma. Bahati nzuri serikali na uongozi wa TASAF unazitambua changamoto hizo na tumejipanga vizuri kukabiliana nazo katika Awamu hii ya Tatu tunayoizindua leo.
Awamu ya Tatu ya TASAF
anati, vituo vya afya na masoko vilivyotokana na miradi kutokana na sababu mbalimbali kama vile uhaba wa watumishi.  

Changamoto nyingine ni pamoja uhaba wa fedha za utekelezaji wa shughuli za kujenga uwezo, wigo mdogo wa utekelezaji wa jitihada nyingine, kama vile Mpango wa Jamii wa Uhawilishaji Fedha kwa Kaya Maskini, Mpango wa Jamii wa Kuweka Akiba na Kuwekeza, uansishwaji wa Taasisi za Maendeleo ya Jamii katika sehemu za mijini. 

Kadhalika ilijitokeza changamoto ambapo baadhi ya wanasiasa walipotosha dhana ya kuanzishwa kwa TASAF na pia kutokuwepo mfumo wa uendelevu thabiti wa kutekeleza TASAF kwa kutegemea rasilimali za ndani. 

Mabibi na Mabwana;Ndugu wananchi
Kufuatia mafanikio katika utekelezaji wa Awamu mbili zilizotangulia na pia katika kukabiliana na changamoto zake, Serikali imeamua kuanzisha Awamu ya Tatu ya TASAF itatekelezwa kwa miaka kumi, katika vipindi viwili vya miaka mitano mitano. ambapo Muondo wake umezingatia kupata ufumbuzi wa chanamoto zilizopatikana na hivyo  ambayo itatekelezwa katika kipindi cha miaka kumi nchi nzima kwa Awamu mbili za miaka mitano mitano. 
Tunategemea  
Awamu hii ya Tatu ya TASAF itatoa mchango mkubwa katika kufikia nalenga kuchangania kufikiwa malengo yetu yaliyomo kwenye ya D Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, Mkakati wa Pili wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA II) na Mkakati wa Pili wa Kukuza Uchumi Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Zanzibar (MKUZA II) na Mpango wa Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mita. Tutaweka mkazo zaidi katika miradi ya huduma za elimu, afya na maji nay a kuondoa umaskini wa kipato. no kwa kuwekeza katika kuendeleza rasilimali watu miongoni mwa kaya maskini na zilizo katika mazingira hatarishi.  Kupitia utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya TASAF tunatarajiainatarajiwa  kuwa kaya nyingimaskini maskini zitapiga hatua na kutoka  kwenyekuanza kutoka katika  umaskini namaisha ya utegemezi. hatimaye kuwa na mchango katika kukuza uchumi na kuondokana na utegemezi. 
Ili kutekeleza miradi ya Awamu ya Tatu ya TASAF, jumla ya Shilingi bilioni 408 zitahitajika. Fedha hizo zitatolewa na serikali yetu, Benki ya Dunia na washirika wengine wa maendeleo. Serikali itatoa Shillingi bilioni 45; Benki ya Dunia itachangia Shillingi bilioni 330; Hispania itatoa Shillingi bilioni 9; Uingereza Shillingi bilioni 24; na Marekani Shillingi bilioni 1.4. Kama ilivyokuwa kwa Awamu zilizotangulia, tunawategemea sana wananchi kutuunga mkono na kuchangia kwa hali na mali. Mafanikio ya Awamu hii yatategemea sana mchango wa wananchi katika maeneo husika.
Ahadi na Wito kwa Wananchi
Ndugu wananchi;
Tunapenda kuahidi kuwa tutaendelea kushirikiana na wananchi wote ambao wanaonesha dhamira ya dhati ya kupambana na umaskini na kujiongezea 
Kwa ushirikiano wenu wananchi, TASAF imetekelezwa vizuri sana na matunda yake yapo wazi, na kwa vile mmeendelea kuiunga mkono Serikali yenu ya CCM katika kutekeleza Mwelekeo wa Sera zake za Miaka mitano (2010-2015) zinazohimiza mageuzi ya kiuchumi na uwezeshaji wananchi, serikali imetenga fedha  tena na kupata mkopo wa masharti nafuu kutoka Benki ya Dunia na washirika wengine wa maendeleo ili kutekeleza Awamu ya Tatu ya TASAF.

Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Dunia iliridhia na kupitisha utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya TASAF tarehe 29 Machi, 2012.  Mkataba kati ya Benki ya Dunia na  Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ulisainiwa tarehe 15 Juni 2012. Na idhini ya kuanza kutumia fedha hizo tayari imeshatolewa.

Awamu ya Tatu ya TASAF inatarajiwa kugharimu Shilingi 408 Bilioni sawa na Dola za Kimarekani 272 Milioni kwa mchanganuo ufuatao:
1.Benki ya Dunia itachangia shilingi 330 bilioni (USD 220 milioni), 
2.Serikali ya Hispania itachangia Shilingi 9 bilioni (USD 6 milioni)
3.Serikali ya Uingereza kwa kupitia Idara ya Serikali ya Uingereza ya Maendeleo ya Kimataifa(DFID) itachangia Shilingi 24 bilioni (USD 16 milioni)
4.Serikali ya Watu wa Marekani kupitia Shirika la Marekani la Maendeleo ya Kimataifa (USAID)  itachangia Shillingi 1.44 bilioni ( USD 900,000)
5.Serikali ya Tanzania itachangia sh.45 bilioni (USD 30 milioni)
Ndugu wananchi
Utekelezaji wa Awamu ya Tatu ya TASAF unategemewa kuwa na changamoto zifuatazo:
1.Upatikanaji wa raslimali fedha za kukidhi mahitaji halisi ya walengwa. Jitihada za kupata rasilimali zaidi ziendelee na Wadau wa Maendeleo watoe ushirikiano zaidi hasa wale ambao wameonyesha nia ya kushiriki katika kuchangia mfuko huu.
2.Kujenga uwezo mapema wa kusimamia na kutekeleza kwa wakati uhawilishaji wa fedha kwa walengwa.  Mpango wa kujenga uwezo wa watekelezaji katika ngazi mbalimbali upewe kipaumbele. Ufuatiliaji na tathmini vifanyike ili kubaini mapungufu mapema iwezekanavyo.
3.Uwezo wa kusimamia utekelezaji miradi kwa ufanisi na kwa wakati. Ngazi zote zinazohusika na utekelezaji zishiriki kikamilifu katika kuhakikisha usimamizi wa utekelezaji unafanyika ipasavyo. Aidha, utekelezaji ufanyike kwa awamu kuzingatia uwezo unavyojengwa.
4.Kusimamia uendelevu wa rasilimali na vituo vya kutolea huduma vilivyotokana na miradi iliyotekelezwa na wananchi. Wataalamu kutoka halmashauri husika na Viongozi katika maeneo ya utekelezaji wawezesha jamii kuwa na mipango endelevu ya uendeshaji.
5.Usimamizi wa fedha zitakazotolewa kutekeleza miradi inayochangiwa na TASAF utahitaji uwepo wa udhibiti mkubwa katika ngazi zote.  Kazi hiyo nayo ifanywe kuanzia sasa na kwa kipindi chote cha utekelezaji.
Ndugu wananchi,
Leo tunapozindua Awamu ya Tatu ya TASAF napenda tujikumbushe kuwa historia yetu ya vita dhidi ya umaskini imetufundisha mambo kadhaa:
Kwanza, sera nzuri, mipango mizuri na nia njema peke yake havileti 
maendeleo.
Pili, fedha za Serikali, mikopo au wahisani peke yake hazileti 
maendeleo.

Tatu, ipo tofauti kubwa kati ya kutamani maendeleo na kuwa tayari 
kutoka jasho kutafuta maendeleo.
Baada ya miaka 50 ya Uhuru sasa nadhani tumeelewa kunahitajika nini ili maendeleo yaje kwa kasi ya kutosha kuweza kupunguza na hatimaye kuondoa umaskini kabisa.
Hatua ya kwanza ya maendeleo ni mtu kutoridhika na hali duni ya maisha yake; ni kujenga tamaa na wivu wa maendeleo na kuchukia hali ya umaskini.
Hatua ya pili ni mtu kuamua kwa dhati kutafuta maendeleo kwa jasho 
lake, na inapobidi kwa kushirikiana na wenzake wanaochukia umaskini kama yeye.
Hatua ya tatu ni mtu kupima uwezo alionao – uwezo wa fedha na wa mali nyingine; uwezo wa akili na maarifa; na uwezo wa nguvu za kufanya kazi na kubuni mbinu za kutumia ili kuboresha hali yake ya maisha na hali ya jamii yake kwa ujumla.
Hatua ya nne ni kutekeleza kwa kadri ya uwezo wake mbinu za maendeleo alizozibuni, au zilizobuniwa na jamii yake.
Hatua ya tano ni kuomba msaada kwa yale mambo yaliyo nje ya uwezo wake, ikiwemo msaada wa fedha, msaada wa vifaa, au msaada wa elimu na utaalamu.
Mfuko huu wa Kuongeza Uwezo wa Wananchi katika Maendeleo ni jitihada nyingine ya Serikali kuwasaidia wale wananchi ambao wamepitia hatua zote hizo za kutafuta maendeleo, yaani tayari wameonyesha chuki yao dhidi ya umaskini, wameamua kwa dhati kuondokana na umaskini kwa kuongeza kkipato chao. Kipato cha mtu kinapoongezeka watoto wake watahudhuria masomo na kupata huduma bora za afya. Wazee na akina mama nao watapata huduma bora za afya. Lakini kipato hakiwezi kuongezeka kama mtu hataki kufanya kazi, hataki maendeleo, na hataki kujishughulisha na kitu chochote. Maisha bora kwa kila mMtanzania yatapatikana kama tutafanya kazi kwa bidii na maarifa.  Inawezekana, kila mtu atimize wajibu wake. 
 kaya ili watoto wahudhurie masomo na kwenda kliniki kupata chanjo na huduma zingine za afya.  Vile vile ongezeko la kipato litawezesha akina mama wajawazito na wazee kupata huduma zote muhimu za afya.

Hivyo ndugu zangu natoa wito kwa wananchi wote watumie vizuri fursa hii murua ya TASAF. Tushirikiane na uongozi wa TASAF kubuni miradi itakayotuletea maendeleo ya haraka, miradi itakayoboresha huduma za jamii. Tushirikiane nao kusimamia utekelezaji wa miradi hiyo. Tuhakikishe kuwa tunafuata maelekezo ya wataalam  na viongozi wetu katika ngazi mbalimbali. Tuwafichue wabadhirifu wa fedha za miradi ya TASAF na wale wote wanaotumia vibaya rasilimali za miradi. Daima tukumbuke kuwa miradi hii ni kwa ajili yetu sisi pamoja na watoto wetu, ndugu zetu na jamaa zetu. Tukifanya hivi nina imani tutakuwa na msingi imara wa kujenga taifa linaloendelea na hatimaye kushinda vita dhidi ya adui watatu wa maendeleo: umaskini, njaa na magonjwa. 
Rai kwa Washirika wa Maendeleo na Viongozi wa TASAF
Mabibi na Mabwana;
Natumaini washirika wetu wa maendeleo wataendelea kuunga mkono juhudi zetu hizi za kuondoa maadui watatu wa maendeleo. Wamekuwa wakifanya hivyo tangu tulipoanzisha Mfuko huu wa TASAF na nina imani wataendelea. Msaada wao utasaidia sana kufikia malengo yetu tuliyojiwekea katika utekelezaji wa Awamu hii. 
Nawaomba pia viongozi wa TASAF, Kamati ya Taifa ya Uongozi, Menejimenti na Mkurugenzi Mtendaji waongeze ufanisi na maarifa katika utendaji wao. Waongeze usimamizi wa fedha na rasilimali, wajenge uwezo wa kusimamia utekelezaji wa miradi katika ngazi mbalimbali, na wabuni vyanzo vingine vya kupata fedha za kuendeleza miradi. Naamini wataweza.

Mwisho
Mheshimiwa Waziri;
Wageni waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Kabla ya kumaliza hotuba yangu naomba nitoe shukrani za dhati kwa Mhe. Benjamin William Mkapa, Rais wa Awamu ya Tatu kwa kubuni wazo hili jema ambalo manufaa yake tunayaona.  Baada ya kusema hayo, sasa nipo tayari kufanya kazi iliyonileta hapa Nazindua Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii kwa matumaini makubwa kuwawamba  sasa Watanzania sasa tumeupata ufunguo wa maendeleo yetu sote. Napenda kutamka kwamba Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii, (TASAF) umezinduliwa rasmi leo. Nawatakia kila la heri na mafanikio katika utekelezaji wake.

Asanteni sana kwa kunisikiliza.kwa kutumia fursa ambazo mageuzi ya uchumi, na usimamizi bora wa uchumi, umeweka mbele yetu.

Kwa pamoja tutafanya mengi. Na kwa mradi huu wa TASAF, ukichanganywa na miradi mingine, na utaratibu huu wa kushirikisha wananchi katika shughuli za kupunguza umasikini, ninaamini Watanzania wote tutakuwa na msingi imara wa kujenga taifa linaloendelea na hatimaye kushinda vita dhidi ya umaskini.  

Na sasa natangaza kuwa nimezindua rasmi Awamu ya Tatu ya Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF III).

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.

No comments:

Post a Comment