Mwanafunzi Khalfan Mkubwa Haji (20) kutoka Zanzibar mshindi wa pili
Mwanafunzi wa kuhifadhi Qur'aan kupitia Tashjii Ali Khamis Mohammed (14)
Murshid Juma Nsengimana (21) wa Rwanda akishiriki mashindano.
Abass Suleiman Mswahili (18) kutoka D R Congo
Mukhtar Abubakar Abdi (14) kutoka Somalia akishiriki mashindano ya Qur'aan kuhifadhi juzuu 30.
Mukhtar Abubakar Abdi (14) kutoka Somalia akishiriki mashindano ya Qur'aan kuhifadhi juzuu 30.
Mwanafunzi Amour Yussuf Mash (20) mshindi wa mashindano hayo ya kimataifa akisoma moja ya aya aliyopewa katika mashindano hayo.
Mwanafunzi kutoka Burundi Nzisabira Mashaka Juma ( 20 )
Hawa ndio watoaji aya ambayo husomwa kidogo tu na kutakiwa mshiriki kuendelea.
Majaji wakiwasikiliza wananafunzi wanashiriki Mashindano ya Qur'aan ambapo kila mmoja alikuwa akifuatilia kitu tofauti kama inavyoonekana kuna wanaofuatilia Makhaarij tu yaani matoleo ya herufi, wengine Tajweed yaani hukumu za kuisoma Qur'aan kwa Tajweed na wengine uwezo wa kuhifadhi.
Mgeni Rasmin, Naibu Kadhi wa Zanzibar, Sheikh Khamis Haji Khamis, akiwa na Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Quran Zanzibar Suleiman Omar (Maalim Sule) na Kadhi Mstaafu Sheikh Habibu Ali Kombo wakifuatilia mashindano hayo yaliofanyika Masjid Afraa Bint Issa Kidongo chekundu Zanzibar
Waumini wa Dini ya Kiislam wakifuatilia mashindano ya kuhifadhi Quran juzuu 30 ya kimataifa
Mwenyekiti wa Jumuiya ya Kuhifadhisha Qur'aan Zanzibar, Suleiman Omar (Maalim Sule) akitowa mukhtasari wa mashindano hayo ya Kimataifa ya Quran yaliofanyika Masjid Afraa Bint Issa Kidongo chekundu Zanzibar.
Naibu Kadhi wa Zanzibar, Sheikh Khamis Haji Khamis akitowa nasaha zake kwa washiriki wa Mashindano hayo na Waumini wa Kiislam baada ya kumaliza mashindano hayo ya Kimataifa ya Kuhifadhi Qur'aan.
Kiongozi wa Majaji akitowa matokeo ya washindi wa mashindano hayo
Naibu Kadhi wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji Khamis akimkabidhi zawadi mshindi wa kwanza wa mashindanob hayo Amour Yussuf Mash kwa kupata point 99.0. na kupata shilingi milioni moja taslim na set ya TV.
Mshindi wa Pili kwa pointi 97.00 Khalfan Mkubwa Haji, akipokea zawadi yake ya birika la maji moto na fedha taslim shillingi laki saba na hamsini.
No comments:
Post a Comment