.

.

.

.

Tuesday, August 28, 2012

MAMBO YA LONDON CARNIVAL



Carnival 

Mh Balozi Kallaghe wa Tanzania nchini Uingereza Peter Kallahe(Kulia)akiwa  na Frank kwenye Notting Hill Carnival.
Freddy Macha akipiga Filimbi.
 Freddy Macha na Frank Katika Notting Hill Carnival.
Freddy Macha na Wadau wakisherekea Carnival.
 Polisi katika pozi.
 Ni furaha na shangwe tu kwa kila mtu.
Watu wakumwaga.
---
Salaam,
Urban Pulse Creative na Freddy Macha wanakuletea taswira ya Notting Hill Carnival iliyofanyika jana tarehe 27.8.12.  Kihistoria sherehe hii ilifanywa siku 40 kabla ya Pasaka kipindi kinachoitwa LENT ( “Kwaresima“ )ambapo waumini wa Kikristo hujinyima, husali, hutoa sadaka, huomba msamaha, huungama makosa , kuwa karibu na  Mwenyezi Mungu kwa kufunga (kama wafanyavyo Wayahudi na pia Waislamu kabla ya Idd El Fitri). Carnival hushereherekewa kidesturi mwezi wa pili na watatu (Brazil, Ujerumani, nk) lakini nchi mbalimbali ( mathalan  Uingereza, Japan, Cape Verde nk) zimegeuza tarehe kufuatana na tamaduni  au matakwa yao. London ni Jumapili na Jumatatu ya mwisho wa mwezi Agosti ambapo  hamna kazi (huitwa Bank Holiday). 
Carnival ni neno lenye asili ya Kilatini  "Carne Vale"  –maana yake  “Kwaheri” (Vale) “Nyama” (Carne)

Baadhi ya nchi maarufu kwa Carnival

1.     Brazil – Rio ni Samba na Bahia ni siku tano za muziki juu ya malori makubwa- Feb na March
2.     Trinidad na Tobago- Mwezi  Feb na March kabla ya Pasaka, athiri sana Carnival ya London kwa muziki wake wa Soca na ngoma za chuma („steel pans“
3.     Nchi za Kiafrika zenye asilia ya Kireno- husheherekea Carnival, Maputo, Luanda na visiwa vya Cape Verde- ambapo Carnival inaitwa “Mindelo“....(mji mkuu wa Cape Verde). Carnival ya Mindelo ni maarufu na kubwa kuliko zote Afrika.


4.     Asakusa, Japan. Carnival la Japan lenye mahadhi ya Samba na Brazil kila mwaka mwisho wa mwezi wa Agosti. Vutia watu laki moja.


Muasisi mkuu wa Carnival ya London ni Claudia Jones- mwanamke mwenye asilia ya Trinidad aliyehamia Uingereza mwaka 1955. Alikuwa mwanahabari aliyepigania haki za watu weusi. Mwaka 1959 alianzisha Carnival ya kwanza katika kitongoji cha St Pacrais. Sherehe hii ilivutia sana Habari na ilitangazwa katika BBC. Claudia Jones alifariki mwaka 1964 kutokana na maradhi ya moyo na kifua kikuu. Amezikwa kando ya kaburi la Karl Marx, High Gate, London kaskazini.

Asanteni,

Urban Pulse wakishirikiana na Freddy macha

No comments:

Post a Comment