.

.

.

.

Saturday, September 08, 2012

NOELA MICHAEL AWA REDDS MISS ILALA 2012Redd's Miss Ilala 2012, Noela Michael
Redd's Miss Ilala 2012, Noela Michael akiwa na wa pili Magdalena Munisi kulia na mshindi wa tatu Mary Chizi kushoto, mara baada ya kutangazwa kuwa washindi wa shindano la Redd's Miss Ilala.

Redd's Miss Ilala 2012, Noela Michael
Redd's Miss Ilala 2012, Noela Michael akiwa na wa pili Magdalena Munisi kulia na mshindi wa tatu Mary Chizi kushoto, mara baada ya kutangazwa kuwa washindi wa shindano la Redd's Miss Ilala.

Picha zote kwa hisani ya Intellectuals Communications Limited
DAR ES SALAAM, Tanzania

MREMBO Noela Michael, 19, kutoka Tabata usiku wa kuamkia leo alitwaa taji la Redd’s Miss Ilala 2012, kinyang’anyiro kilichofanyika kwenye Ukumbi wa Nyumbani Lounge, Namanga, Dar es Salaam.

Noela ambaye amemaliza kidato cha sita na sasa anajiandaa kuingia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), aling’ara katika usiku huo, ingawa alipata upinzani mkali kutoka kwa Magdalena Roy Munisi, 21, ambaye ni Redd’s Miss Dar City Centre, aliyeshika nafasi ya pili.

Kimwana Mary Chizi alikuwa ana usiku mzuri pia jana, kwani pamoja na kutwaa taji la Mrembo Mwenye Kipaji Zaidi na kupata Sh. 500,000, pia alishika nafasi ya tatu na kuungana na wenzake hao wawili kushiriki Redd’s  Miss Tanzania kutokea kanda ya Ilala.

Katika shindano  hilo liliosindikizwa na burudani ya wasanii Wanne Star, Chegge, T Africa kutoka Temeke, Spencer Group na Machozi Band, mshindi wa nne alikuwa Mecktilda Martin, 19, akitokea Redd’s Miss Dar City Centre na wa tano alikuwa mrembo Elizabeth Pretty, 21 kutoka Ukonga.

Kwa ushindi huo, Noela anayerithi taji la Salha Israel ambaye pia ni Miss Tanzania 2011, alijipatia kitita cha Sh. Milioni 1.5, wakati Magalenda alipata Milioni 1.2 na Merry 700,000, huku Mecktilda na Elizabeth kila mmoja akipata sh. 400,000.

Washiriki wengine ni Suzan Deodatus, Whitness Michael, Stella Moris, Wilmina Mvungi, Zawadi Mwambe, Rehema Said, Diana Simon, Amina Sangwe na Phillios Lemi, ambao kila mmoja alipata Sh. 200,000. Zawadi zote zinatarajiwa kutolewa katika ukumbi wa Nyumbani Lounge, sambamba na pati maalum.

Noela sasa anakabiliwa na changamoto si tu ya kutetea tu taji la Redd’s Miss Ilala, bali kuendeleza rekodi nzuri ya kanda hiyo katika Redd’s Miss Tanzania, iliyowekwa na akina Hoyce Temu, Jacqueline Ntuyabaliwe, Angela Damas na Salha Israel.

No comments:

Post a Comment