.

.

.

.

Wednesday, October 17, 2012

ALICE BAGENZI ALONGA KUHUSU PICHA ZAKEMWIGIZAJI nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Alice Bagenzi 'Rayuu' ameshitushwa na picha zake za nusu utupu zilizozagaa katika mitandao ya kijamii. 

Msanii huyo ambaye yupo katika tasnia kuanzia kundi la Kaole Sanaa Group amekiri kwa kusema kuwa kweli hizo picha ni zake na alijipiga kwa kutumia simu yake ya mkononi. 

Picha hizo kweli ni zangu na nilijipiga kwa kutumia simu yangu ya mkononi pia niwahi kuwarushia baadhi ya rafiki zangu wa karibu, lakini si kwa maana ya kuzirusha hewani katika mitandao ya kijamii, siwezi kumhisi mtu yeyote kama kanifanyia hivyo kwani simu niliyotumia kupigia picha hizo ilipotea sasa inanichanganya sana kujua zimefikaje huko,alisema Rayuu. 

Picha za msanii huyo za nusu utupu zimezagaa katika kurasa za Facebook na twitter akiwa kalala katika kitanda na kuonyesha sehemu yake ya mwili ikiwa na alama za michoro mgongoni.

No comments:

Post a Comment