.

.

.

.

Sunday, November 18, 2012

FRED MTOI WA BBC AFARIKI DUNIAFredd Mtoi
BBC inasikitika kutangaza kifo cha mtangazaji mwenzetu Fred Mtoi ambaye alifariki Ijumaa usiku mjini London.

Fred alianza kazi ya utangazaji katika Radio Tanzania kabla ya kuja Ulaya kwa mafunzo.

Amekuwa akifanya kazi huku akiendelea na masomo ya shahada ya pili ya masters kwenye digital media katika chuo kikuu kimoja cha London.

Alishiriki katika vipindi muhimu na vilivyopata sifa hasa vya sanaa, utamaduni na jamii kutokana na kuwafahamu wakaazi wengi wa London hasa wenye asili ya Afrika Mashariki.

Alishiriki pia katika matangazo ya kawaida ya habari ya Idhaa ya Kiswahili ya BBC.

Wenzake katika Idhaa ya Kiswahili ya BBC wanamkumbuka Fred kuwa mtu mwema, mpole, mchangamfu na anayepatana na wote, na ambaye alikuwa mtangazaji tulivu na akishikilia kazi lazima ahakikishe kuwa ameimaliza vema iwezekanavyo.

Matayarisho yanafanywa kusafirisha mwili wake hadi Tanzania.

1 comment:

  1. FREDRICK MTOI!!! Tunasikitishwa sana na kifo cha Mwanasheria mwenzetu aliyechipukia katika tasnia ya habari na kuwa mzuri pande zote na kwa jamii. Naipa pole sana BBC, familia yake na wanadarasa wenzake LLB UDSM 2000. Mungu aipumzishe roho yake pema mbinguni, Amina. Gemini S. Mushy

    ReplyDelete