.

.

.

.

Friday, February 15, 2013

GOLDIE HARVEY (WA PREZZO) AFARIKI DUNIA


Taarifa Kupitia mitandao mbalimbali ya Nigeria inaendelea kusikitika kufuatia  kifo cha aliyekuwa mwakilishi wa Nigeria katika shindano la Big Brother Afrika 2012,Goldie harvey, na mchumba wa rapa kutoka Kenya Prezzo. Habari zinaendelea kupokelewa kwa hisia tofauti huku wengine wakiwa bado hawaamini kama kweli Goldie amefariki lakini ukweli ni kwamba mitandao yote ya nchini Nigeira iimedhibitisha kifo hicho. Hii ni taarifa rasmi kutoka katika label yake Kennis Music kuhusiana na kifo chake. kwa niaba ya Kennis Music, nasikitika kuthibitisha rasmi kifo cha ghafla na kushtua cha pop star wa Nigeria Goldie Harvey. "Goldie, 31, amefariki alhamis baada ya kulalamika kupatwa na maumivu makali ya kichwa katika jumba lake lililopo park view, muda mfupi baada ya kurejea kutoka marekalani, alipoenda kushuhudia tuzo za Grammy. aliwahishwa katika hospitali anayotibiwa Reddington, Victoria Island, Lagos, ambapo madactari walisema amefariki baada tu ya kufika". mwili wa marehem Goldie, umeshapelekwa katika mochwari ya Lagos University Teaching Hospital iliyoko Ikeja, Lagos. Goldie aliiwakilisha Nigeria katika Big Brother Star Game 2012. Juhudi zake za hivi karibuni, ni pamoja na single tatu kutoka katika album yake ya nne iliyokuwa inafata "African Invasion", "skibo", "Miliki" na "Got to have it" ambazo kwa sasa zinapata kuchezwa sana katika vituo mbali mbali vya redio na tv Africa. Mipango ya mazishi itatangazwa na familia yake..
" Mungu ailaze roho ya marehem mahala pema peponi, Amen

1 comment:

  1. A fastest growing IT services provider company provides their specialized website design and web development services in London UK.
    We also offer logo design, b2b portal development and internet marketing services to make their business
    successful one and in order to derive them critical output. "cheap web design"

    ReplyDelete