.

.

.

.

Sunday, February 17, 2013

PADRI WA KANISA KATOLIKI AUWAWA ZANZIBAR


TAARIFA ILIYOIFIKIA GLOBU YA JAMII HIVI PUNDE TOKA VISIWANI ZANZIBAR,INATUHABARISHA KUWA PADRI EVERIST MUSHI (PICHANI) WA KANISA KATOLIKI HUKO ZANZIBAR,AMEPIGWA RISASI YA KICHWA NA WATU WASIOJULIKANA NA KUFARIKI PAPO HAPO ASUBUHI HII WAKATI AKIELEKEA KWENYE IBADA KATIKA KANISA LA MTONI,ZANZIBAR.

SABABU ZA KUPIGWA RISASI KWA PADRI HUYO BADO HAZIJAFAHAMIKA MPAKA SASA. 

MASHUHUDA WA TUKIO HILO WANASEMA KUWA WATU HAO WALIOFANYA TUKIO HILO WALIKUWA NI WAWILI NA WALIKUWA WAMEPAKIZANA KWENYE PIKIPIKI AINA YA VESPA WAKATI PADRI HUYO ALIKUWA KWENYE GARI LAKE AMBALO BAADA YA KUTOKEA KWA TUKIO HILO NALO LILIACHA NJIA NA KWENDA KUGONGA NYUMBA MOJA ILIYOKUWA JIRANI 



KWA HISANI YA MICHUZI BLOG





Raisi Kikwete Atoa Tamko

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa ya kuuawa kwa Padri Evarist Mushi wa Parokia ya Minara Miwili ya Kanisa Katoliki mjini Zanzibar, mauaji yaliyotokea Zanzibar.
Rais Kikwete anawapa pole nyingi na rambirambi za dhati ya moyo wangu Baba Askofu Augustino Shayo wa Jimbo Katoliki, Zanzibar, maaskofu wote nchini na waumini wote wa Parokia ya Minara Miwili kwa msiba huo mkubwa uliowakuta.
Rais kikwete amemwambia Baba Askofu Shayo. ”Napenda kuwahakikishia kuwa tupo pamoja katika kuomboleza kifo cha Mpendwa Marehemu Padri Evarist Mushin a kuwa msiba huu ni wa kwetu sote.”
Ameongeza Rais Kikwete: “Nimeligiza Jeshi la Polisi nchini kukusanya nguvu zake zote na maarifa yake yote kuhakikisha kuwa uchunguzi wa kina na wa haraka sana unafanyika ili kubaini mhusika ama wahusika na kuwakamata ili kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.”
“Aidha, nimewaagiza Jeshi la Polisi washirikiane na vyombo vingine vya Usalama nchini na mashirika ya upepelezi ya nchi rafiki katika kufanya uchunguzi wa mauaji haya.”
Amesisitiza Rais Kikwete: “Nataka ukweli wake ujulikane ili kama kuna jambo lolote zaidi liweze kushughulikiwa na kukata mzizi wa fitina.”
Vile vile, Rais Kikwete amewataka waumini wa Kanisa katoliki na wananchi wote kuwa watulivu wakati Serikali inashughulikia suala hili na kuwa hakuna mtu wala watu ama kikundi cha watu kitachoruhusiwa kuvuruga amani ya nchi yetu.




































No comments:

Post a Comment