BREAKING NEWS ............
Leo kulikuwa na uzinduzi wa Parokia mpya ya Olasit mjini Arusha. Mgeni rasmi alikuwa Mwakilishi wa Papa toka Vatican. Kulikuwa na wageni wengi waliambatana na mwakilishi wa papa, wakiwemo maaskofu, mapadre na watawa kutoka mataifa mbalimbali.
Mtoto mmoja ameeleza kuwa aliona watu waliokuwa kwenye mini bus wakirusha kitu kuelekea kwenye mkusanyiko wa wakristo waliokuwepo kwenye ibada.
Taarifa zinaeleza kuwa eneo kubwa limetapakaa damu, watu wengi wamejeruhiwa. Inasadikiwa kuwa wapo waliokufa lakini haijathibitika. Muda huu vyombo vyote vya usalama vipo eneo la tukio.
Kwa update zaidi sikiliza Radio Mariahttp://streema.com/radios/play/6848.
Hivi sasa kuna taharuki kubwa, na kuna taarifa ya milipuko mingine, haijulikani kama ni ya washambuliaji au ya polisi, mbali na eneo la ibada.
Nawapeni pole nyingi waliokumbwa na mkasa huu, wakatoliki, wakristo wote na wanaolitakia amani Taifa letu.
Taarifa kutoka mkoani Arusha ambazo mtandao huu umezipata zinaeleza kuwa kuna mlipuko mkubwa mfano wa bomu umejitokeza katika kanisa la RC Arusha na kujeruhi baadhi ya waumini.
Mlipuko huo unadaiwa kusababisha taharuki kubwa katika mji wa Arusha na kuendelea kuiweka nchi katika hali tete zaidi .
mwandishi maalum wa mtandao huu kutoka Arusha anasema kuwa tukio hilo limetokea katika parokia ya Olasit mjini Arusha na bado jitihada za uokoaji zinaendelea kufanyika.
No comments:
Post a Comment