.
.
Wednesday, September 24, 2008
MANJI AJITOA
MKURUGENZI Mtendaji wa Kampuni ya Quality Group, Yusuf Manji, amejitoa katika nafasi ya kuwa mmoja wa wawakilisha wa Tanzania katika mkutano wa wafanyabiashara wenye mchango kiuchumi katika nchi zao kutoka Afrika na wengine wa nchi za Ulaya.
Uamuzi huo umekuja siku chache baada ya nafasi hiyo ya Manji kuibua mjadala, huku baadhi ya watu wakihoji sababu za mfanyabiashara huyo kupewa nafasi hiyo kubwa ya kuwa mmoja wa wawakilisha wa nchi.
Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Manji alisema ameamua kuchukua uamuzi huo baada ya kuona amekuwa akichafuliwa jina lake na baadhi ya watu na vyombo vya habari nchini.
Manji ambaye alitajwa na kusifiwa na gazeti la The Econimist kama mfanyabiashara maarufu ambaye ana mchango mkubwa kwa uchumi wa Tanzania, alisambaza nakala ya barua ya uamuzi huo kwenda kwa Rais Jakaya Kikwete na waandaji, mjini Vienna, Austria.
Alisema uamuzi huo unatokana na taarifa za kumchafua ambazo zimekuwa zikiandikwa na magazeti matatu ya kila siku.
"Baada ya kupitia matukio ya hivi karibuni kwa kina, kwa heshima na taadhima nimeamua kutoa jina langu katika orodha. Uamuzi huo nimeufikia mwenyewe baada ya kuona nashutumiwa sana."
Manji alisisitiza kuwa kuingizwa kwake katika orodha hiyo kulitokana na uzoefu na mchango wake wa kuimarisha sekta binafsi kwa kuunganisha sekta ndogo na kubwa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment